WAKUU WA SHULE ZA SEKONDARI SHINYANGA WAMEONYWA KUTONGOZA WALIMU WA KIKE

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainabu Telack akifungua kikao cha wakuu wa shule za sekondari mkoani Shinyanga (Tahosa), na kuwaonya walimu hao wakuu kuacha tabia ya kutongoza walimu wa kike, ikiwa mapenzi na kazi ni vitu viwili tofauti na hawatoweza kusimamia taaluma mashuleni.


SOMA HABARI KAMILI


Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Zainabu Telack, ameonya tabia kwa baadhi ya wakuu wa Shule za Sekondari Mkoani hapa, kuacha tabia ya kutongoza Walimu wa Kike .

Amesema Mkoa huo kunashida ya wakuu wa shule kuwa na mahusiano na walimu Kike, na hivyo kushindwa kusimamia taaluma vizuri na kusababisha wanafunzi kufanya vibaya kwenye mitihani yao ya kuhitimu.

Telack aliyabainisha hayo Febrauri 15 kwenye kikao cha Walimu wakuu wa Shule za Sekondari Mkoani Shinyanga, (Tahosa )wakati wakifanya Tathimini ya matokeo ya kidato cha Nne mwaka 2017, pamoja na kujadili changamoto na kuzitatua ilikuongeza ufaulu kwa wananfunzi.

Alisema mkuu wa Shule anapoingia kwenye mahusiano na Mwalimu wake, kamwe hawezi kusimamia taaluma ikiwa atashindwa kumkanya mwalimu ama kumpatia adhabu, pale anapokuwa akipuuzia kufundisha .

"Suala hili nalizungumza kwenu sababu nimepewa taarifa kuwa wakuu wa Shule wanatabia ya kufanya mapenzi na Walimu wa Kike, tabia hiyo naomba ikome, tafuteni wadada mitaani siyo Walimu wenu," alisema.

Aliongeza kwa kuwataka wakuu hao wa Shule, kukaa vikao na Walimu wa kiume kuacha tabia ya kutongoza wanafunzi wa Kike ,na atakaye patikana kufanya vitendo hivyo Serikali itamshughulikia.

Aidha aliwataka wakuu hao wa Shule kuendelea kusimamia taaluma ya ufundishaji mashuleni, licha ya kukabiliwa na changamoto mbalimbali, wakati Serikali ikiendelea kuzitatua moja baada ya nyingine.

Nao baadhi ya wakuu wa Shule za Sekondari waliahidi kuzingatia maagizo hayo ,huku wakibainisha baadhi ya changamoto ambazo zimekuwa zikisababisha wanafunzi kufanya vibaya, kuwa ni ubovu wa miundombinu ya Shule, utoro  ukosefu wa vyakula, na uhaba wa Walimu wa Sayansi.

SOMA  HABARI PICHA HAPA CHINI

, Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainabu Telack akiwataka pia wakuu hao wa shule kuacha kuwa na makundi ya walimu mashuleni pamoja na kuondoa ukilitimba bali wawe na mahusiano mazuri na walimu pamoja na wanafunzi ili pale kwenye shida wajadiliane kwa pamoja na kuitatua  na siyo kujifanya wao ndio ma mwinyi mashuleni.

Pia amewaagiza maofisa elimu wote kuacha tabia ya kukaa maofisi bali wafanya ukaguzi mashuleni kwa kuzitembelea na kuzungumza na walimu changamoto zinazo wakabili na kuzitatua ili kuendelea kuboresha ukuaji wa elimu mkoani Shinyanga .



Ofisa elimu taaluma mkoa wa Shinyanga James Malima akizungumza kwenye kikao hicho na kuagiza wakuu hao wa shule marufuku kujichukulia kibali cha kukalilisha wanafunzi na wala kuwepo na upigaji picha kwa wanafunzi wanaotarajiwa kuhitimu ikiwa zoezi hilo litakuwa likifanywa na wataalamu kutoka baraza la mitihani pamoja na picha hizo kugharamikiwa na Serikali kasoro tu shule za binafsi.

Pia alitaja shule Kumi zilizofanya vizuri katika matokeo ya kidato cha Nne mwaka 2017 na kuufanya mkoa kushika nafasi ya Nne kitaifa katika ya mikoa 31 kuwa ni shule za Underlake. Kwema, St Tereza, Komu, Donbosco, Shybush, Mhongolo, John Paulo, pamoja na Lwepazi

Pia alitaja shule Kumi zilizofanya vibaya kwenye matokeo hayo ya kidato cha Nne kuwa ni,Ngitile, Kolandoto, Tinde, Gembe, Town, Kishapu, Oldshinyanga, Mwasele, Ibinzamata, pamoja na Shingita.


Ofisa elimu mkoa wa Shinyanga Mohamed Kahudi akizungumza kwenye kikao hicho na kuwataka  wakuu hao wa shule wasimamie ufundishaji pamoja na kuwapatia taarifa wazazi juu ya maendeleo ya watoto wao, ikiwamo na kutolea masuala ya utoro ambapo mtoto akifikisha siku 90( Miezi Mitatu hajaonekana shule afukuzwe


Ofisa elimu mkoa wa Shinyanga Mohamed Kahundi akisistiza wakuu wa shule za sekomdar mkoani Shinyanga kuzingatia michezo mashuleni huku akizionya baaadhi ya shule binafsi ambazo zimekuwa zikipuuzia suala la michezo na kubainisha michezo ni moja ya kumwandaa mwanafunzi kufanya vizuri kitaaluma, na kusema mkoa huo kwenye matokea yake ya kidato cha Nne mwaka 2017 imeshika nafasi ya Nne kitaifa  na kuwataka walimu waongeze bidii ya ufundishji ilikurudi kwenye nafasi yake ya kwanza au ya pili
Walimu wa shule kumi zilizofanya vibaya kwenye matokeo ya kidato cha Nne mwaka 2017, wakiwa wamesimama mbele ya wenzao kujieleza kwanini wamefelisha sana wanafunzi na shule hizo niNgitile, Kolandoto, Tinde, Gembe, Town, Kishapu, Oldshinyanga, Mwasele, Ibinzamata, pamoja na Shingita.

Aliye simama wa pili kutoka mkono wa kushoto ni mkuu wa shule ya Sekondari Oldshinyanga Joseph Maiga, ametaja changamoto zilizosababisha wanafunzi wake kufanya vibaya katika matokeo hayo ya kidato cha Nne kuwa  ni uhaba wa walimu wa masomo ya sayansi, wanafunzi kutoka katika shule za msingi wakiwa hawajui kitu, pamoja na baadhi ya walimu kutokuwa na uwezo wa kufundisha.

Wa kwanza mkono wa kulia ni mkuu wa shule ya sekondari Mwasele  Peter Makula, amesema ubovu  wa miundombinu ya shule ndio imekuwa kikwazo kwa wanafunzi kufanya vibaya, pamoja na kuwepo na matamko ya viongozi kuzuia michango mashuleni na kufanya shule kuendelea kukabiliwa na hali ngumu ya ufundishaji, ukosefu wa kula chakula wanafunzi mashuleni, ubari mrefu, uhaba wa madawati, walimu waliopangiwa masomo husika ya kufindisha kutokuwa na uwezo ambapo alipokuwa akikagua madarasi anakuta walimu wakifundisha masomo hayo kwa kiswahili, na kuiomba serikali iandae semina elekezi ya kufundisha walimu hao namna ya kutoa elimu kwa wananfunzi.
Mkuu wa shule ya sekondari Shinyanga (SHYBUSH) James Malelemba akizungumza kati ya shule kumi zilizofanya vizuri kwenye matokeo ya kidato cha Nne mwaka 2017 na kuufanya mkoa kutoka kifua mbele kushika nafasi ya Nne kitaifa ambapo mwaka 2016 ilikuwa ya Tisa na kusema kuwa jambo la msingi kwa wanafunzi kufanya vizuri ni kuwa nao karibu kwa kusikiliza nini wanachotaka, kufanya majaribio ya mitihani mara kwa mara, ukaguzi wa walimu katika ufundishaji kwa kufuata Slybasi,walimu kujituma pamoja na kuwepo mazingira rafiki ya shule katika ufundishaji.
Wakuu wa shule za sekondari mkoani Shinyanga 140 wakiwa kwenye kikao cha TAHOSA, Wakisikiliza maagizo kutoka kwa viongozi wao wakuu namna ya kusimamia taaluma pamoja na kuwa wabunifuzi kwenye suala la ufundishaji ilikuweza kuunyanya mkoa kidedea kwenye matokea ya kuhitimu mitihani na hatmaye kuzalisha taifa la watu wasomi.
Mkuu wa shule ya sekondari Oldshinyanga Joseph Maiga akiuliza swali juu ya serikali kwanini hua wanachelewa kutoa Living Certificate mapema ambapo wanafunzi pale wanapokuwa wakipata nafasi za kujiunga na majeshi wamekuwa wakisumbua, ambapo alipewa majibu na ofisa elimu mkoa wa Shinyanga Mohamed Kahundi kuwa ,wakuu wote wa shule wanapaswa kuwa wabunifu kwa kutengeneza vyeti vyao hapo shuleni ya muda wakati wakisubili cheti hicho kutoka wizarani.
Wakuu wa shule za sekondari mkoani Shinyanga wakisiliza hotuba ya mkuu wa mkoa na kuagiza shule ambazo zina maeneo ya kulima chakula walime ilikuondoa changamoto ya ukosefu wa vyakula mashuleni na kubainisha kuwa yeye hatotoa kibali tena cha kuruhusu uchangiaji wa chakula ambapo Rais John Magufuli ameshapiga marufuku, huku wakitakiwa kijutuma licha ya kukabiliwa na changamoto hizo za ufundishaji pamoja na kutobeza suala la elimu bure na kushusha hali ya ufundishaji.
wakuu wa shule za sekondari mkoani Shinyanga wakiandika mawili matatu kwenye kikao hicho cha TAHOSA ambayo yatawasidia kwenye kumbukumbu zao na kuongeza juhudi za ufundishaji na kuongeza ufaulu kwa wanafunzi


Wakuu wa shule za sekondari mkoani Shinyanga wakisikiliza kwa makini maelekezo ya usimamizi wa taaluma mashuleni kwao, pamoja na kushirikisha bodi za shule kwenye kuzia masuala ya utoro mashuleni kwa wanafunzi.

Na Marco Maduhu




































Powered by Blogger.