Mkurugenzi wa halmashauri ya shinyanga vijijini Kiomon Kibamba akimsalimia diwani katika hospitali ya rufaa ya mkoa
SOMA HABARI KWA KINA.
Jeshi la Polisi mkoani shinyanga lina
mshikilia mwalimu mkuu wa shule ya msingi Itubamilo shinyanga vijijini
Paulo Msakabili, kwa tuhuma za kumshambulia diwani viti maalumu Mengi
Charles mara baada kutofautia kauli kwenye kikao cha harusi.
Tukio
hilo limetokea juzi ambapo diwani huyo alikuwa na mwalimu mkuu kwenye kikao cha harusi na wajumbe wengine wa
kamati tendaji wakijadili mikakati ya kufanikisha harusi ya ndugu yao ambapo
mkuu huyo wa shule alitaka kamati ya mapambo apewe yeye lakini diwani alipinga
na uhasama ukaanzia hapo.
Akielezea
tukio hilo kwa shida huku akiwa amelezwa kwenye hospitali ya rufaa ya mkoa wa
shinyanga diwani Chalres alisema baada ya kikao hicho cha harusi kuisha ndipo
mwalimu huyo alipomfuata na kumkata mtama na kuanza kumshambulia sehemu za
kichwani na kumsababishia maumivu makali na kuharibu jicho lake la kushoto.
“Ugomvi
uliibuka pale nilipopinga mwalimu huyo kupewa kamati ya mapambo ambapo alidai
kunamtu anamfahamu ampe na kumtaka aje na huyo mpambaji iliwajumbe wa kamati
tendaji wamuone na kumuhoji pamoja na kufahamu gharama zake lakini Mwalimu huyo
alikuja juu na kuanza kunishambulia,”alisema Charles
Aidha
kaimu mganga mfawidhi wa hospitali ya rufaa mkoani shinyanga dkt Mwita Ngutunya
alikiri kumpokea diwani huyo na kudai
kuwa hali yake ni mbaya hasa kwenye jicho lake la kushoto na taya ambapo
wamempatia rufaa ya kwenda kutibiwa bugando jijini mwanza kwa matibabu zaidi.
Kwa
upande wake kaimu kamanda wa jeshi la polisi mkoani shinyanga Graifton Mushi
alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na mtuhumiwa wanamshikilia na upelelezi
ukikiamilika na kubainika anakosa atafikishwa mahakamani kujibu shitaka la
kushambulia mwili.
Na Marco Maduhu- Msukuma Blog
|