SHIBUDA AFUNGUKA CHANZO MIGOGORO YA KISIASA HAPA NCHINI




Mwenyekiti wa baraza la vyama vya Siasa nchini Tanzania John Shibuda, amedai ufumbuzi wa kuondoa migogoro ya vyama vya siasa hapa nchini, ni kutolewa kwa elimu ya Uraia kwa viongozi wa kisiasa wote bila ya kujali itikadi ya vyama vyao.


Alisema ndani ya miaka 30 sasa, mfumo wa vyama vingi umetekekezwa, ambapo zamani viongozi wote wa kiasisa walikuwa wakipatiwa elimu ya uraia pamoja na kufundwa kwenye vyuo vya siasa, ambapo viongozi walikuwa na maadili mazuri wala kutokuwapo kwa siasa za chuki.

Shibuda amebainisha hayo leo mei 20,2018 wakati akizungumza na vyombo vya habari mjini Shinyanga, kuwa dawa ya kuondoa migogoro ya kisiasa hapa nchini imepatikana, ambapo ni viongozi wote wa kisiasa wanatakiwa wapatiwe mafunzo ya elimu ya uraia, ambayo itasaidia kuwapatia dira namna ya kuendesha siasa zisizo na migogoro.

“Mlezi wa vyama vingi vya siasa ni Serikali, ambayo inapaswa kutenga bajeti ya kutolewa semina elekezi ya elimu ya uraia kwa viongozi wa vyama vyote vya siasa, ili waweze kupata dira ya uongozi ,na kujua historia ya nchi yetu imetoka wapi na namna ilivyokombolewa”alisema Shibuda.

“Vyama vya siasa vimetelekezwa na Serikali kutopewa mafunzo ya elimu ya Uraia ndani ya miaka 30 sasa, hii ni sawa na kumtelekeza mtoto mitaani, ambapo baadae atakuwa chokolaa na kutokuwa na maadili mazuri, lazima atakusumbua tu, hivyo suluhu yake siyo kufunga viongozi jela, wala kufuta vyama bali ni kupatiwa elimu ya uraia,”aliongeza.

Aidha alimtaka Rais John Magufuli kuzifanyia kazi mbinu hizo ambazo amezitaja, kuwa zitamsaidia kuongoza vizuri kwenye utawala wake, na kuwapo na siasa safi zenye kujali demokrasia, ikiwa mfumo wa vyama vingi ulianzishwa sababu ya kuifanya Serikali iliyopo madarakani ipate kuwajibika kwa wananchi, ikiwamo na kuondoa Masuala ya Rushwa na ufisadi.
TAZAMA PICHA HAPA CHINI

Mwenyekiti wa baraza la vyama vya siasa hapa nchini John Shibuda akizungumza na waandishi wa habari mjini Shinyanga.

Mwenyekiti wa baraza la vyama vya siasa hapa nchini John Shibuda akizungumza na waandishi wa habari mjini Shinyanga.

Mwandishi wa habari gazeti la Mtanzania mjini Shinyanga Sam Bahari akiwa kwenye kikao cha mwenyekiti wa baraza la vyama vya siasa nchini John Shibuda akiandika mawili matatu kwa ajili ya kuhabarisha umma.

Waandishi wa habari mjini Shinyanga wakiwa kwenye kikao na Shibuda, wa kwanza mkono wa kushoto ni Kareny Masasy Mwandishi wa gazeti la habari Leo, akiwa na Suzy Butondo Mwandishi wa Gazeti la Mwananchi.

Waandishi wa habari mjini Shinyanga wakiwa kwenye mkutano na Shibuda ambaye pia aliwahi kuwa Mbunge wa Maswa Magharibi mkoani Simiyu.

Wanahabari wakitayarisha vifaa kwa ajili ya kuanza mkutano na Shibuda.

Wanahabari wakitayarisha vifaa kwa ajili ya kuanza mkutano na Shibuda.

Wanahabari wakitayarisha vifaa kwa ajili ya kuanza mkutano na Shibuda.

Mwenyekiti wa baraza la siasa nchini Tanzania John Shibuda akiandaa makabrasha kwa ajili ya kuzungumza na wanahabari mjini Shinyanga, mkono wa Kushoto ni Mwandishi wa habari wa Gazeti la Habari Leo Kareny Masasy.

Mwandishi wa habari gazeti la Mtanzania mjini Shinyanga Sam Bahari akiwa kwenye kikao cha mwenyekiti wa baraza la vyama vya siasa nchini John Shibuda

Mwenyekiti wa baraza vyama vya Siasa nchini Tanzania John Shibuda akiwa na waandishi wa habari mjini Shinyanga.

Waandishi wa habari mjini Shinyanga wakiwa kwenye kikao na Shibuda, wa kwanza mkono wa kushoto ni Kareny Masasy Mwandishi wa gazeti la habari Leo, akiwa na Suzy Butondo mwandishi wa Gazeti la Mwananchi.

Na Marco Maduhu ambaye pia ni Mwandishi wa Gazeti la Nipashe mkoani Shinyanga



Powered by Blogger.