Makamu wa rais awacharukia wanasiasa wanaopinga maendeleo




MAKAMU wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema ametangulia Iringa kuja kusafisha njia ya ujio wa Rais Dkt John Magufuli huku akikemea wanasiasa wanaopinga maendeleo.

Kuwa suala la maendeleo halina chama hivyo anayepinga maendeleo au kuhujumu miradi ya maendeleo hafai katika jamii.
Akiwahutubia wananchi wa Manispaa ya Iringa Leo katika viwanja vya Mwembetogwa ,makamu wa Rais amesema kuwa kazi yake ni ya Yohana Mbatizaji hivyo amekuja kusafisha njia ili aweze kuja Iringa.

Pia alisema Rais anawapongeza wakazi wa Iringa na watanzania kwa kuendelea kudumisha amani pia jinsi wanavyojituma kufanya kazi.

Alisema serikali ya awamu ya tano imeendelea kuwatumikia watanzania na itaendelea kufanya hivyo kama njia ya kuwakomboa watanzania.

Makamu wa Rais alisema Mkoa wa Iringa umepiga hatua kubwa katika sekta ya elimu na upatikanaji wa huduma ya maji safi na Salama pamoja na usogezaji wa umeme vijijini.

"Nineshuhudia mazuri Mengi katika Mkoa wa Iringa kwa utunzaji wa mazingira kwa kiasi kikubwa na uharibifu kwa kiwango cha chini"

Alisema changamoto kubwa kwa Mkoa wa Iringa ni barabara na kuwa barabara zote za Tanroads na zile za Tarula zitajengwa.

Aidha aliwataka wananchi wa Iringa kujiunga na kilimo cha Korosho kwani ni moja kati ya mazao yenye uchumi mzuri zaidi.

Kuwa zao hilo linamwezesha mwananchi kuvuna miaka yote tofauti na mazao mengine.

Kuhusu wajasilia Mali alisema kuwa serikali kwenye ilani yake imetamka wazi kuwa itaendelea kurasilimisha biashara zao kwa kuwatengea maeneo na kuwaunganisha na mifuko ya jamii .

"Nawaombeni sana Halmashauri kufunga barabara ambazo hazitumiki sana kwa wiki Mara moja kufanya shughuli zao japo suluhisho ni kuwatengea maeneo rasmi yenye miundo mbinu sahihi na waweze kulipa kodi"


Japo alisema katika sekta ya elimu ni mabweni ya wanafunzi na uchakavu wa nyumba za walimu ambazo pia zitatatuliwa.


Aidha alisema hajaridhiwa na baadhi ya maeneo juu ya usimamizi wa raslimali za umma kama vyanzo vya maji na wabunge kulinda waharibifu wa vyanzo vya maji.


Vyanzo vya maji haviletwi na serikali hivyo lazima vyanzo hivi vilindwe hivyo si sahihi kuona vyanzo vya maji vinaharibiwa.


Kuendelea kukata miti ovyo ni uharibifu wa raslimali za umma hivyo wale wasiopanda miti marufuku kukata miti anayepanda miti ndie avune miti.


"Nawaomba sana viongozi tokeni ofisini nendeni kusimamia raslimali za umma"


Pia suala la unyanyasaji na ukosefu wa Haki kwa wanyonge naomba suala hili lisiendelee kuwepo katika jamii yetu.


Hata hivyo makamu wa Rais alitaka suala la usimamizi wa pesa za makusanyo ya ndani kufuatiliwa na kuona pesa hizo zinatumika katika miradi ya maendeleo.


"Asilimia 10 ya vijana na wanawake zitumike vema na vitatue changamoto zao sio zitumike kununua madela au kufanya starehe"


Makamu wa Rais amekemea suala la upinzani katika maendeleo .


"Utakuta Leo ametokea mwendawazimu mmoja ambae kichwa hakipo sawa anataka wananchi kususia maendeleo niwaeleze wazi maendeleo hayana chama naomba mheshimiwa mkuu wa Mkoa kama kuna tatizo la watu wa aina hiyo tukuletee watu wa saikolojia ili waje Iringa kutoa elimu ya saikolojia"


Suala la ushirikiano wa viongozi kwa viongozi lazima uwepo kwani sitegemei unakwenda sehemu viongozi wananunuana.


Japo napenda kuwapongeza viongozi na wananchi kwa kuwa na viwanda vingi zaidi .


"Iringa mpo juu sana kwa viwanda mlianza zamani sana na sasa mnaendelea na juhudi za uanzishaji wa viwanda kama mnavyoendelea"


Makamu wa Rais alisema juu ya maombi ya Halmashauri yaliyotolewa na Mstahiki meya Alex Kimbe na mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela likiwemo la mkwamo wa Machinjio atalitolea jibu kesho.


Makamu wa Rais anataraji kumaliza ziara take kesho kwa kufanya majumuisho ya ziara yake
 
Powered by Blogger.