WAZIRI JAFO KUISHUGHULIKIA KAMPUNI YA JASCO



Waziri wanchi ofisi ya Rais TAMISEMI Selemani Jafo, amelalamikia utendaji kazi mbovu wa Kampuni ya Jasco, ambayo inatekeleza ujenzi wa mradi wa barabara za Lami katikati ya mji wa Shinyanga kilomita 13, wenye thamani ya Shilingi bilioni 15 kuwa ndani ya miezi mitatu awe ameshakamilisha mradi huo kabla ya kumshughulikia.


Imeelezwa Kampuni hiyo ilipewa kazi ya ujenzi wa barabara hizo tangu mwaka (2016) na mkataba huo ulitarajiwa kukamilika June (2017), lakini mpaka sasa zimeshajengwa barabara za Lami kiliomita 4 na kusalia Tisa, ambazo zimedaiwa kuwa ndani ya miezi mitatu ijayo zitakuwa zimeshakamilika.

Jafo ameilalamikia kampuni hiyo Leo Mei 14, 2018 alipokuwa mkoani Shinyanga, kwenye ziara yake ya kikazi ya kukagua miradi hiyo ya ujenzi wa barabara za lami katikati ya mji wa Shinyanga, ambayo imekuwa ikisua sua kukamilika kwake .

“Baada ya miezi mitatu ambapo utakuwa ni Mwezi wa Nane nitakuja tena kuangalia kazi hii kama utakuwa umeshamaliza, tofauti na hapo tutakushughulikia sababu kampuni hii imekuwa na utendaji wake kazi mbovu, kila sehemu ambazo mnamiradi mmekuwa mkilalamikiwa sana,”alisema Jafo.

“Mkuu wa mkoa naomba hili ulisimamie huyu bwana akamilishe ujenzi huu wa barabara za Lami haraka sana, na azijenge kwa kiwango kinachotakiwa na ziwe za kudumu ndani ya miaka 20 na siyo miwili , sababu serikali tunatumia pesa nyingi sana kwenye jenzi hizi za barabara,”aliongeza.

Awali mkandarasi kutoka kampuni hiyo ya Jasco Karan Bachu, alisema kilomita hizo Tisa zilizosalia na ufungwaji wa mataa kwenye barabara hizo watakuwa wameshazikamilisha ndani ya miezi hiyo mitatu, ikiwa fedha wanazo pamoja na vitendea kazi.

Naye Meneja wakala wa barabara mijini na vijijini Tarura David Mwakalalile, akisoma taarifa ya ujenzi wa barabara hizo za Lami, alisema mkataba ulianza mwaka (2016) na kutarajiwa kukamilika (2017), lakini ulishindwa kukamilika kwa wakati, kutokana na ukosefu wa fedha kuja kwa wakati sababu ya utendaji kazi kuwa chini pamoja na mtililiko wa fedha kutokuwa mzuri kwenye mkataba.

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainabu Telack, aliahidi kulisimamia suala hilo kama agizo lilivyotolewa, na kubainisha kuwa kutokana na utendaji wa Kampuni hiyo kuwa siyo wa kulidhisha, awali walishamweka Rumande na hivyo kumuonya mkandarasi wa kampuni hiyo akamilishe kazi kwa muda huo uliopangwa.
TAZAMA PIA HABARI PICHA HAPA CHINI

Waziri wa nchi ofisi ya Rais TAMISEMI Seleman Jafo akizungumza na Mkandarasi wa Kampuni ya Jasco Karan Bachu, juu ya utendaji wao kazi wa kusuasua na kuwataka waache kufanya kazi za ubabaishaji, huku akimuahidi kuja kufuatilia ujenzi wa barabara hizo za Lami baada ya miezi mitatu kama alivyo ahidi kuikamilisha.

Meneja wakala wa barabara mijini na vijijini Tarura David Mwakalalile, akisoma taarifa ya ujenzi wa barabara hizo za Lami, alisema mkataba ulianza mwaka (2016) na kutarajiwa kukamilika (2017), lakini ulishindwa kukamilika kwa wakati, kutokana na ukosefu wa fedha kuja kwa wakati sababu ya utendaji kazi kuwa chini, pamoja na mtililiko wa fedha kutokuwa mzuri kwenye mkataba.

Mkurugenzi wa halmashauri ya manispaa ya Shinyanga Geofley Mwangulumbi, akizungumza mbele ya waziri Jafo kuwa mkandarasi huyo Jasco kazi zake ni za kusuasua, huku wakwanza mkono wa kulia ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro, na mkono wa Kushoto ni Naibu Meya wa manispaa ya Shinyanga Agness Machiya.

Waziri wa nchi ofisi ya Rais TAMISEMI Seleman Jafo, akisikiliza hoja ya mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro juu ya kutolewa ufafanuzi hoja ya mikopo ya halmashauri kama inalipiwa Riba mbele ya mkurugenzi wa halmashauri ya manispaa ya Shinyanga Geofley Mwangulumbi ,na kutolewa maelezo kuwa mikopo hiyo ya halmashauri ya akina mama na vijana haina Riba.

Waziri wa nchi Ofisi ya Rais TAMISEM Selemani Jafo akiwasili kwenye ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga, hapo akipeana mkono na mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro ,akimkaribisha mkoani Shinyanga kwa ajiri ya ziara yake ya kukagua mradi wa barabara za Lami katikati ya mji wa Shinyanga.

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainabu Telack akitoa taarifa ya mkoa kwa waziri wa nchi ofisi ya Rais TAMISEMI Selemani Jafo, kuwa mkoa huo upo salama isipokuwa kuna matukio ya mauaji ya wanawake kwa kukatwa mapanga kutokana na wivu wa kimapeni na imani za kishirikina, ambazo huhamasishwa na waganga wa kienyeji ambapo mmoja wa waganga hao ameshakamatwa, na mkoa kubaki kuwa salama, pamoja na kuwepo na changamoto hiyo ya mkandarasi Jasco kutomaliza kazi zake za ujenzi wa barabara kwa wakati.

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainabu Telack, akimuonyesha CD na kumkabidhi waziri wa nchi ofisi ya Rais TAMISEMI Seleman Jafo, inayohusua makubaliano ya baraza la madiwani la halmashauri ya msalala juu ya makao makuu ya msalala yatakuwa wapi, huku akimweleza suala la  mgawo wa fedha za Mgodi wa Bulyanhuru kupewa Msalala na wilaya ya Nyang'wale mkoani Geita, kuwa limeshakwisha ambapo mgao huo zitapewa halmashauri zote, na kumuomba waziri huyu apuuze maneno ya watu ambao humpelekea maneno ya uongo juu ya migogoro hiyo ambayo imeshakwisha kutatuliwa na maridhiano yapo kwenye hiyo CD.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEM Seleman Jafo, akimtoa wasiwasi mkuu huyo wa mkoa, kuwa suala la migogoro hiyo analifahamu na ndio maaana amekaa kimya sababu anafahamu ukweli  licha Figisu zote hizo ,pamoja na kuchukua CD hiyo kwenda kuisikiliza, huku akiagiza pia wakurugenzi wa halmashauri wasimamie miradi ya maendeleo kikamilifu, pamoja na kuwa wanajibu kwa ufasaha hoja za mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za Serikali (CAG) ilikusiwepo na hati chafu kwenye halmashauri, bali zote zipate hati safi.

Pia Waziri huyo aliagiza vituo vyote vya afya makusanyo yake yakusanywe kwa njia ya Kielectroniki, pamoja na kumaliza mauaji ya vikongwe na Albino ikiwa kwenye mikoa ya Kanda ya Ziwa vitendo hivyo bado vipo, ambavyo vina haribu sifa ya nchi.

Watendaji wa Serikali mkoani Shinyanga akiwamo na mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro, wakimsikiliza Waziri wa nchi ofisi ya Rais TAMISEMI Seleman Jafo, ambaye amepongeza mkoa huo kwa kuendelea kufanya vizuri kwenye matokeo ya mtihani, tofauti na miaka ya nyuma ambapo kitaifa mkoa huo ulishika nafasi ya Nne kwenye matokeo ya kidato cha Nne mwaka jana.

Na Marco Maduhu, ambaye pia ni Mwandishi wa Gazeti la Nipashe mkoani Shinyanga.





Powered by Blogger.