JAMII IMEONYWA KUGEUZA VITEGA UCHUMI WATOTO WA KIKE
![]() |
Wadua wa maendeleo mkoani Shinyanga wakiendelea kujadili namna ya kupambana na vitendo vya ukatiri mkoani Shinyanga hasa kukomesha ubakaji,ulawiti,mimba na ndoa za utotoni. |
![]() | |||||
Wadau wa maendeleo wakiwa makini kusikiliza mikakati mbalimbali inayopangwa juu ya kukomesha matendo ya ukatiri mkoani Shinyanga ambayo inaongoza kwa aslimia 59. ikifuatiwa tabora 58 na mara 55. |
SOMA HABARI KWA KINA
Wananchi mkoani hapa hususani
wale wanaoishi maeneo ya vijijini, wameonywa kugeuza watoto wao wa kike vitega
uchumi kwa kuwaodhesha wakiwa na umri mdogo huku wakiwakatisha masomo yao kwa
tamaa ya kupata mali hasa mifugo, wametakiwa kuacha tabia hiyo ikiwa ni
ukweukwaji wa haki ya mtoto.
Hayo
yamezungumzwa na wadau wa maendeleo mkoani Shinyanga kwenye kikao cha kujadili
namna ya kupanga mikakati ya kumaliza tatizo la mimba na ndoa za utotoni, ambapo
mkoa huo unaongoza kwa asilimia 59,ikifuatiwa tabora 58, na yatatu ni mara 55.
Baadhi ya wadau
hao David Nkulila na Maduhu Emmanuel wakizungumza kwenye kikao hicho kilicho andaliwa
na Shirika la Agape linalotetea haki za watoto mkoani shinyanga, walisema
tatizo ambalo limekuwa likisababisha vitendo hivyo kushika kasi ni jamii
yenyewe kwa kugeuza watoto wa kike vitega uchumi.
“Tatizo hili la
mimba na ndoa za utotoni kukithiri mkoani shinyanga linasababishwa na jamii
yenyewe kwa kugeuza watoto wao wa kike vitega uchumi kwa kuwaodhesha kwa tamaa
ya kupata mifugo mingi bila ya kujali anaumri mdogo wao wanacho thamini ni
kupata mali,”alisema Nkulila
Aliongeza”
ilikumaliza tatizo hili wananchi wapewe elimu ya kutosha juu ya madhara ya
kuodhesha mtoto mdogo pamoja na kuwachukulia hatua kali za kisheria wazazi
wenye tabia hiyo na kuwasweka rumande jambo ambalo litakuwa fundisho ikiwa
jamii yetu imeshazoea mpaka mtu mmoja atolewe mfano.”
Hata hivyo wadau
hao pia walivitaka vyombo vya maamuzi mkoani humo kuacha tabia ya kuchezea kesi
hizo za mimba, ubakaji,ulawiti na ndoa za utotoni bali wanatakiwa kuwa kitu
kimoja kwa kuzitolea hukumu haraka na kuwafunga watuhumiwa, kitendo ambacho
kitakomesha ukatiri huo mkoani shinyanga.
Naye hakimu wa
mahakama ya mwanzo kata ya usanda shinyanga vijijini Evalyn Polle, alisema kesi
nyingi za namna hiyo wamekuwa wakishindwa kuzitolea hukumu kutokana na jamii
yenyewe kulindana ambapo wamekuwa wakimalizana kimyakimya na hivyo mahakama
kukosa ushahidi wa kutosha na kumwachia huru mtuhumiwa.
Kwa upande wake
mkurugenzi wa shirika la Agape John Myola aliiomba serikali kushirikiana nao
kikamilifu kupiga vita ukatili huo, kwakutoa maamuzi magumu hasa kwa viongozi
wa ngazi za chini, vitongoji, mitaa na vijiji ambao ndio wamekuwa wakibariki
vitendo hivyo kwa kuwalinda waharifu.
Na Marco Maduhu- Msukuma blog