JINSI BODABODA SHINYANGA ALIVYOUAWA KINYAMA
Dereva wa bodaboda anayefahamika kwa jina la Amani Mkumbo (45) mkazi wa Mtaa wa Mabambasi kata ya Ndembezi mjini Shinyanga ,ameuwawa kwa kupigwa na kitu chenye ncha kali kichwani na kumcharanga kwa panga maeneo mbalimbali ya mwili wake na watu wasiojulikana.
Imeelezwa bodaboda huyo baada ya kuuawa, watu hao wasiofahamika walifanikiwa kumnyang’anya pikipiki yake yenye namba za usajili MC 883 BSL na kisha kuondoka nayo.
Kaimu kamanda wa jeshi la polisi mkoani Shinyanga ambaye pia ni mkuu wa polisi wilaya Shinyanga(OCD) Claud Kanyorota, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo ambalo limetokea juzi majira ya saa 5.45 usiku katika kijiji cha Imalilo kata ya Kitangili mjini humo, eneo ambalo alikuwa amewapeleka wateja wake .
Kanyorota alisema kuwa dereva huyo aliuwawa kwa kupigwa na kitu chenye ncha kali kichwani na kumcharanga kwa panga maeneo mbalimbali ya mwili wake ,na abiria wake ambao alikuwa amewapakiza mshikaki , na alifariki wakati akikimbizwa kupewa matibabu kwenye hospitali ya rufaa Mkoani Shinyanga.
“Ninachowaomba madereva wa bodaboda wachukue elimu waliyopewa na jeshi la polisi waache kufanya kazi nyakati za usiku ,"alisema Kanyorota.
Naye Ramadhani Shija mwendesha bodaboda, alisema kuwa wimbi la mauaji la kutekwa madereva limeanza kuibuka tena ,kwani awali lilishamiri ambapo jeshi la polisi lilifanikiwa kulimaliza.
Mwenyekiti wa waendesha bodaboda mkoa wa Shinyanga Wenceslaus Modest ,alisema kuwa marehemu sio mwanachama wao ila madereva wote waendesha bodaboda walikwisha pewa elimu ya kujilinda na kutoendesha Pikipiki nyakati za usiku.
Mke wa marehemu Josephine Kitundu alipohojiwa alidai kuwa mume wake huwa anakawaida ya kurudi usiku katika kazi yake hiyo ila juzi kabla ya tukio hilo aliondoka kwenda kwenye kazi yake akiwa salama alishangaa kuona majira ya saa sita usiku baadhi ya askari kumfuata nyumbani kwake akiwa amelala bila kumwambia chochote nakutaka aende atoe maelezo kituo cha polisi dhidi ya mume wake.
“Nilikuwa nimelala nikasikia napigiwa hodi majira ya saa sita usiku nilipofungua mlango walikuwa ni maaskari walionifuata nakunieleza niondoke nao mpaka kituoni bila kunieleza chochote nilipofika wakaniambia nitoe maelezo ya mume wangu ila hawakuniambia kama amefariki walichonieleza niwahi alfajiri hospitali ya rufaa kumbe alikuwa amekwisha fariki”alisema Kitundu.
Na Marco Maduhu