CHADEMA KUDAI BAJETI YA KATIBA MPYA NJE YA BUNGE



Chama cha demokrasia na maendeleo Chadema, kimedai kwenda kuanzisha mjadala nje ya bunge wa kudai bajeti ya mchakato wa katiba mpya, ambayo ndio itakuwa mkombozi kwa wananchi, sababu kutakuwepo na uwajibikaji wa viongozi wa Serikali ipasavyo na kutokuwapo kwa muingiliano wa kiutawala.


Imeelezwa kuwa katika uwasilishwaji wa bajeti za wizara mbalimbali Bungeni Jijini Dodoma, bajeti ya mchakato wa kuundwa katiba mpya haipo, ambayo ndiyo ilipaswa kupewa kipaumbele na kutengewa fedha za kutosha, ikiwa ndio itakuwa muongozo mzuri wa kunyoosha nchi.

Hayo yalibainishwa jana Mei 19,2018 na Naibu Katibu mkuu Taifa kutoka Chadema John Mnyika, wakati akitoa hotuba kwenye ufunguzi wa kikao cha baraza la mashauriano ya Chadema mkoani Shinyanga lililohusisha wajumbe kutoka majimbo sita ya mkoa huo ambayo ni Msalala, Ushetu, Kahama , Solwa, Kishapu na Shinyanga mjini.

Alisema katika makabrasha yote aliyopitia ya uwasilishwaji wa bajeti za wizara mbalimbali Bungeni Jijini Dodoma, hakuna bajeti iliyotengwa ya kuwepo kwa mchakato wa kuendelea kwa katiba mpya, jambo ambalo limewashaghaza na hivyo kuwataka wabunge wote hadi wa (CCM) Kuungana kwa pamoja kuidai bajeti hiyo iwepo.

“Sisi kama chadema hivi sasa tuna wauliza kwanza wananchi kwenda kuidai bajeti ya katiba mpya, na baada ya hapo tutakwenda bungeni kuanzisha mjadala nje ya bunge wa kuidai bajeti hiyo ambayo ndio itakuwa dira ya nchi yetu, kuliko hivi sasa nchi imekosa uelekeo na wanchi wa hali ya chini kuendelea kuumia,”alisema Mnyika.

“Hata sasa hivi bajeti ambazo zinaendelea kuwasilishwa bungeni, hazina nia kabisa ya kumsaidia mwananchi bali zinamkandamiza zimekuwa finyu mno, na yote haya ni sababu ya mfumo wa utawala kuwa mbovu,”aliongeza.

Naye Makamu mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Serengeti Gimbi Masaba, akizungumza kwenye mkutano huo kabla ya kumkaribisha John Mnyika, alisema lengo lake ni kukijenga chama katika kuelekea chaguzi zijazo za (2019-20), ilikupata viongozi wengi na hatimaye kushika dola.

Aidha aliwataka wajumbe wote waliohudhulia mkutano huo, kuwa maadhimio ambayo watakubaliana wakayatekeleza ipasavyo wala kutoteteleka, ikiwa katika harakati za kukijenga chama na kutafuta ukombozi wanchi inahitaji mtu kuwa shupavu na mwenye misimamo thabiti.

TAZAMA HABARI PICHA HAPA CHINI


Naibu katibu mkuu Chadema Taifa John Mnyika akizungumza na wajumbe wa baraza la mashaurinao Chadema mkoa wa Shinyanga kuwa wasiwe na hofu juu ya matukio ambayo  wamekuwa wakitendewa viongozi wa kisiasa bali waendelee kuwa na misimamo katika kuikomboa nchi.
Makamu mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Serengeti Gimbi Masaba, akizungumza kwenye mkutano huo kabla ya kumkaribisha John Mnyika, amesema lengo la mkutano huo ni kukijenga chama katika kuelekea chaguzi zijazo za (2019-20), ilikupata viongozi wengi na hatimaye kushika dola.
Aidha aliwataka wajumbe wote waliohudhulia mkutano huo, kuwa maadhimio ambayo watakubaliana wakayatekeleza ipasavyo wala kutoteteleka, ikiwa katika harakati za kukijenga chama na kutafuta ukombozi wanchi inahitaji mtu kuwa shupavu na mwenye misimamo dhabiti.

Kaimu mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Shinyanga Wiliamu Shayo ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Ndala manispaa ya Shinyanga akifungua mkutano huo wa baraza la mashauriano Chadema mkoa wa Shinyanga.

Viongozi wa Chadema taifa na mkoa wa Shinyanga wakisimama kwa dakika moja kumkumbuka Marehemu Geogre Kitalama ambaye alikuwa Katibu wa Chadema wilaya ya Shinyanga mjini.

Wajumbe wa mkutano huo nao wakisimama kwa dakika moja kumkumbuka Marehemu Geogre Kitala ambaye alikuwa Katibu wa Chadema wilaya ya Shinyanga na alishanga wahi kuwa diwani wa Kata ya Kitangili manispaa ya Shinyanga.

Katibu wa Kanda ya Seregenti (Chadema) Renatus Nzemo akitambulisha viongozi wa Kitaifa kabla ya mkutano huo kuanza ambapo Kanda hiyo inajumuisha mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga ambapo makao yake makuu yapo mjini Shinyanga.

Wajumbe wakiwa kwenye mkutano wao wa Baraza la mashauriano mkoa wa Shinyanga, kwa kukutana wajumbe kutoka majimbo Sita ambayo ni Msalala, Ushetu, Kahama, Kishapu, Solwa na Shinyanga mjini.

Wajumbe wakiendelea na mkutano wao wa kukijenga chama katika kuelekea harakati za ukombozi wa kushika dola.

Wajumbe wakiendelea kuchuka mawili matatu kwa ajili ya kwenda kuyafanyia kazi ili chama kipate fursa ya kushika dola kwa kupewa ridhaa na wananchi.

Wajumbe wakiendelea kuchuka mawili matatu kwa ajili ya kwenda kuyafanyia kazi ili chama kipate fursa ya kushika dola kwa kupewa ridhaa na wananchi.

wajumbe wakiendelea na mkutano.

Wajumbe wakiendelea kuchuka mawili matatu kwa ajili ya kwenda kuyafanyia kazi ili chama kipate fursa ya kushika dola kwa kupewa ridhaa na wananchi.

Makamu mwenyekiti wa Kanda ya Serengeti Gimbi Masaba ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu mkoani Simiyu, wakiteta jambo na Naibu Katibu mkuu Chadema Taifa John Mnyika kwenye mkutano huo.

Wajumbe wakiendelea kuchuka mawili matatu kwa ajili ya kwenda kuyafanyia kazi ili chama kipate fursa ya kushika dola kwa kupewa ridhaa na wananchi.

Katibu wa Chadema mkoa wa Shinyanga Zacharia Obadi akitambulisha wajumbe na wageni waalikwa waliofika kwenye mkutano huo.

Wajumbe wakiendelea na mkutano.

Mkutano ukiendelea.

Wajumbe wakiendelea na mkutano wa baraza la mashauriano ya Chadema mkoa wa Shinyanga.

Mkutano ukiendelea.

Naibu Katibu mkuu  Chadema Taifa John Mnyika mkono wa Kushoto akiwa na Makamu Mwenyekiti Kanda ya Serengeti Gimbi Masaba, wakati akiingia kwenye ukumbi tayari kuanza kwa mkutano huo wa baraza la mashauriano Chadema mkoa wa Shinyanga.
Na Marco Maduhu, ambaye pia ni Mwandishi wa Gazeti la Nipashe mkoani Shinyanga.































Powered by Blogger.