SERIKALI SHINYANGA YAVUNJA MIKATABA JENZI ZA BARABARA
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainabu Telack akizungumza kwenye ufunguzi wa kikao cha bodi ya barabara mkoani Shinyanga na kuagiza wakandarasi ambao hawana sifa wasipewe kazi mkoani humo kwani wanadumaza ukuaji wa maendeleo ya mkoa huo ikiwa barabara ni kiungo muhimu katika mji unaotaka kukua kimaendeleo.
NA MARCO MADUHU- SHINYANGA
Serikali mkoani Shinyanga imelazimika kuvunja mkataba wa ujenzi wa barabara na makandarasi wa kampuni ya (Termite Investment) ya dar e s salaamu, mara baada ya kushindwa kufanya kazi yake kwa ufanisi kwa mjibu wa mkataba na kusuasua kwenye ujenzi huo.
Mkandarasi huyo alipewa mkataba na Serikali ya mkoa huo katika mwaka wa fedha (2016-17 ) kiasi cha Shilingi 314,834,505.00 kwa ajili ya kujenga barabara za Kata ya Kambarage, Ndala na Masekelo kiwango cha changalawe kwa muda wa siku 120, lakini imedaiwa utendaji wake kazi ulikuwa siyo wa kuridhisha.
Hayo yalibainishwa Februari 13 mwaka huu na mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainabu Telack, wakati akisoma hotuba kwenye ufunguzi wa kikao cha bodi ya barabara mkoani humo, kuwa Serikali imeshavunja mkataba na mkadarasi huyo, na kumtafuta mwingine kutokana na kutokuwa na sifa za ukandarasi.
“Mkandarasi huyu wakati wa utekelezaji wake kazi aliacha vifusi barabarani ndani ya miezi miwili na kuleta ufumbufu kwa wananchi, na tulipombana alisambaza vifusi na kisha kusimamisha kazi bila hata ya kutoa taarifa , hivyo tukaona ni vyema kuvunja naye mkataba ili apatiwe mwingine,”alisema.
Aliongeza katika halmashauri ya Msalala wilayani Kahama waliingia mkataba wa Shilingi 397,734,600.00 na umoja wa Makandarasi Tingwa Co Limited na Derick Co Limted kwa ajili ya matengenezo ya barabara, ambapo wakandarsi hao walifanya kazi yenye thamani ya shilingi 123,569,600.00 na kuishia hapo.
Alisema halmashauri ilishindwa kuwalipa shilingi 57,404,600.00 na kusababisha wakandarasi hao kushindwa kumaliza kazi kwa muda uliopangwa, jambo lililosababisha wakandarsi hao kushindwa kufanya kazi kwa muda uliopangwa na hatimaye halmashauri kuvunja mkataba na mkandarasi.
“Nataka kuwaambia wasimamizi mnaosimamia matengenezo ya barabara hakikisheni mnasimamia kikamilifu matengenezo hayo, kwa kuzingatia sheria na kanuni za ujenzi wa barabara, na ikibainika mkandarasi amefanya kazi chini ya kiwango sitamruhusu aendelee kufanya kazi mkoani hapa,”alisema Telack.
Aliongeza kwa kuwataka wakurugenzi wa halmashauri mkoani humo kutowapatia kazi wakandarasi wasio na sifa, ambao wamekuwa chanzo cha kuudumaza mkoa huo kimaendeleo, sababu ubora wa barabara ndio kichocheo cha uchumi kukua kwa wananchi na mkoa kwa ujumla.
Pia aliwataka wakurugenzi, wakuu wa wilaya ,mawakala wa barabara Tanroad na Tarura kutoa elimu kwa wananchi juu ya matumizi ya barabara na kuacha kuharibu miundombinu yake, ikiwamo kulima kandokando ya barabara kufanyia biashara, kuchungia mifugo, hali ambayo imekuwa ikiigharimu fedha Serikali ya kufanya matenegenzo ya mara kwa mara.
Nao baadhi ya wajumbe waliohudhulia kikao hicho waliipongeza Serikali kwa uwamuzi waliouchukua juu ya wakandarasi wazembe, kupitia wakala wake wa barabara za vijijini na mijini Tarura, pamoja na kuiomba Serikali iongeze kasi ya ujenzi wa barabara mkoani humo kwa kiwango cha lami, ikiwamo ya Kolandoto, Kishapu hadi Arusha.
Kwa upande wake kaimu meneja wa barabara Tanroad mkoani Shinyanga mhandisi Mibara Ndirimi, alisema Serikali katika mwaka wa fedha (2017-18) imeshatenga jumla ya shilingi 12,650,863, kwa ajili ya ujenzi wa barabara pamoja na shilingi 11,322,863 kwa ajili matengenezo ya barabara na madaraja, na kubainisha kuwa ujenzi wa barabara Kolandoto hadi Arusha bado mchakato wake unaendelea.
TAZAMA PICHA CHINI KIKAO BODI YA BARABARA
Kaimu meneja wa Tanroad mkoani Shinyanga mhandisi Mibara Ndirimbi akizungumza kwenye kikao hicho cha bodi ya barabara changamoto wanazokumbana nazo kwenye matunzo ya barabara kuwa ni wananchi kufanyabishara zao kandokando ya barabara,shughuli za kilimo, kuchungia mifugo na hivyo kufanya Serikali kuingia gharama za matenezo ya barabara hizo mara kwa mara , huku akibanisha kuwa kwa mwaka wa fedha 2017-18 jumla ya fedha shilingi 11,322,863 zitatumika kwenye matengenzo ya barabara pamoja na madaraja.

Mkuu wa wilaya ya kishapu Nyabaganga Taraba akizungumza kwenye kikao hicho cha bodi ya barabara na kutaka elimu itolewe kwa kwa wananchi kuacha tabia ya kufanyashughuli zao kandokando ya barabara pamoja na kuacha kucheza kwenye barabara hizo hasa nyakati za usiku ambapo kuna baadhi ya wananchi wamekuwa wakicheza na kulala kwenye barabra hizo na kuhatarisha maisha yao.
Amesema wakati akija kwenye kikao hicho alipofika njiani alikutana na gari Kata ya Uchunga likiwa limegonga watoto wawili ambapo mmoja alifariki papo hapo na mwingine kuvunjika miguu, huku pia akiomba Serikali iiweke kwenye mpango kutengeneza barabara ya Kolandoto kwenye kishapu kwa kiwango cha Lami ambapo barabara hiyo ni kitega uchumi mkubwa wa mkoa wa Shinyanga.
Naye Kaimu meneja Tarura mkoa wa Shinyanga Ezekiel Nyaranyara akisoma taarifa na kuelezea kazi za Tarura ambao ni mawakala wa barabara za vijijini na mijini ambayo ilianzishwa rasmi kwa mujibu wa Sheria ya wakala za serikali za serikali sura 245 na kutangzwa rasmi na gazeti la Serikali 12/5/2017, ambao wamechukua majukumu ya kiutendaji kuhusiana na ujenzi na matenegezo ya mtanadao wa barabara vijijini na mijini ambayo yalikuwa yakitekelezwa na mamlaka za serikali za mitaa( MSM) na kuratibiwa na idara ya miundombinu chini ya wizara ya OR-TAMISEMI
wajumbe wakiendelea na kikao cha bodi ya barabara
Wajumbe wakisikiliza maagizo ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga na kuchukua ndoo ndoo muhimu juu ya kutofanya kazi na wakandarasi wasio na sifa pamoja na kutoa elimu kwa wananchi kutoharibu miundombinu ya barabara ambayo imekuwa ikiigharimu fedha nyingi serikali
Kushoto ni mwenyekiti wa halmashauri ya Kahama mji Abeli Shija akiwa na mbunge wa Jimbo la Msalala Ezekiel Maige wakipitia makablasha kwenye kikao cha bodi ya barabara .
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainabu Telack akitoa pia maagizo kuwa Kandokando ya barabara papandwe miti ilikuependesha madhari ya mkoa wa Shinyanga pamoja na kuzuia mmomonyoko wa udongo kutoharibu barabra hizo.

Mkurugenzi wa halmashauri ya manispaa ya Shinyanga Geofley Mwangulumbi akizungumza hatima ya mkandarasi Jasco anayejenga barabara za katikati ya mji wa Shinyanga kwa kiwango cha Lami kuwa baada ya changamoto zilizokuwa zinakwamisha kuendelea kwa jenzi na barabara hizo zimeshakwisha na ataingia site hivi karibuni