DC AINGIWA HOFU MWAKANI KUWEPO UHABA MKUBWA WA MADAWATI
![]() |
Wakwanza kushoto ni Meneja wa Benki ya CRDB Said Pamui akishikana mkono na mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine matiro kama ishara ya kumkabidhi madawati hayo 50 na mwenyesuti nyeus katika ni Meya wa manispaa ya shinyanga Gulaam Mukadam akifuatiwa na mkurugenzi wa halmshauri ya manispaa ya shinyanga Lewis Kalinjuna wakishuhudia zoezi hilo la kukabidhi madawati 50 yenye thamani ya Milioni 5.5 |
SOMA HABARI KAMILI
Mkuu wa wilaya
ya shinyanga Josephine Matiro ameingiwa na hofu ya kuwepo na uhaba mkubwa wa
madawati mashuleni mwaka 2017 kutokana na wananchi kuitikia suala la elimu bure
na kupeleka watoto wao kwa wingi kupata elimu wakiwamo na wafungaji ambao
walikuwa wakiipatia elimu kisogo.
Matiro ameingiwa
na hofu hiyo kufuatia mwaka huu kuwepo na idadi kubwa ya wanafunzi mashuleni na
kufanya baadhi ya shule kuwepo na uhaba mkubwa wa vyumba vya madarasa pamoja na
uhaba huo wa madawati huku serikali
ikiendelea kuzitatua changamoto hizo moja baada ya nyingine.
Matiro
alizungumza hayo wakati akipokea
madawati 50 yalitolewa na benki ya CRDB tawi la Shinyanga mjini kwa lengo la
kuunga juhudi za serikali la kumaliza tatizo la uhaba wa madawati mashuleni,
kuwa mwakani ana hofu ya changamoto hiyo
kuongezeka kutokana na wananchi kuitikia suala la elimu.
“Nimeingiwa na
hofu kuwa mwakani kuna uwezekano wa tatizo la uhaba wa madawati mashuleni
likawa kubwa zaidi kutokana na wananchi kuwa na muitikio mkubwa wa kupeleka
watoto wao kupata elimu tofauti na miaka iliyopita,” alisema Matiro na kuongeza
kuwa
“hivyo naomba
wananchi na wadau wa maendeleo muendelee kuchangia utengenezaji wa madawati mashuleni,
msichoke ilituweze kuwa na madawati ya ziada hata kama idadi ya wanafunzi
ikiongezeka mwakani tatizo la wanafunzi kusoma wakiwa wamekaa chini liwe
historia.”
Naye Meneja wa
benki hiyo Said Pamui alisema madawati hayo 50 yamegharimu kiasi cha shilingi
milioni 5.5 na wamekuwa na huduma ya kuchangia shughuli za maendeleo kwa
wananchi kama kurudisha fadhira kwa wateja
huku akiahidi kuendelea kushirikiana na serikali kumaliza matatizo ndani
ya jamii.
Kwa upande wake
Ofisa Elimu ufundi wa halmashauri ya manispaa ya Shinyanga Mhela Mohamedi
alisema awali kabla hawajapokea madawati hayo 50 kutoka benki ya CRDB walikuwa
na upungufu wa madawati 1,969 lakini mpaka sasa wanakabiliwa na uhaba wa
madawati 1,919
Na Marco Maduhu- Msukuma Blog.