MBINU ZA KUZUIA UHARIBIFU WA MAZINGIRA ZABAINISHWA KWENYE MDAHALO MANISPAA YA SHINYANGA



Halmashauri ya manispaa ya Shinyanga, imeendesha mdahalo wa namna ya kuzuia uharibifu wa mazingira, kwa kushirikiana na watendaji wa Kata wa halmashauri, wananchi na baadhi ya walimu wastaafu.


Mdahalo huo umefanyika leo June 2,2018 kwenye ukumbi wa halmashauri ya manispaa ya Shinyanga ,wenye lengo la kutafuta ufumbuzi wa kuzuia uharibifu huo wa mazingira.

Akifungua mdahalo huo mkurugenzi wa halmashauri ya manispaa ya Shinyanga Geofley Mwangulumbi, aliwataka washirika hao kuwa huru kila mmoja kutoa maoni yake namna ya nini kifanyike ilikufanikisha zoezi la kuzuia uharibifu wa mazingira, likiwamo suala la kutokomeza uchomaji mikaa.

Aidha mdahalo huo umeendeshwa ikiwa zimebaki siku Tatu kuelekea kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya mazingira duniani, ambayo hufanyika kila mwaka June 5, na mwaka huu Kauli Mbiu ya Kitaifa inasema , Mkaa ni Gharama tumia Nishati Mbadala.

Katibu wa walimu Wastaafu mkoani Shinyanga Nsolo Steven akichangia mada kwenye mdahalo huo, alisema wao wamebaini mbinu ambazo zitasaidia kuzuia uharibifu wa mazingira kuwa ni kuanzisha kiwanda cha Uzalishaji mkaa, cha kutumia mabaki ya mazao ambacho kitasaidia kwa kiasi kikubwa kuzuia ukataji miti hovyo.

Alisema wao kama walimu wastaafu waliunda kikundi chao mara baada ya kubaini tatizo la matumizi ya mkaa kuwa ndio chanzo cha uharibifu mkubwa wa mazingira, na kuamua kununua mashine ambayo itakuwa ikizalisha mkaa kwa kutumia mabaki ya mazao ya chakula na kutumiwa katika mapishi.

Alitaja mabaki hayo ya mazao kuwa ni Mabua ya Mtama,Mahindi,Mpunga,pumba za mchele,maganda ya Karanga, Makaratasi magumu, pamoja na takataka mbalimbali zisizo asili ya Plastik, na kubainisha wanatarajia kuanza kazi mwishoni mwa mwezi huu June.


Naye Ikanda Ryms ambaye ni mkazi wa manispaa ya Shinyanga, alisema wananchi wanatakiwa kuendelea kuelimishwa jju ya suala zima la utunzaji wa mazingira faida na hasara zake, ikiwa baadhi yao wamekuwa wakiharibu mazingira bila ya kujua matatizo yake, pamoja na kusisitizwa kupanda miti kwa wingi.

Ofisa mazingira wa manispaa ya Shinyanga Ezra Majerenga, alisema kwa takwimu za Tanzania nzima jumla ya Hekali 37,200 hualibiwa kila mwaka, na kubainisha kuwa katika kampeni ya upandaji miti mwaka jana (2017) walipanda jumla ya miti Laki 487 ,na mwaka huu wanatarajia kupanda Miti Laki 6.

Kwa upande wake mkurugenzi wa halmashauri ya manispaa ya Shinyanga Geofley Mwangulumbi, aliwataka wakazi wa mji huo kuyatunza mazingira ikiwa hilo ni jukumu la kila mtu na kuwasisitiza kucha tabia ya kukata miti hovyo.

TAZAMA HABARI PICHA HAPA CHINI


Mkurugenzi wa halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga,Geofrey Mwangulumbi akifungua mdahalo wa maadhimisho ya siku ya mazingira duniani kwa maafisa watendaji wa kata katika anispaa ya Shinyanga.

Mkurugenzi wa halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga,Geofrey Mwangulumbi akizungumza wakati wa mdahalo huo uliongozwa na swali : Nini unadhani kitasaidia kufanikisha kampeni ya serikali ya utunzaji mazingira ikiwemo wananchi kuacha matumizi ya mkaa na badala yake kutumia nishati mbadala ambayo inatajwa kuwa na gharama nafuu kuliko mkaa?.

Wa kwanza kushoto ni Afisa Nyuki na Misitu kutoka NAFRAC wilaya ya Shinyanga,Franael Sumari akifuatiwa na Mtaalamu wa takataka kutoka Ujerumani Dorothea Kruse na Afisa Mazingira Manispaa ya Shinyanga Ezra Manjerenga

Afisa Mazingira Manispaa ya Shinyanga Ezra Manjerenga akizungumza wakati wa mdahalo huo na kubainisha kuwa hiyo ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya mazingira duniani ambapo kilele chake kitakuwa Juni 5,2018.

Afisa Nyuki na Misitu kutoka NAFRAC wilaya ya Shinyanga,Franael Sumari akieleza kuhusu hali ya misitu na ufugaji nyuki katika manispaa ya Shinyanga. Pamoja na mambo mengine alisema ufugaji nyuki unasaidia utunzaji mazingira.

Mtaalamu wa takataka kutoka Ujerumani Dorothea Kruse akifafanua namna ya kutumia taka ngumu kutunza mazingira.

Afisa Mtendaji kata ya Ngokolo Salum Soud akichangia mada wakati wa mdahalo huo pamoja na kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa uhifadhi wa mazingira kwenye Kata hiyo.

Afisa Mtendaji kata ya Ibinzamata,Mwajuma Bakari akichangia hoja wakati wa mdahalo huo pamoja na kuwasilisha taariifa ya utekelezaji wa uhifadhi wa mazingira kwenye Kata hiyo na kubainisha kuwa wameshapanda Miti 150.

Afisa Mtendaji kata ya Shinyanga Mjini Simon Mashishanga akichangia mada wakati wa mdahalo huo pamoja na kuwsilisha taarifa ya utekelezaji wa uhifadhi wa mazingira kwenye Kata hiyo.

Kaimu Afisa Mtendaji kata ya Kitangiri,Ansila Materu akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa uhifadhi wa mazingira kwenye Kata hiyo Ndani ya mdahalo wa mazingira.

Wadau wa mazingira wakiandika dondoo muhimu wakati wa mdahalo huo.

Maafisa watendaji wa kata ya Shinyanga Mjini Simoni Mashishanga akiwa na mtenadji Kata ya Ibadakuli wakifuatilia mdahalo wa Mazingira.

Katibu wa chama walimu wastaafu Mkoa wa Shinyanga,Nsolo Stephen akielezea namna chama hicho kinavyoshiriki katika shughuli za utunzaji mazingira. kuwa wameanzisha mradi wa kutengeneza mkaa kwa kutumia mabaki ya mazao.

Mtendaji wa Kata ya Ndala Seleman Katonga akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa uhifadhi wa mazingira kwenye Kata hiyo.

Wadau wa mazingira wakiwa ukumbini.

Mtendaji wa Kata ya Mwawaza Nhiga Nhiga akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa uhifadhi wa mazingira kwenye Kata yake ndani ya mdhalo huo.

Mtendaji wa Kata ya Ndembezi Felister Msemelwa akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa uhifadhi mazingira kwenye kata hiyo na kubainisha kuwa wameshapanda Miti 850.

Ester Daudi mtendaji wa Kata ya Masekelo akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa uhifadhi wa mazingira kwenye Kata hiyo kuwa wameshapanda miti kwenye taasisi mbalimbali pamoja na kuhamasisha wananchi kutunza mazingira kwa kufanya usafi.

Daudi Ong'washi ni mtendaji wa Kata ya Kizumbi akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa uhifadhi wa mazingira kwenye Kata hiyo, alisema wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya Dampo ambalo limekuwa likitumika kutupiwa mifupa na vichwa vya Punda, ambavyo vimekuwa vikitoa harufu kali na kusababisha Fisi kuvamia enelo hilo wakati wa mchana na usiku na kuhatarisha maisha ya wananchi, pamoja na kiwanda cha wachina kutililisha kemikali zenye Sumu jirani na makazi ya watu.

Wajumbe wakiendelea na mdahalo wa mazingira.

Na Marco Maduhu, ambaye pia ni Mwandishi wa Gazeti la Nipashe mkoani Shinyanga.
















































Powered by Blogger.