KAMPUNI BUBU SHINYANGA YAFUNGWA KWA UTAPELI NA KUNYANYASA WAFANYAKAZI WAKE
Ofisi ya mwenyekiti wa mtaa wa Dome kilipofanyika kikao hicho cha kufunga Kampuni hiyo Bubu ya New Vission
SOMA HABARI KAMILI
Kaimu mtendaji wa Kata ya Ndembezi manispaa ya Shinyanga Jakson Njau ambaye ni Ofisa maendeleo ya jamii kwenye Kata hiyo, ameizui Kampuni bubu ya kuuza bidhaa mbalimbali vikiwamo vipodozi, kutofanya kazi zake mara baada ya kuendeshwa kiujanja na kunyanyasa wafanyakazi wake.
Imeelezwa Kampuni hiyo yenye jina la New Vission ambayo ofisi zake zipo mtaa wa Dome Kata ya Ndembezi manispaa ya Shinyanga, ilianza kufanya kazi zake Kinyemela mjini hapa mwaka jana, pamoja na kuajiri wafanyakazi hasa mabinti kutoka mikoa mbalimbali kwa kufanya kazi za kuuza bidhaa kwa kutembeza.
Akizungumza jana Mei 23, 2018 kwenye kikao maalumu cha wafanyakazi wa Kampuni hiyo Bubu na wamiliki wake kilicho fanyika kwenye Ofisi ya Mwenyekiti wa mtaa wa Dome, Njau alisema marufuku kufanya kazi zake mjini humo mpaka pale itakapokamilisha kufuata taratibu zote za Kiserikali pamoja na kulipa kodi.
“Kampuni hii inafanya kazi Kinyemela haitambuliki Serikalini wala kwa mwenyekiti wa mtaa, na wanalaza mabiti Sita kwenye Chumba Kimoja pamoja na wamiliki kuishi nao, jambo hili halikubaliki fuateni utaratibu ndipo tutawaruhusu kufanya kazi zenu,”alisema Njau.
Naye mwenyekiti wa Mtaa huo wa Dome ambapo Kampuni hiyo mahali ilipo, Solomo Najulwa alisema baada ya kupokea malalamiko ya manyanyaso ya wafanyakazi hao ndipo akaifahamu, na hivyo kuamua kuwaita ilikuijua na kubainika kufanya kazi zake Kinyemela.
Nao wafanyakazi wa Kampuni hiyo ambao wanatoka Kigoma, Simiyu, Kahama, Kagera na Shinyanga, waliishukuru Serikali kwa kuwasaidia kuwatatulia matatizo yao pamoja na kupewa nauli za kurudi makwao, ikiwa kwenye matangazo waliahidiwa mishahara laki Tatu na Nusu kwa mwezi , na kuambulia kupewa Posho kulingana na mauvo.
Mmoja wa wafanyakazi wa Kampuni hiyo Imani Festo kutoka Kigoma, alisema malipo ya Posho yao yanatokana na mauzo ya bidhaa ambapo akiunza moja pesa yake ni Shilingi Miamoja, ndipo atapigiwa hesabu kwa wiki mbili au mwezi na kulipwa pesa yake , huku hela ya kula mchana hujitegemea na kushinda njaa.
Naye Mmiliki wa Kampuni hiyo Olalifu Michael kutoka Arusha ,alikiri kufanya kazi zake Kinyemela na kuwalipa Posho na siyo mshahara, na kuahidi kutii sheria ya kutouza bidhaa zake, pamoja na kuwapatia Nauli wafanyakazi wake ambao wapo Nane wakiume mmoja, kurudi makwao hadi pale atakapo kamilisha taratibu za Serikali.
Na Marco Maduhu, ambaye pia ni Mwandishi wa Gazeti la Nipashe mkoani Shinyanga.