NYUKI WAVAMIA MAKABURINI WASHAMBULIA WAZIKAJI, WANG'ATWA MIDOMO
Katika
hali isiyo ya kawaida nyuki wa ajabu wameibuka na kushambuliwa
waombolezaji muda mfupi tu baada ya mwili wa Msanii wa nyimbo za asili
maarufu kwa jina la Kalanga "Ng'wana Kolagwa" kufikishwa katika kaburi
lake.
Msanii
Kalanga alifariki dunia siku ya Jumatano Februari 21,2018 majira ya saa
11 alfajiri nyumbani kwao katika kijiji cha Chambo - Mwamakumbi Nzega
mkoani Tabora baada ya kuugua muda mrefu.
Mazishi
yamefanyika jana Alhamis Februari 22,2018 nyumbani kwao majira ya saa
moja usiku baada ya waombolezaji kushindwa kumzika marehemu saa nane
mchana kutokana na kuvamiwa na kundi la nyuki.
Inaelezwa
kuwa baada ya mwili wa marehemu kufikishwa katika kaburi kwa ajili ya
mazishi,ghafla walitokea nyuki na kuanza kuwashambulia waombolezaji na
kusababisha taharuki kubwa kila mmoja akitafuta mahali pa kujificha.
Hata hivyo baada ya balaa hilo la zaidi ya saa tatu wazee walifanya tambiko na kufanikiwa kumzika marehemu.
Mbali
na tukio hilo kuhusishwa na imani za kishirikina/kichawi ,Wataalamu wa
mambo wanasema mila na desturi za uzikaji wa ma manju/wasanii wa nyimbo
za asili zilikiukwa.
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Msanii Kalanga "Ng'wana Kolagwa" enzi za uhai wake
Mwili wa marehemu Kalanga ukiingizwa kaburini
Waombolezaji wakiondoka kaburini baada ya nyuki kuibuka kaburini
Waombolezaji wakitawanyika
Nyuki balaa...kila mtu anapambana na hali yake....
Mmoja wa waombolezaji akionesha jinsi mdomo ulivyoshambuliwa na nyuki