KOCHA WA MWADUI JULIO KIWELU ATANGAZA KUJIUZULU KUFUNDISHA SOKA TANZANIA


Kocha wa klabu ya Mwadui FC ya Shinyanga Jamhuri Kiwelu Julio jioni ya Oktoba 2 2016 alitangaza maamuzi ya kuwashtusha walio wengi, hiyo ni baada ya mchezo wake wa ugenini kati ya Mwadui FC dhidi ya Mbeya City kumalizika kwa kupoteza kwa goli 1-0.

Julio baada ya mchezo huo uliochezwa katika uwanja wa Sokoine Mbeya alitangaza kuachana na soka la Tanzania, hiyo inatokana na kutoendelea kuridhishwa na uwezo wa waamuzi wa soka wa Tanzania, kwani katika mchezo dhidi ya Mbeya City amekiri kuwa walifungwa kihalali lakini muamuzi alionesha kuwawekea vikwazo wasisawazishe.
 
 "Natumia nguvu nyingi kufundisha, kampuni inatumia pesa nyingi kugharamia timu, tunasafiri safari ndefu halafu mwisho wa siku waamuzi wanafanya upendeleo wa wazi wazi",alisema Julio.

“Mchezaji wetu anapambana hadi anapata mpira kwenda kufunga refa badala yake anatoa faulo kwao kwenye timu ya adui kusema kweli kimeniuma sana, kwa hiyo nitangaze rasmi kuanzia sasa hivi na kuendelea mimi sitaki kuwa kocha wa mpira wa miguu katika soka la Tanzania tena”
Powered by Blogger.