MWANAMKE AHUKUMIWA KIFO BAADA YA KUMUA MWANAUME ALIYEMBAKA
Mahakama moja nchini Sudan imemhukumu kifo mwanamke/binti mwenye umri wa miaka 19 kwa kumuua mumewe aliyembaka.
Jaji wa mahakama hiyo iliopo Omdurman alithibitisha hukumu hiyo ya kifo baada ya familia ya mumewe mwanamke huyo kukataa kufidiwa kifedha.
Wakati alipokuwa na umri wa miaka 16 , Nourra Hussein alilazimishwa kuingia katika ndoa na familia yake ambapo imedaiwa kuwa hakuwa na raha hatua iliyomlazimu kutoroka na kujificha katika nyumba ya shangazi yake.
Lakini miaka mitatu baadaye , amesema kuwa alidanganywa arudi nyumbani na familia yake ambayo ilimrudisha tena kwa mumewe.
Baada ya siku sita mumewe aliwaita binamu zake ambao walimzuia chini na mumewe akambaka na wakati alipojaribu kumbaka tena siku iliofuata Nourra alimdunga kisu mumewe hadi akafariki.
Imeelezwa kuwa baada ya tukio hilo Noura litoroka na kurudi kwa wazazi wake ambao walimpeleka kwa maafisa wa polisi.
Wakati wa kusikizwa kwa kesi yake Jaji huyo aliipatia familia ya mumewe chaguo la kumsamehe Nourra lakini ikachagua auwawe.
Aidha Mawakili wake wamewasilisha ombi la hukumu ndogo ya mauaji ambapo wametakiwa kukata rufaa ndani ya siku 15.
Pamoja na hayo kundi la wanaharakati wa kupigania haki za kibinaadamu la E'quality Now' limesema kuwa litamwandikia rais Omar al-Bashir kumuomba amuonee huruma