WAKURUGENZI WAPEWA MBINU KUKWEPA HATI CHAFU




Waziri wa nchi ofisi ya Rais TAMISEMI Selemani Jafo, amewataka wakurugenzi wa halmashauri hapa nchini kusimamia miradi ya maendeleo kwa umakini, pamoja na kujibu hoja zote za mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za Serikali (CAG) ili kutopa hati chafu.


Alisema usimamizi mzuri wa fedha za miradi ya maendeleo kutazuia ufujaji wa fedha, na kufanikiwa kujibu hoja zote za (CAG), na hatimaye halmashauri kupata hati safi.

Jafo alizungumza jana Mei 14,2018 alipokuwa mkoani Shinyanga, wakati akipokea taarifa ya mkoa huo kabla ya kuanza ziara yake ya kukagua mradi wa barabara za Lami unaojengwa katikati ya mjini huo na Kampuni ya Jasco, kuwa Serikali haitaki halmashauri yoyote kupata hati chafu.

“Naagiza wakurugenzi wote hapa nchini msimamie vizuri miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwenye halmashauri zenu, ilikuzia ufujaji wa fedha pamoja na kujibu hoja zote za (CAG) ili kukwepa kupata hati chafu,”alisema Jafo.

“Katika taarifa ya (CAG) iliyopita kulikuwa na halmashauri Tatu ambazo zilipata hati Chafu, hivyo katika tarifa ijayo hatutaki kusikia tena hati chafu, bali halmashauri zote nchini ziwe na hati safi,”aliongeza.

Pia aliagiza fedha zote kwenye vituo vya afya zikusanywe kwa njia ya kielectronic ilikuzia upotevu wa mapato, pamoja na kumaliza kuondoa watumishi hewa ikiwa bado kwenye halmashauri kunatatizo hilo, ikiwamo halmashauri ya wilaya ya Nyang’wale mkoani Geita.

Naye mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainabu Telack, akisoma taarifa yake ya mkoa huo alisema bado unakabiliwa na uhaba wa watumishi hususani kwenye Sekta ya Afya na maofisa ushirika, ambapo kuna vituo vya afya saba vimeshajengwa, lakini vimeshindwa kuanza kazi sababu ya ukosefu wa wauguzi.

Aidha alimwomba waziri katika ajira ambazo zimetangazwa za watumishi wa afya 6,100 wauangalie na mkoa huo, pamoja na kuwapatia maofisa ushirika ikiwa kuna baadhi ya halmashauri hazina kabisa, na hivyo kupata wakati mgumu wa kutoa elimu kwa wakulima wa pamba kujiunga na vyama vya ushirika.

TAZAMA HABARI PICHA HAPA CHINI


Waziri wa nchi ofisi ya Rais TAMISEMI Selemani Jafo akizungumza na viongozi wa mkoani Shinyanga mara baada ya kuwasili mkoani hapa kwa ajili ya ziara yake ya siku moja ya kukagua miradi ya barabara.

Waziri wa nchi ofisi ya Rais TAMISEMI Seleman Jafo akizungumza na Mkandarasi wa Kampuni ya Jasco Karan Bachu, juu ya utendaji wao kazi wa kusuasua na kuwataka waache kufanya kazi za ubabaishaji, huku akimuahidi kuja kufuatilia ujenzi wa barabara hizo za Lami baada ya miezi mitatu kama alivyo ahidi kuikamilisha.

Meneja wakala wa barabara mijini na vijijini Tarura David Mwakalalile, akisoma taarifa ya ujenzi wa barabara hizo za Lami, alisema mkataba ulianza mwaka (2016) na kutarajiwa kukamilika (2017), lakini ulishindwa kukamilika kwa wakati, kutokana na ukosefu wa fedha kuja kwa wakati sababu ya utendaji kazi kuwa chini, pamoja na mtililiko wa fedha kutokuwa mzuri kwenye mkataba.

Mkurugenzi wa halmashauri ya manispaa ya Shinyanga Geofley Mwangulumbi, akizungumza mbele ya waziri Jafo kuwa mkandarasi huyo Jasco kazi zake ni za kusuasua, huku wakwanza mkono wa kulia ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro, na mkono wa Kushoto ni Naibu Meya wa manispaa ya Shinyanga Agness Machiya.

Waziri wa nchi ofisi ya Rais TAMISEMI Seleman Jafo, akisikiliza hoja ya mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro juu ya kutolewa ufafanuzi hoja ya mikopo ya halmashauri kama inalipiwa Riba mbele ya mkurugenzi wa halmashauri ya manispaa ya Shinyanga Geofley Mwangulumbi ,na kutolewa maelezo kuwa mikopo hiyo ya halmashauri ya akina mama na vijana haina Riba.

Waziri wa nchi Ofisi ya Rais TAMISEM Selemani Jafo akiwasili kwenye ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga, hapo akipeana mkono na mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro ,akimkaribisha mkoani Shinyanga kwa ajiri ya ziara yake ya kukagua mradi wa barabara za Lami katikati ya mji wa Shinyanga.

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainabu Telack akitoa taarifa ya mkoa kwa waziri wa nchi ofisi ya Rais TAMISEMI Selemani Jafo, kuwa mkoa huo upo salama isipokuwa kuna matukio ya mauaji ya wanawake kwa kukatwa mapanga kutokana na wivu wa kimapeni na imani za kishirikina, ambazo huhamasishwa na waganga wa kienyeji ambapo mmoja wa waganga hao ameshakamatwa, na mkoa kubaki kuwa salama, pamoja na kuwepo na changamoto hiyo ya mkandarasi Jasco kutomaliza kazi zake za ujenzi wa barabara kwa wakati.

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainabu Telack, akimuonyesha CD na kumkabidhi waziri wa nchi ofisi ya Rais TAMISEMI Seleman Jafo, inayohusua makubaliano ya baraza la madiwani la halmashauri ya msalala juu ya makao makuu ya msalala yatakuwa wapi, huku akimweleza suala la mgawo wa fedha za Mgodi wa Bulyanhuru kupewa Msalala na wilaya ya Nyang'wale mkoani Geita, kuwa limeshakwisha ambapo mgao huo zitapewa halmashauri zote, na kumuomba waziri huyu apuuze maneno ya watu ambao humpelekea maneno ya uongo juu ya migogoro hiyo ambayo imeshakwisha kutatuliwa na maridhiano yapo kwenye hiyo CD.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEM Seleman Jafo, akimtoa wasiwasi mkuu huyo wa mkoa, kuwa suala la migogoro hiyo analifahamu na ndio maaana amekaa kimya sababu anafahamu ukweli licha Figisu zote hizo ,pamoja na kuchukua CD hiyo kwenda kuisikiliza, huku akiagiza pia wakurugenzi wa halmashauri wasimamie miradi ya maendeleo kikamilifu, pamoja na kuwa wanajibu kwa ufasaha hoja za mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za Serikali (CAG) ilikusiwepo na hati chafu kwenye halmashauri, bali zote zipate hati safi.

Pia Waziri huyo aliagiza vituo vyote vya afya makusanyo yake yakusanywe kwa njia ya Kielectroniki, pamoja na kumaliza mauaji ya vikongwe na Albino ikiwa kwenye mikoa ya Kanda ya Ziwa vitendo hivyo bado vipo, ambavyo vina haribu sifa ya nchi.

Watendaji wa Serikali mkoani Shinyanga akiwamo na mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro, wakimsikiliza Waziri wa nchi ofisi ya Rais TAMISEMI Seleman Jafo, ambaye amepongeza mkoa huo kwa kuendelea kufanya vizuri kwenye matokeo ya mtihani, tofauti na miaka ya nyuma ambapo kitaifa mkoa huo ulishika nafasi ya Nne kwenye matokeo ya kidato cha Nne mwaka jana.

Na Marco Maduhu, ambaye pia ni Mwandishi wa Gazeti la Nipashe mkoani Shinyanga
Powered by Blogger.