WANNE MBARONI SHINYANGA WAKISAFIRISHA BANGI KILO 98
Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga, linawashikilia watu wa Nne kwa tuhuma ya kukamatwa wakisafirisha madawa ya kulevya aina ya Bangi, kwenye viroba vitano ikiwa na uzito wa kilo 98 kutoka Kata ya Kagongwa wilayani Kahama mkoani hapa kwenda Jijini Dar es salaam.
Akitoa taarifa leo Aprili 16, 2018 kwa vyombo vya habari Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Kamishina msaidizi wa Polisi Simoni Haule, alisema watu hao walikamatwa jana April 15 majira ya saa 12 asubuhi katika geti la maliasiri barabara ya Kahama, Tinde Kata ya Itogwanholo wilaya ya Kipolisi Msalala.
Aliwataja watu hao kuwa ni Simon Juma Kashindye (46) mkazi wa Nyanshimbi Shinyanga vijijini, Lameck Nicombolwe (44) Kulwa Nelson (21), na Shabani Nurdin(20), wote hao watatu wakiwa wakazi wa Jijini Dar es salaam ,wakisafirisha Bangi hiyo kwa kutumia gari lenye namba za usajili T 872 CVS Coaster mali ya Precabi mkazi wa Dar es salaam.
“Bangi hii kama mnavyoiona imefungwa kwenye viroba 5 na inauzito wa Kilo 98 na watuhumiwa hawa walikuwa wakisafirisha kwenda Jijini Dar es salaam kwa kutumia gari hiyo ya abiria, na tunaendelea kuwashikilia kwa mahojiano zaidi na uchunguzi ukikalimika wata fikishwa mahakamani kuchukuliwa hatua za Kisheria,” alisema Haule.
“Na uchunguzi ukikamilika na watu hawa watafikishwa mahakamani kuchukuliwa hatua kali za kisheria, na mahakama ndio itatoa amri ya Bangi hii kuharibiwa, nasi ndipo tutakapoiteketeza kwa Moto,” aliongeza.
Naye mmoja wa watuhumiwa hao Lameck Nicombolwe ambaye ni Dereva wa Gari hilo, alisema wao walikodiwa kuleta msiba katika Kata hiyo ya Kagongwa, ndipo wakapata tenda ya kupakia Bangi hiyo na kuambiwa kuwa ni Tumbaku, lakini walishaghaa muhusika wa mzigo huo ghafla ana shuka kwenye gari na kutokomea huku wao wakikamatwa.
Aidha kufuatia tukio hilo Kamanda alitoa wito kwa wananchi mkoani Shinyanga, kuachana na tabia ya kujihusisha na biashara haramu, pamoja na kushirikiana na Jeshi hilo kutoa taarifa za waharifu ili wapate kushughulikiwa mapema na mkoa ubaki kuwa salama.
TAZAMA MATUKIO KATIKA PICHA HAPA CHINI
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Kamishina msaidizi wa Polisi Simoni Haule akielezea namna walivyokamata madawa hayo ya kulevya aina ya Bangi.
Askari wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga wakikagua viroba ambavyo vina madawa hayo ya kulevya aina ya Bangi Kilo 98.
Askari wa jeshi la Polisi mkoani Shinyanga wakifungua Viroba vitano walivyo vikamata vikiwa na madawa hayo ya kulevya aina ya Bangi.
Bangi ikionekana kwenye Kiroba.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Shinyanga Kamishina msaidizi wa Polisi Simoni Haule, akihoji watuhumiwa waliokamatwa na madawa hayo ya kulevya aina ya Bangi.
Lameck Nicombolwe ambaye ni Dereva wa Gari hilo, alisema wao walikodiwa kuleta msiba katika Kata hiyo ya Kagongwa, ndipo wakapata tenda ya kupakia Bangi hiyo, na kuambiwa kuwa ni Tumbaku, lakini walishaghaa muhusika wa mzigo huo ghafla ana shuka kwenye gari na kutokomea huku wao wakikamatwa.
Watuhumiwa waliokamatwa na madawa hayo ya kulevya aina ya Bangi wakijieleza, wakanza kushoto ni Lameck Nikombolwe (44) ambaye ni Dereva na Mkazi wa Dar es salaam, Simon Juma Kashindye (46) mkazi wa kijiji cha Nyanshimbi Shinyanga vijijini.
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga kamishina msaidizi wa Polisi Simoni Haule, akionyesha gari aina ya Toyota Coaster yenye namba za usajili T. 872 CVS Mali ya Precabi mkazi wa Jijini Dare es salaam ambayo imetumika kusafirisha madawa hayo ya kulevya aina ya Bangi.
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Kamishina msaidizi wa Polisi Simon Haule akitoa taarifa hiyo ya kukamata madawa hayo ya kulevya aina ya Bangi kwa vyombo vya habari.
Baadhi ya waandishi mbalimbali wa vyombo vya habari mkoani Shinyanga wakiwa katika press conference na Jeshi la Polisi juu ya kukamatwa kwa madawa hayo ya kulevya aina ya Bangi.
Baadhi ya waandishi mbalimbali wa vyombo vya habari mkoani Shinyanga wakiwa katika press conference na Jeshi la Polisi juu ya kukamatwa kwa madawa hayo ya kulevya aina ya Bangi.
Na Marco Maduhu ambaye pia ni mwandishi wa Gazeti la Nipashe mkoani Shinyanga