DC MATIRO AKIFUNGA CHOO CHA MABASI SHINYANGA




Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro, amekifunga Rasmi choo cha zamani cha Standi ya Mabasi ya kwenda wilayani mkoani hapa, kutokana na kukithiri kwa uchafu na kuhatarisha afya za watumiaji wa standi hiyo, kwa kuweza kupatwa na magonjwa ya mlipuko.


Choo hicho kimedaiwa hakina sifa ya kutoa huduma ya kujisaidia, sababu ya kuwa kichafu ambapo kipindi cha nyuma mkuu huyo wa wilaya aliangiza kifungwe ili kifanyiwe ukarabati, lakini hakuna kilichotekelezwa na kuendelea kutumiwa, na hivyo kuamua kukifunga moja kwa moja na kutotoa huduma hiyo tena.

Matiro amekifunga choo hicho Leo June 5,2018 wakati alipokuwa akikagua usafi wa mazingira katika eneo hilo la standi ya mabasi ya kwenda wilayani, ikiwa ni siku ya kuadhimisha kilele cha mazingira duniani katika mansipaa ya Shinyanga, kuwa choo hicho kifungwe na hakitakiwi kifanye kazi tena.

“Hapa Standi kuna choo kipya kabisa kwanini muendelee kung’ang’ania kutumia hiki cha zamani ambacho ni kichafu na hakina hadhi kabisa ya kutoa huduma ya kujisaidia, hivyo kuanzia sasa choo hiki na kifunga rasmi, hakuna tena kufanya kazi kitumieni kile kipya,”alisema Matiro.

“Choo hiki kipya nacho hakiridhishi kabisa usafi wake kinatoa harufu kali, nacho naagiza kifanyiwe usafi wa hali ya juu pamoja na kuwekewa dawa, pia muwasimamie abiria ambao wanatupa uchafu hovyo, mshusheni ndani ya basi aje aokote uchafu wake,”aliongeza.

Naye kaimu ofisa mazingira wa halmashauri ya manispaa ya Shinyanga Ezra Majerenga, amelaani kitendo cha watumiaji wa standi hiyo kukojoa mikojo kwenye makopo ya maji na kisha kuyatupa kwenye mitaro, hali ambayo ni hatari kwa afya zao na kuchafua mazingira.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Standi hiyo ya Mabasi Rashidi Issa, alipongeza kufungwa kwa choo hicho, huku akiahidi kusimamia zoezi la usafi wa mazingira kikamilifu, pamoja na kuwabana watu ambao wamekuwa wakikojoa mikojo kwenye makopo.

TAZAMA MATUKIO KATIKA PICHA HAPA CHINI


Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akitoka nje mara baada ya kukagua choo cha zamani cha Standi ya mabasi wilayani ambacho ni kichafu na kinatoa harufu kali, kama unavyo muona mkuu wa wilaya akitahamaki na harufu hiyo.

Uchafu ukiwa jirani na choo hicho cha Standi ya mabasi ya kwenda wilayani mkoani Shinyanga.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiendelea na zoezi la ukaguzi katika choo cha Zamani cha Standi ya Mabasi ya kwenda Wilayani.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro (Mwenye Tshirt Nyeupe) akiwa katika eneo la Standi ya Mabasi ya kwenda wilayani, akikagua usafi wa mazingira.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiongea kwenye Standi hiyo ya Mabasi na kuwataka wawe wasafi pamoja na kuwakamata abiria ambao wamekuwa wakitupa uchafu chini, na kwenda kushusha ili wauokote, pamoja na Mabasi yote kuwa na vifaa vya kutunzia uchafu ndani.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akikagua vifaa vya kutunzia uchafu katika choo kipya cha Standi hiyo ya Mabasi ya kwenda wilayani ambacho nacho usafi wake siyo wa kuridhisha.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiangalia vifaa vya kutunzia uchafu katika choo kipya cha Standi hiyo ya Mabasi ya kwenda wilayani, ambavyo havina hadhi na kuagiza viwekwe vingine vipya.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiendelea na ukaguzi wa choo kipya cha Standi ya Mabasi ya kwenda wilayani, ambacho ni kichafu na kuagiza kifanyiwe usafi wa hali ya juu pamoja na kuwekewa madawa.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiendelea na zoezi la ukaguzi wa usafi wa mazingira katika Standi hiyo ya Mabasi ya kwenda wilayani, huku wakwanza mkono wa Kushoto ni mwenyekiti wa Standi hiyo Rashidi Issa.

Mkuu walaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza kwenye Standi hiyo ya mabasi ya kwenda wilayani na kuwataka akina mama na vijana wajiunge pia kwenye vikundi ili waweze kupata mikopo ya halmashauri na hatimaye kuinuka kiuchumi.

Wafanyabiashara ndogo wa Standi hiyo ya Mabasi ya kwenda wilayani wakifanya usafi.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro mkono wa kushoto akimtaka msimamizi wa choo kipya cha Standi hiyo Emmanuel Limbu kukifanyia usafi wa hali ya juu pamoja na kuweka madawa.

Wafanyabiashara wa Standi ya Mabasi ya kwenda wilayani mkoani Shinyanga wakimsikiliza mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro alipofika kukagua usafi wa mazingira kwenye Standi hiyo pamoja na kutatua kero zinazowakabili.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro mkono wa kushoto, akiwa na Mwenyekiti wa Stand hiyo Rashidi Issa wakati wa zoezi la ukaguzi wa usafi wa mazingira.

Mwenyekiti wa Standi ya Mabasi ya kwenda wilayani Rashidi Issa amewataka wafanyabishara hao kuzingatia usafi wa mazingira pamoja na kuvaa Sare.

Wafanyabiashara ndogo wakiendelea kumsikiliza mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro alipofika kwenye Stand hiyo ya Mabasi ya kwenda Wilayani.

Mama Lishe wa Stand hiyo ya Mabasi ya kwenda wilayani wakipika Chakula.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro mwenye Tshirt Nyeupe akitoa maagizo kwa Ofisa biashara wa manispaa ya Shinyanga Deogratius Sunday, kuhakikisha choo cha zamani cha Standi hiyo akifanyi kazi tena mara baada ya kukifunga.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiendelea kutoa maagizo kwa Ofisa Biashara wa manispaa ya Shinyanga Deogratius Sunday kuwa kwenye Standi hiyo ahakikishe vinakuwapo vifaa vya kutunzia uchafu,pamoja na kufuatilia mmoja wa wafanyabishara ambaye amekuwa akitoa huduma vya Pombe lakini hana choo.

Skauti wa wilaya ya Shinyanga wakifanya usafi katika maeneo mbalimbali ya mjini Shinyanga kama siku ya kuadhimisha kilele cha Mazingira Duniani.

Skauti wa wilaya ya Shinyanga wakiendelea na zoezi la usafi wa mazingira.

Kaimu Ofisa Mazingira wa halmashauri ya manispaa ya Shinyanga Ezra Majerenga akifanyia usafi mti kwa kuuwekea mazingira mazuri.

Zoezi la usafi wa mazingira likiendelea.

Kaimu Ofisa Mazingira wa halmashauri ya manispaa ya Shinyanga Ezra Majerenga akiongoza zoezi la Usafi wa Mazingira katika kuadhimisha siku ya kilele cha Mazingira Duniani

Dorothea Kruise ambaye ni mtaalamu wa takataka kutoka Germani naye akishiriki zoezi la kufanya usafi wa Mazingira katika manispaa ya Shinyanga.

Dorothea Kruise ambaye ni mtaalamu wa takataka kutoka Germani naye akishiriki zoezi la kufanya usafi wa Mazingira katika manispaa ya Shinyanga.

Zoezi la usafi wa mazingira likiendelea.

Skauti wa wilaya ya Shinyanga wakiendelea na zoezi la kufaya usafi wa mazingira.
Zoezi la usafi wa mazingira likiendelea.

Usafi wa mazingira ukiendelea.

Dorothea Kruise ambaye ni mtaalamu wa takataka kutoka Germani naye akishiriki zoezi la kufanya usafi wa Mazingira katika manispaa ya Shinyanga.

Dorothea Kruise ambaye ni mtaalamu wa takataka kutoka Germani naye akishiriki zoezi la kufanya usafi wa Mazingira katika manispaa ya Shinyanga.

Zoezi la usafi wa mazingira likiendelea.

Zoezi la usafi wa Mazingira likiendelea.

Kaimu Ofisa Mazingira wa halmashauri ya manispaa ya Shinyanga Ezra Majerenga akiwa amekamata magogo ambayo yalikuwa hayana kibari.

Mfanyabiashara ndogo akifanya biashara zake za kuuza matunda karibu na kona ya hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga.

Zoezi la usafi wa mazingira likiendelea.

Mdau wa mazingira akichoma moto takataka.

Na Marco Maduhu, ambaye pia ni Mwandishi wa Gazeti la Nipashe mkoani Shinyanga.
Powered by Blogger.