ASKARI AFUKUZWA KAZI KWA RUSHWA
Askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani ambaye anaonekana akiomba rushwa kwenye mkanda wa video uliosambaa mitandaoni kuanzia mwishoni mwa wiki, ametimuliwa kazi na Jeshi la Polisi Zanzibar.
Sajini Hamad Kassim wa Kituo cha Mkokotoni visiwani hapa, amefukuzwa kazi kwa tuhuma za kuomba rushwa.
Kwenye mkanda huo, askari anaonekana akizungumza na mwanamke mwenye Kiswahili kibovu na kujadiliana naye kuhusu kosa lake na kupewa ushauri wa jinsi ya kuepuka askari wengine.
Hilo ni tukio la pili mwaka huu, baada ya askari mwingine wa kikosi hicho mkoani Tanga kutimuliwa baada ya kurekodiwa akiomba na kupokea rushwa.
Jana, Kassim alikamatwa na polisi jana baada ya kutuhumiwa kuomba na kupokea rushwa kutoka kwa raia wa kigeni baada ya kumkamata akiwa hajafunga mkanda wakati akiendesha gari.