UWT SHINYANGA YACHANGIA DAMU SALAMA


Umoja wa wanawake wa CCM (UWT) Wilaya ya Shinyanga vijijini wakichangia Damu Salama kwenye hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga ,ili kupunguza uhaba wa Damu kwenye Hospitali hiyo na kuokoa Vifo vitokananvyo na Uzazi Sababu ya Uhaba wa Damu kwa akina Mama Wajawazito na watoto wadogo
Katibu wa Umoja huo wa wanawake wa CCM Grace Haule akiongoza Jopo hilo kuchangia Damu Salama kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akishirikiana na Umoja huo wa wanawake wa CCM Shinyanga Vijijini Kuchangia Damu Salama na kufanikiwa kupata Uniti 21.
Zoezi la utoaji Damu Likiendelea
Kaimu Mratibu wa Damu kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga Felix Manda akitoa Maelekezo mara baada ya kumaliza Kuchukua damu Salama.
Zoezi la uchukuaji Vipimo likiendelea kabla ya kuanza kutoa Damu Salama ilikubaini Kama mtu huyokama Afya yake ina mruhusu kutaoa damu.
Uchukuaji vipimo ukiendelea na baada ya hapo damu hutolewa ilikuhakikisha tatizo la Vifo vya Mama Mjamzito na Watoto vinapungua Mkoani Shinyanga Sababu ya Uhaba wa Damu Salama.
 
SOMA HABARI KWA KINA

Umoja wa wanawake wa chama cha Mapinduzi Ccm (UWT) wilaya ya Shinyanga vijijini umechangia utoaji wa damu salama kwenye hospitali ya Rufaa ya mkoani hapa, kwa lengo la kuondoa vifo vya Mama na Mtoto vitokanavyo na uzazi sababu ya uhaba wa damu.
Hospitali hiyo ya Rufaa inakabiliwa na tatizo la uhaba wa damu asilimia 100 ikiwa bohari yake ina uniti 25 za damu salama, huku uhitaji ikiwa ni Uniti 20 kwa Siku moja, hali ambayo ni hatari hususani kwa akina mama wajawazito na watoto ambao ndio watumiaji wakubwa wa damu hiyo.

Akizungumza juzi wakati wakichangia damu hiyo salama Katibu wa umoja huo wa wanawake Grace Haule, alisema wameamua kufanya zoezi hilo ilikupunguza tatizo la uhaba wa damu salama kwenye hospitali hiyo ya rufaa, hali ambayo itaondoa ama kupunguza vifo vya mama na mtoto vitokanavyo na ukosefu wa damu mwilini.

“Sisi umoja wa wanawake UWT Shinyanga vijijini tumeguswa na tatizo la uhaba wa damu salama kwenye hospitali ya Rufaa ya mkoa, na kufanikiwa kupata uniti 21 ambayo itasaidia kuokoa vifo vya wagonjwa wenye uhitaji wa damu,” alisema Haule

Naye kaimu mratibu wa Damu Salama kutoka Hospitali ya Rufaa mkoani humo Felix Manda aliupongeza umoja huo wa wanawake wa (CCM) Kwa moyo waliouonyesha wa kuchangia damu, ikiwa hospitali hiyo inakabiliwa na tatizo hilo kwa asilimia kubwa ambapo inatakiwa kwa wastani kuwe na Uniti 150 kwa wiki.

Aidha Mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga dk Ntuli Kapologwe alitoa takwimu za vifo vitokananavyo na uzazi kwa akina mama wajawazito, kuwa mwaka (2014) vilikuwa vifo 80 na (2015), vifo vilikuwa 60 huku akitoa wito kwa wananchi kuendelea kujitokeza kwa wingi kuchangia damu salama ilikumaliza vifo hivyo.

HABARI NA MARCO MADUHU MSUKUMA BLOG

Powered by Blogger.