MWANAMKE SHINYANGA AJIFUNGUA MTOTO ALIYEKUWA AKIONGEA KAMA MTU MZIMA TANGU ALIPOKUWA TUMBONI





  Katika hali isiyokuwa ya kawaida mwanamke Mwanamke Maria Mpago mkazi wa kijiji cha Nyarigongo kata ya Mwakitolyo halmashauri ya wilaya na mkoa wa Shinyanga amejifungua mtoto ambaye amekuwa akizungumza wakati akiwa tumboni mwa mama yake.

Akizungumzia tukio hilo huyo mama aliyejitambulisha kwa jina la Maria Mpago kuwa  wakati wa ujauzito vipimo vya kitabibu vilishindwa kubaini kama ni mjamzito licha ya kumsikia mtoto akichezacheza tumboni.


“Nilipimwa mimba haikuonekana nikaambiwa labda nikajaribu Kahama lakini nako haikuonekana basi nikaendelea kulea mimba..wiki mbili zilizopita siku ya Ijumaa majira ya saa saba usiku nikasikia mtoto akiniongelesha tumboni akisema nipeleke msikitini nikaombewe dua,asiponipeleka mimba itaharibika ndipo asubuhi yake nikaenda msikitini nikakutana na shehe akaniombea…na siku ya Ijumaa Juni 1,2018 ndipo nikajifungua nyumbani”,ameeleza Maria


Licha ya mfululizo wa visa hivyo Maria na mumewe wanasema hawana wasiwasi wowote na kwamba hali hiyo ni hali ya kawaida wakidai hayo huenda ni matukio tu yanawatokea hata watu wengine.


Mtoto huyo anaendelea kupatiwa huduma mbalimbali za kiafya ikiwa ni pamoja na chanjo za magonjwa mbalimbali katika zahanati ya Mwakitolyo.


Muuguzi wa zahanati hiyo Tizila Kijanda anasema hata wao wanashangaa na wanaendelea kumpatia matibabu kama kawaida

Wakazi wa eneo hilo wamelihusisha tukio hilo la imani za kidini hivyo ni mipango tu mwenyezi Mungu kwani yeye ndiye muweza wa mambo yote.

Na Malaki Philipo- RFA Na Malunde 1 Blog
Powered by Blogger.