MILIONI 50 ZA RAIS MAGUFULI ZADAIWA KUVUNJA VIKUNDI VYA UJASIRIAMALI



Ofisa maendeleo ya jamii Kata ya Ndembezi manispaa ya Shinyanga Jackson Njau, amebainisha kuwa vikundi vingi vya ujasiriamali vya akina mama na vijana, vimevunjika sababu ya kukosa fedha za mikopo milioni 50 kwa kila kijiji, ahadi iliyotolewa na Rais John Magufuli katika kipindi cha kampeni kwenye uchaguzi mkuu 2015.


Imedaiwa idadi kubwa ya vikundi hivyo vilikuwa havina malengo ya kujikwamua kiuchumi, ambapo mara baada ya kukosekana kwa fedha hizo Milioni 50 kwa kila kijiji, waliamua kuvunja vikundi vyao, ikiwa wangeweza kuviendeleza kwa kuomba mikopo asilimia 10 fedha za mapato ya ndani ya halmashauri.

Njau alibainisha hayo jana Mei 30,2018  kwenye kikao cha vijana wa mtaa wa Dome Kata ya Ndembezi manispaa ya Shinyanga, kilichoitishwa na mwenyekiti wa mtaa huo Solomoni Najulwa kwa lengo la kuhamasisha vijana kujiunga kwenye vikundi, ili wawe shughuli za kufanya ambazo zitawaingizia kipato na kujikwamua kiuchumi.

Awali akijibu swali lililoulizwa na mmoja wa vijana hao John Kihumbi, kuwa kipindi cha nyuma kuna vikundi vingi viliundwa, lakini gafla vikavunjika bila ya kufanya shughuli za uzalishaji mali, je Serikali imejipangaje kutovunjika tena kwa vikundi, na kupewa majibu kuwa vilivunjika mara baada ya kukosekana kwa Milioni 50 za Magufuli.

“Vikundi vingi kwa kipindi cha nyuma vilikuwa havina malengo ya kujikwamua kiuchumi ambapo lengo lao lilikuwa ni kuchukua mamilioni ya Rais Magufuli na kutokomea, lakini mara baada ya kukosena ndipo vikavunjika, hivyo natoa wito kwenu vikundi mtakavyounda muwe na nia ya kujikwamua kiuchumi,”alisema Njau.

Aliongeza “Serikali imejipanga kuwa kila kikundi kabla ya kupewa fedha, lazima wapewe kwanza semina elekezi namna ya kuzitumia fedha hizo, ndipo wanakabidhiwa kupitia akaunti waliyofungua, njia ambayo itasaidia vikundi vyao kutovunjika pamoja na kuwatembelea mara kwa mara kwenye miradi yao kupewa ushauri.”

Naye Mwenyekiti wa mtaa huo wa Dome Solomoni Najulwa, aliwataka vijana hao kuchangamkia fursa za fedha hizo asilimia 10 za mapato ya ndani ya halmashauri, kwa kuunda vikundi vya watu watano watano, iliwapate kujikwamua kiuchumi na kuachana na dhana tegemezi kutoka kwa wazazi wao huku wengine wakiwa vibaka.

Nao baadhi ya vijana hao walipongeza kutolewa kwa elimu hiyo ya kujiunga kwenye vikundi vya ujasiriamali, na kutoa tahadhali kwa Serikali kudhibiti tatizo la baaadhi ya watu kwenye vikundi kuzungukana, na kwenda kuchukua Pesa Benki bila ya kushirikisha wenzao na kusababisha kuwapo na mpasuko kwenye vikundi.

TAZAMA HABARI PICHA ZAIDI HAPA CHINI


Ofisa maendeleo ya jamii Kata ya Ndembezi manispaa ya Shinyanga Jackson Njau akijibu swali la Kijana John Kihumbi, kuwa kwanini vikundi vingi ambavyo viliundwa mwaka juzi na jana vilikufa bila ya kufanya shughuli ya uzalishaji, na kujibiwa kuwa vikundi hivyo havikuwa na malengo ya kujikwamua kiuchumi bali vilitaka kuchukua fedha Milioni 50 za Rais John Magufuli na baada ya kukosekana kwa fedha hizo ndipo vikavunjika.

John Kihumbi akisikiliza kwa makini Jibu la swali lake alilouliza juu ya vikundi vingi ambavyo viliundwa vya akina mama na vijana mwaka juzi na jana, ambavyo gafla vilivujika na kutaka kujua Serikali imejipangaje katika vikundi vipya ambavyo vitaundwa kutokuvunjika tena.

Vijana wa mtaa wa Dome Kata ya Ndembezi manispaa ya Shinyanga wakisikiliza elimu ya namna ya kujiunga kwenye vikundi vya Ujasiriamali ili wapate kujikwamua kiuchumi na kuachana na dhana tegemezi kutoka kwa wazazi wao.

Ester Mahona akiuliza swali namna ya urejeshaji wa fedha hizo pale watakapopewa mkopo na halmashauri, kuwa watarejesha mmoja mmoja na kujibiwa watapeleka wote wanakikundi.

Vijana wa mtaa wa Dome Kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga wakifurahia Jambo kwenye kikao chao cha kupewa elimu ya kujiunga kwenye vikundi vya ujasiriamali, ili wapate kujiajiri na kuweza hata kufungua viwanda vidogo vidogo.

Issa Stima akiuliza swali kuwa Serikali imejipangaje kudhibiti baadhi ya vikundi ambavyo vimekuwa vikiiba na kutumia katiba na majina ya wenzao kwenda kuombea mikopo huku wengine baadhi kwenye vikundi huzungukana na kwenda kuchukua pesa benki bila kushirikisha wenzao, na kupewa jibu kuwa pale kunapotokea shida hiyo kwa wanakikundi wato taarifa kwenye ofisi ya Kata mapema ili wapate kushughulikiwa mapema, na siyo kukaa nalo na kuanza kulisemea mitaani.

Mwenyekiti wa Mataa wa Dome Kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga Solomoni Najulwa (Cheupe) aliwataka vijana wa mtaa huo wasibweteke kusubilia ajira ,bali watumie fursa hiyo ya kujiunga kwenye vikundi na kupewa mikopo asilimia Tano ambayo haina Riba na kuweza kujikwamua kiuchumi.

Charles Mosha ni mwenyekiti wa Saccos manispaa ya Shinyanga aliwat.aka vijana hao wale ambao watakuwa na mawazo mazuri wafike Ofisini kwake ili kuyarekebisha na kuweza kuwasaidia pale watakapo pata mikopo halmashauri yapate kuwa kwamua kiuchumi.

Vijana wa Mtaa wa Dome Kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye kikao chao cha kuhamasishwa kujiunga kwenye vikundi kuanzia watu watano.

Kikao kikiendelea.

Kikao cha hamasa ya vijana kujiunga kwenye vikundi kikiendelea.

Vijana wakiendelea kusikiliza elimu namna ya kujiunga kwenye vikundi na kutimiza masharti ya kupewa mikopo Asilimia 5 kutoka kwenye mapato ya ndani ya Halmashauri.

Vijana wakiwa kwenye kikao cha hamasa kujiunga kwenye vikundi vya Ujasiriamali ili wawe na shughuli za uzalishaji mali ambazo zitawaingizia kipato na kuweza kujikwamua kiuchumi.

Vijana wa mtaa wa Dome Kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye Picha ya Pamoja na viongozi wa Mtaa huo na Kata, mara baada ya kumaliza kikao cha hamasa ya kujiunga kwenye vikundi.

Na Marco Maduhu, ambaye pia ni Mwanishi wa Gazeti la Nipashe mkoani Shinyanga.





Powered by Blogger.