WABUNGE CHADEMA WA KWAMA KUHUDHURIA KIKAO CHA BUNGE


Wabunge wa Chadema leo Jumatano Mei 30, 2018 hawajahudhuria kikao cha Bunge la Bajeti, kwa madai kuwa wengi wamekwenda mkoani Kigoma kushiriki maziko ya aliyekuwa mbunge wa chama hicho, Kasuku Bilago.


Bilago ambaye alikuwa mbunge wa Buyungu, alifariki dunia Jumamosi Mei 26, 2018 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH). Aliagwa jana na wabunge kwenye viwanja vya Bunge na mwili wake kusafirishwa mkoani Kigoma kwa maziko.

Eneo wanaloketi wabunge wa chama hicho ndani ya ukumbi wa Bunge, lipo tupu, wakati wa kipindi cha maswali na majibu leo asubuhi, maswali ya wabunge hao wa Chadema likiwamo la Joseph Mkundi (Ukerewe), yaliulizwa na wabunge wa CCM
Powered by Blogger.