WALENGWA TASAF WATAKIWA KUJIUNGA KWENYE VIKUNDI



Walengwa wa mfuko wa Maendeleo ya jamii TASAF111 wenye mpango wa kunusuru kaya maskini Shinyanga vijijini, wametakiwa kujiunga kwenye vikundi vya ujasiriamali, ili waweze kuzungusha fedha wanazozipata kibiashara na kujiwekea akiba, hali ambayo itawafanya waweze kuinuka kiuchumi pale mradi huo utakapo koma kutoa fedha hizo kwao.


Hayo yalibainishwa na meneja wa Tathimini TASAF kutoka makao makuu Jijini Dar es salaam Farij Mishael, wakati wakitembelea walengwa wa Kaya Maskini Katika Vijiji vya Isela ,Singita na Bukene Shinyanga vijijini, kwa lengo la kuona maendeleo ya fedha hizo namna zinavyotumika kuondoa umaskini kwa wananchi.

Alisema ni vyema walengwa hao wakajiunga kwenye vikundi hivyo vya ujasiriamali, ambapo pale mradi huo utakapokoma kutolewa fedha kwao wakawa na biashara ndogondogo, ambazo zitawaendeleza kuwapatia fedha na kuinuka kiuchumi ili wasipate kurudi kwenye hali ya umaskini walipotoka.

“Mradi huu wa TASAF awamu ya Tatu katika halmashauri ya Shinyanga vijijini ulianza mwaka 2015 na unatarajiwa kukoma mwakani, hivyo na waomba walengwa wote mlionufaika na mradi huu mjiunge kwenye vikundi vya ujasiriamali, mpate kufungua biashara na miradi mbalimbali ya kiuchumi”alisema Mishael.

Naye mmoja wa wanufaika wa mradi huo Bestina Mhoja, aliipongeza TASAF kwa kwa kuweza kuwainua kiuchumi na kuwatoa kwenye dimbwi la umaskini, na kuomba ombi waongezewe mwaka tena kuendelea kulipwa fedha hizo, ili waendelee kujiimarisha kiuchumi kwa kuanzisha miradi hiyo ya kibiashara.

Alisema tangu aanze kupokea fedha hizo za TASAF mwaka (2015), amepata faida ya kujenga nyumba ya bati, kununua mbuzi Nane, Kondoo Mmoja, na Kuku Saba, na kutoa ahadi ya kujiunga kwenye vikundi ili kuanzisha biashara ndogondogo ambayo itamsaidia kuendelea kuinuka kiuchumi.

Kwa upande wake Mratibu wa TASAF halmashauri ya wilaya ya Shinyanga vijijini Happnes Shayo, alisema jumla ya Kaya 8787 zimenufaika na Mradi huo, na kubainisha kuwa jumla ya Shilingi Bilioni 5,519,652,000zimeshatolewa kwa walengwa hao hadi mwezi marchi mwaka huu.

TAZAMA HABARI PICHA HAPA CHINI 


Meneja wa Tathimini TASAF kutoka makao makuu Jijini Dar es salaam Farij Mishael, akizungumza na wanufaika wa mpango huo wa kunusuru Kaya maskini juu ya kuanzisha miradi ya uzalishaji mali, ambayo itawasidia kujikwamua kiuchumi na kuondokana na umaskini kabisa na kutokurudi kama zamani.

Mratibu wa TASAF kutoka Benki ya dunia nchini Marekani ( Program Cordinator) Krishina Pidatala, akizungumza na walengwa hao wa TASAF Shinyanga vijijini, na kuwataka fedha wanazozipata wazitumie, kwa madhumuni yaliyokusudiwa ili wapate kuondokana na umaskini.

Walengwa wa TASAF katika kijiji cha Isela Kaya ya Samuye Shinyanga vijijini, wakiwa kwenye mkutano wa wadau wa maendeleo na wafadhili wa mradi huo, wakisikiliza Nasaha mbalimbali ambazo zitawafanya kuendelea kujikwamua kiuchumi pindi mradi huo utakapokoma kutoa fedha tena kwao.

Walengwa wa TASAF katika kijiji cha Singita Kata ya Usanda Shinyanga vijijini, wakiwa kwenye mkutano wa wadau wa maendeleo na wafadhili wa mradi huo.

Wanafunzi wa shule ya msingi Isela Kata ya Samuye Shinyanga vijijini nao wakiwa kwenye mkutano huo wa TASAF .

Grace Mwebeha ni mnufaika wa mradi huo wa TASAF katika kijiji cha Isela Kata ya Samuye Shinyanga vijijini, akielezea faida aliyoipata tangu aanze kupewa fedha hizo za TASAF mwaka 2015, kuwa amejenga nyumba ya Bati, ana mbuzi watatu, anasomesha watoto shule na kuwatimizia mahitaji yao, na pia anawapeleka Clinic na ameshajiunga na mfuko wa bima ya afya CHF.

Mhoja Charles ni Mnufaika wa mradi huo wa TASAF katika kijiji cha Isela Kata ya Samuye Shinyanga vijijini naye akielezea mfanikio aliyoyapata, kuwa ana Kondoo 10, Mabati 30 na pia amejiunga na CHF.

Magdalena Shija ambaye ni mlegwa wa TASAF akiipongeza kwa kuwatoa kwenye dimbwi la umaskini na kutoa maombi Muda uongezwe Pamoja na  fedha ziongezwe ili waendelee kujiimarisha zaidi hasa kwenye kufungua miradi ya kiuchumi.
Wanafunzi wa shule ya msingi Isela Kata ya Samuye Shinyanga vijijini wakiwa kwenye mkutano huo wa TASAF.

Wadau wa maendeleo kupitia mpango huo wa kunusuru Kaya Maskini TASAF wakielekea kwenye Kaya za walengwa kuangalia maendeleo waliyoyapa tangu kupewa fedha hizo Mwaka 2015 kwa awamu 17.

Ester Maganga ambaye ni Mnufaika wa TASAF katika kijiji cha Isela Kata ya Samuye akiwa kwenye nyumba yake ya Bati ambayo ameijenga kupitia fedha za TASAF.

Ester Maganga ambaye ni Mnufaika wa TASAF katika kijiji cha Isela Kata ya Samuye akionyesha nyumba yake ya Zamani ya Nyasi, ambayo alikuwa akiishi kabla ya kuungwa kwenye mradi huo wa kunusuru Kaya maskini  ambapo kwa sasa ana fugia Nguruwe wawili.

Nguruwe wa mnufaika wa TASAF Ester Maganga wakionekana ndani ya nyumba ya majani ambayo amehama mara baada ya kujenga nyingine ya Mabati.

Ester Maganga akionyesha Ng'ombe wake watatu ambao amewapata kupitia fedha za TASAF.

Bestina Mhoja ambaye ni mnufaika wa TASAF akionyesha mbuzi wake Nane na Kondoo Mmoja ambao amewapata kupitia fedha za TASAF, huku pia akiwa na nyumba ya Bati ,pamoja na Kuku Saba.

Meneja wa Tathimini kutoka TASAF makao makuu Jijijni Dar es Salaam Fariji Mishael (wa kwanza mkono wa Kushoto) akiwa na Mratibu wa mradi huo wa Tasaf kutoka Benk ya Dunia Krishina Pidatala, pamoja na familia ya Bestina Mhoja ambaye ni mnufaika wa mpango huo wa Tasaf wa kunusuru Kaya Maskini.

Meneja wa Tathimini kutoka TASAF makao makuu Jijini Dar es Salaam Fariji Mishael (wa kwanza mkono wa Kulia) akiwa na Mratibu wa mradi huo wa Tasaf kutoka Benk ya Dunia Krishina Pidatala, wakijadili mawili matatu wakati wakifuatilia maendeleo ya walengwa hao wa TASAF.

Mhoja Charles ambaye ni mnufaika wa TASAF katika kijiji cha Isela Kata ya Samuye akionyesha Mabati 30 ambayo ameyapata kupitia fedha za TASAF na anatarajia naye kujenga Nyumba ya Bati.

Mhoja Charles ambaye ni mnufaika wa TASAF katika kijiji cha Isela Kata ya Samuye akionyesha Kondoo wake 10 ambao amewapata kupitia fedha hizo za TASAF.

Kondoo wa Mhoja Charles kama unavyowaona.

Mhoja Charles ambaye ni Mnufaika wa Tasaf mkono wa Kulia akiwa na mkewake wakiswaga Kondoo ambao wamewapata kupitia TASAF.

Wadau wa maendeleo na wafadhili wa mradi huo wa TASAF Wakikusanya maoni kwa walengwa hao, ili wapate kuuboresha zaidi mpango huo wa kunusuru Kaya maskini na kuwainua kiuchumi.

Maoni yakiendelea kukusanywa.

Maoni yakiendelea kukusanywa kutoka kwa walengwa hao wa TASAF.

Ukusanyaji maoni ukiendelea.

Ukusanyaji maoni ukiendelea.

Maoni yakiendelea kukusanywa.

Mtendaji wa kijiji cha Isela Kata ya Samuye Shinyanga vijijini Bundini Mungo, akisoma taarifa ya kijiji hicho amesema jumla ya walengwa 72 ndio wananufaika na mradi huo sawa wakazi 432, jinsia ya Kike wakiwa 218,Kiume 214 na mpaka sasa jumla ya fedha Shilingi Milioni 46,524,000 zimeshatolewa kwa walengwa hao katika awamu 17 tangu mwaka 2015.

Mtendaji wa Kijiji cha Bukene Kata ya Bukene Tarafa ya Itwangi Shinyanga vijijini Charles Mayunga, akitoa taarifa ya TASAF Kwenye kijiji hicho kuwa jumla ya Kaya 80 ndio zipo kwenye mradi huo, jinsia ya kiume wakiwa 221,Kike 208 na kubainisha kuwa jumla ya Shilingi Milioni 49,492,000 zimeshatolewa kwa walengwa hao tangu mwaka huo 2015.

Josiah Colonel ni mtendaji wa Kijiji cha Singita Kata ya Usanda Shinyanga vijijini, akisoma taarifa ya TASAF kijijini humo, amesema jumla ya walengwa 106 ndio wananufaika na Mpango huo, Jinsia ya Kike wakiwa 45 na Kiume wakiwa 61 ambapo jumla ya Shilingi Milioni 100,504,000 zimeshatolewa kwa walengwa hao.

Mratibu wa TASAF halmashauri ya wilaya ya Shinyanga vijijini Happnes Shayo, anasema jumla ya Kaya 8787 zimenufaika na Mradi huo, na kubainisha kuwa jumla ya Shilingi Bilioni 5,519652,000 zimeshatolewa kwa walenga hao hadi mwezi April mwaka huu.

Kikundi cha Ngoma cha Ugoyangi kutoka Kijiji cha Usule Kata ya Bukene Shinyanga vijijini wakitoa Burudani kwenye mkutano huo wa TASAF wa kufanya Tathimini ya mradi huo kwa walengwa, na namna wanavyonufaika nao na kuwatoa kwenye Dimbwi la Umaskini.

Burudani zikiendelea kwa kuonyesha utaalamu wa kucheza na Nyoka.

Kikundi cha Ngoma cha Jembe kutoka kijiji hicho cha Bukene Shinyanga vijijini kikijiandaa kutoa burudani.

Kikundi cha Jembe kikitoa burudani.

Mratibu wa TASAF Halmashauri ya Shinyanga Vijijini Happnes Shayo akifurahia jambo.

Burudani zikiendelea.

Kikundi cha Ngoma ya Ugoyangi wakiendelea kutoa burudani katika kijiji cha Bukene leo, wakati wa ufangaji mkutano wa Tathimini na uchukuaji maoni nini kiboreshwe kwenye mradi huo wa TASAF kipindi kijacho.

Burudani zikiendelea.

Mwandishi wa Habari Gazeti la Dailynews Suleiman Shaghata mkono wa kulia akibadilishana mawazo na Mratibu wa TASAF Kutoka Benk ya Dunia ( Program Coordinator) Krishina Pidatala.

Mratibu wa TASAF Kutoka Benk ya Dunia ( Program Coordinator) Krishina Pidatala akipokea Zawadi kutoka kwa walengwa wa TASAF ,Sanamu ya Rais John Pombe Magufuli.

Zawadi.

Pokea Zawadi.

Burudani zikifunga mkutano huo wa TASAF katika kijiji cha Bukene Shinyanga vijijini.

Na Marco Maduhu ambaye pia ni Mwandishi wa Gazeti la Nipashe mkoani Shinyanga.


















Powered by Blogger.