NAPE ATOA UJUMBE MZITO BAADA YA KINANA KUNG'ATUKA CCM


Mbunge wa Mtama, na Mjumbe wa Kamati Kuu CCM, Nape Nnauye amemuaga na kumuahidi aliyekuwa Katibu wa chama chao, Ndg Abdulrahman Kinana aliyestaafu jana kuwa wataendelea kumuenzi na mbegu aliyopanda itaota.


Nape ametoa ahadi hiyo kwa Kinana baada ya kiongozi huyo kutangaza kustaafu nafasi hiyo na kukubaliwa na Mwenyekiti wa Chama hicho na Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli.


Pamoja na hayo Nape ameweka wazi kumtambua kinana kama mwalimu uliyebadili mtazamo wetu juu ya siasa na utumishi kwa umma.


"Pumzika rafiki wa kweli, pumzika Mlezi na Mzazi usiyemfano, pumzika Kiongozi, pumzika Komredi. Mwalimu uliyebadili mtazamo wetu juu ya siasa na utumishi kwa umma! Umepanda mbegu na itaota,"


Powered by Blogger.