WABUNGE WAFANIKISHA AZIMA YA KUMNG'OA WAZIRI MKUU


Leo June 1, 2018 Waziri Mkuu wa Hispania bwana Mariano Rajoy ameondolewa kwa lazima madarakani baada ya kupigiwa kura ya kutokuwa na imani na wabunge wa nchi hiyo.

Aidha Kiongozi msoshalisti Pedro Sanchez alieanzisha vuguvugu la kumng’oa kiongozi huyo baada ya kuhusishwa na skendo ya kula rushwa ndiye atakaye mrithi Rajoy.

“Tunaenda kufungua ukurasa mpya katika historia ya demokrasia ya nchi yetu” alisema Sanchez. Aidha Rajoy anaingia kwenye vitabu vya kumbukumbu ya taifa hilo kwa kuwa Waziri Mkuu wa kwanza kupigiwa kura ya kutokuwa na imani katika historia ya Hispania mpya
Powered by Blogger.