STAND UNITED YAWAHAKIKISHIA MASHABIKI WAKE KUTOSHUKA DARAJA BAADA YA KUIBAMIZA AZAM FC



Timu ya mpira wa miguu ya Stand United ya mjini Shinyanga (Chama la wana) ambayo inashiriki msimu wa pili sasa kucheza Ligi kuu bara, imewahakikisha mashabiki wake kuwa haitaweza kushuka daraja mara baada ya kuibamiza Timu ya Azamu Fc Magori mawili kwa moja.


Mchezo huo wa Stand United na Azamu Fc umechezewa leo Mei 6, 2018 katika uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga, ambapo katika Kipindi cha Kwanza Timu ya Stand chama la wana walionekana kuutawala mchezo huo, ambapo Dakika ya 45 Kipindi cha Kwanza Blais Brigmana alipachika bao kwa shuti kali, lakini Gori hilo lilikataliwa.

Hata hivyo katika dakika Mbili za nyongeza kipidi hicho cha Kwanza Sixtus Sabilo akaipatia Stand United bao la kuongoza, hadi mchezo unakwenda mapunziko Chama la wana walikuwa mbele kwa Gori moja.

Katika Kipindi cha Pili Dakika ya 80 Shabani Iddi kutoka Azam Fc akasawazisha bao hilo, lakini ndani ya dakika 90 furaha yake ikazimwa na mchezaji Ally Ally kutoka Stand United ambaye alifunga Gori kwa Kichwa na kuiandikia Stand bao la Pili, hadi mchezo unakwisha dakika Tatu za Nyongeza Chama la wana wakaibuka na Point Tatu na kufikisha 32 wakiwa nafasi ya Tisa.

Akizungumzia mchezo huo kocha msaidizi wa Timu ya Stand United Athumani Bilali, amesema mchezo huo ulikuwa muhimu sana wao kushinda ambapo umewahakikishia kutoweza kushuka daraja, na kuwatoa hofu mashabiki kuwa katika michezo Mitatu iliyosalia watafanya vizuri, ili kumaliza msimu wakiwa nafasi za juu.

Naye Kocha msaidizi wa Timu ya Azam FC Mwijage Abdul alikiri mchezo huo kuwa mgumu kwao, ambapo nafasi walizokuwa wanazipata walishindwa kuzitumia, ambapo makosa waliyotengeneza wenzao waliweza kuyatumia na hatimaye kuibuka na ushindi, huku akiahidi mashabiki wa Timu hiyo kufanya vizuri katika Mechi zilizosalia ikiwa zote watacheza wakiwa nyumbani ambapo kwa sasa wamesalia na Pointi zao 49 wakishika nafasi ya Pili.


TAZAMA MATUKIO KATIKA PICHA


Mashabiki wa Timu ya Stand United Chama la wana ya mjini Shinyanga wakishangilia ushindi walioupata dhidi ya Timu ya Azam Fc kwa kuwafunga Magori mawili kwa moja mchezo uliochezwa katika uwanja wa CCM Kambarage mjini humo.

Mchezaji wa Timu ya Stand United Ally Ally aliyepachika bao la Pili Dakika ya 90 na kuipatia ushindi Stand United dhidhi ya Azam Fc na hatimaye kuibuka na Point Tatu katika uwanja wa Nyumbani CCM Kambarage.

Shabiki wa Timu ya Stand United Mwita akishangilia Gori hilo la Ally Ally huku Askari Polisi akimzuia.


Kocha msaidizi wa Timu ya Stand United Athumani Bilali akizungumza na waandishi wa habari, na kufurahia ushindi huo ambao umewahakikishia kutoweza kushuka daraja na kutarajia tena Timu hiyo kushiriki Ligi kuu katika Msimu ujao.

Kocha msaidizi wa Timu ya Azam FC Mwijage Abdul akizungumza na waandishi wa habari amesema mchezo huo ulikuwa mgumu kwao, na kuahidi katika mechi zilizosalia watafanya vizuri kwani watakuwa nyumbani pamoja na majeruhi wao kupona.

Shabiki wa Timu ya Stand United Mwita akiendelea kupambana na Askari Polisi ambaye amekuwa wakimzui kutoa Hamasa ya kushangilia Timu yake mara baada ya kuibuka na ushindi wa Magori mawili kwa Moja dhidi ya Azam Fc.

Mashabiki wa Timu ya Stand United wakiendelea kushangilia ushindi wao mnono ambao umewafanya kuwa na uhakika wa kutoshuka Daraja.


Na Marco Maduhu ambaye pia ni Mwandishi wa Gazeti la Nipashe mkoani Shinyanga.

Powered by Blogger.