SHIRIKA LA AGAPE LAENDESHA KONGAMANO ELIMU YA AFYA YA UZAZI NA UJINSIA KWA WANAFUNZI 120
Shirika la Agape AIDS Control Programme (AACP) limeendesha kongamano kwa wanafunzi 120 kutoka shule nane zilizopo katika kata Usanda halmashauri ya wilaya ya Shinyanga (Vijijini) kwa lengo la kuwajengea uelewa wanafunzi kuhusu masuala ya afya ya uzazi na ujinsia, ilikujiepusha na masuala ya ngono katika umri mdogo.
Kongamano hilo lililoongozwa na mdahalo wenye mada "Je Kijana akibalehe/akivunja ungo anakuwa tayari kuoa/kuolewa au kufanya ngono?" limefanyika leo Jumapili Mei 13,2018 katika ukumbi wa Ibanza Hotel uliopo mjini Shinyanga.
Mbali na kuongozwa na mada hiyo,pia wanafunzi hao wameonesha michezo kadha wa kadha huku mada mbalimbali zikitolewa ikiwemo huduma rafiki kwa vijana,ukatili wa kijinsia na madhara yake,majukumu ya afisa ustawi wa jamii na mazingira rafiki shuleni pamoja na umuhimu wa michezo.
Awali akizungumza, Afisa Mradi wa Elimu ya Afya ya Uzazi na Ujinsia kwa Vijana unaotekelezwa na shirika la AGAPE kwa ufadhili wa shirika la Kimataifa la Sida kutoka SWEDEN , Lucy Maganga alizitaja shule hizo kuwa ni shule za msingi Busanda,Nzagaluba,Manyada,Shingida,Shabuluba na shule za sekondari Usanda,Singita na Samuye.
“Mdahalo huu umelenga kuwajengea uelewa wanafunzi kujiepusha na tabia hatarishi zinazoweza kusababisha wapate mimba wakiwa shuleni na magonjwa ya zinaa ukiwemo Ukimwi”,alieleza.
Kwa upande wake,Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Agape, John Myola alisema vitendo vya ukatili dhidi ya watoto vinasababisha ndoto za watoto kutotimia hivyo kuitaka jamii kuungana katika kuhakikisha haki za watoto zinalindwa.
“Masuala ya ukatili yameumiza sana watoto,yamekatisha ndoto zao na wakati mwingine kusababisha madhara ya kudumu kwa watoto yakiwemo ya kimwili na kisaikolojia,lazima jamii ibadilike ili kuwalinda watoto hawa”,alisema Myola.
Katika hatua nyingine aliwataka wazazi na walezi kutengeneza urafiki na watoto ili kujua matatizo wanayokutana nayo ikiwemo kufanyiwa ukatili na watu wa karibu waliopo katika jamii inayowazunguka.
Naye Afisa Elimu kata ya Usanda Essero Ashery alisema ataendelea kuhamasisha walimu na viongozi mbalimnbali kutoa elimu juu ya masuala ya afya ya uzazi na ujinsia kwa vijana huku akiwataka wazazi,walezi na walimu kuangalia aina za adhabu kwa watoto na kuhakikisha wanawapatia muda wa kucheza.
Nao washiriki wa kongamano walikubaliana kuendelea kutoa elimu ya uzazi na masuala ya ukatili dhidi ya watoto kwa wanafunzi wengine na jamii kwa ujumla ili kuhakikisha kuwa watoto wanapata haki zao.
Tazama picha za matukio yaliyojiri wakati wa mdahalo huo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la AGAPE, John Myola akifungua mdahalo uliokutanisha pamoja wanafunzi 120 kutoka shule 8 zilizopo katika kata ya Usanda halmashauri ya wilaya ya Shinyanga katika ukumbi wa Ibanza Hotel Mjini Shinyanga.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la AGAPE, John Myola akifungua mdahalo akifungua mdahalo huo ambapo aliwataka wanafunzi hao kuepuka tabia hatarishi zinazoweza kusababisha wakatishe masomo yao mfano kupata mimba wakiwa shuleni.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la AGAPE, John Myola akizungumza ukumbini. Kushoto ni Afisa Elimu kata ya Usanda Essero Ashery, kulia ni Afisa Maendeleo ya Jamii halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Atupokile Maseta aliyehudhuria mdahalo huo kwa niaba ya Afisa Ustawi wa jamii wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Wanafunzi wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la AGAPE, John Myola ukumbini.
Wanafunzi wakifurahia jambo ukumbini.
Wanafunzi wakiendelea kufuatilia matukio ukumbini.
Afisa Mradi wa Elimu ya Afya ya Uzazi na Ujinsia unaotekelezwa na shirika la AGAPE ,Lucy Maganga akielezea malengo ya mdahalo huo wenye mada isemayo "Je Kijana akibalehe/akivunja ungo anakuwa tayari kuoa/kuolewa au kufanya ngono?".
Afisa Mradi wa Elimu ya Afya ya Uzazi na Ujinsia unaotekelezwa na shirika la AGAPE ,Lucy Maganga akitoa mwongozo wa kuchangia mada ya '"Je Kijana akibalehe/akivunja ungo anakuwa tayari kuoa/kuolewa au kufanya ngono?".
Mwanafunzi kutoka shule ya sekondari Shingita,Kashindye Shija akichangia mada ukumbini
Mwanafunzi kutoka shule ya msingi Shabuluba, Philipo Jacob akichangia mada wakati wa mdahalo huo.
Mwanafunzi kutoka shule ya sekondari Samuye, Veronica John akichangia mada wakati wa mdahalo huo.
Mwanafunzi kutoka shule ya sekondari Usanda,Philipo Malale akichangia mada ukumbini.
Afisa Maendeleo ya Jamii halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Atupokile Maseta kwa niaba ya Afisa Ustawi wa jamii wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga akitoa mada kuhusu majukumu ya afisa ustawi wa jamii.Alisema miongoni mwa majukumu hayo ni pamoja na kuhakikisha ulinzi na usalama kwa watoto.
Kulia ni mwanafunzi wa shule ya sekondari Samuye akimuuliza swali Atupokile Maseta kuhusu hatua zipi zinachukuliwa endapo mzazi atatekeleza familia yake.
Afisa Elimu kata ya Usanda Essero Ashery akitoa mada kuhusu Mazingira salama kwa wanafunzi shuleni na umuhimu wa michezo kwa wanafunzi.
Mwanafunzi akielezea umuhimu wa michezo kwa watoto.
Wanafunzi wa shule ya Msingi Nzagaluba wakiimba wimbo kuhusu masuala ya ukatili dhidi ya watoto.
Wanafunzi wa shule ya Msingi Manyada wakiimba ngonjera.
Wanafunzi wa shule ya Sekondari Samuye wakiimba shairi.
Wananfunzi wakicheza muziki ukumbini.
Afisa ulaghabishi wa shirika la AGAPE, Dotto Wayala akicheza muziki na wanafunzi ukumbini.
Muziki umekolea: Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la AGAPE, John Myola akikata viuno wakati wanafunzi wakicheza muziki ukumbini.
Kushoto ni Afisa Mradi wa Elimu ya afya ya uzazi na ujinsia ,Lucy Maganga naye akionesha uwezo wa kucheza muziki.
Wanafunzi wa shule ya sekondari Shingita wakifuatilia matukio ukumbini.
Wanafunzi wa shule ya sekondari Usanda wakionesha mchezo wa igizo kuhusu nafasi ya mtoto wa kike katika jamii.
Wanafunzi wa shule ya msingi Shingida wakicheza ukumbini
Walimu wakifurahia jambo ukumbini.
Walimu wakifuatilia matukio ukumbini.
Walimu wakiwa ukumbini.
Wafanyakazi wa shirika la AGAPE wakifurahia jambo ukumbini.
Wanafunzi wa shule ya sekondari Samuye wakionesha mchezo wa igizo.
Wanafunzi wakicheza muziki.
Wanafunzi wa shule ya sekondari Shingita wakicheza ukumbini
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la AGAPE, John Myola akitoa mada kuhusu masuala ya ukatili.
Kijana Samson Mtesigwa akitoa burudani ya wimbo maalumu kuhusu umuhimu wa kupeleka watoto shule.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog