SERIKALI KULIPA FIDIA KINGA BIMA YA MAZAO
Ofisa mwandamizi wa shirika la Bima ya Taifa kutoka
Makao Makuu jijini dare s salaamu Catherine Nangali kitengo cha Madai ya fidia
ya Magari na Kilimo akitoa elimu kwa wakulima hao juu ya umuhimu wa kujiunga na Bima hiyo ya Kinga ya
mazao.
SOMA HABARI KAMILI
Serikali kupitia Shirika la Bima la Taifa linatarajia kuzindua Bima ya Kinga ya Mazao kutoka kwa mkulima yakiwa Shambani, ambapo pale atakapo kosa kuvuna mavuno ya uhakika tofauti na misimu mingine iliyopita, Shirika hilo litamlipa fidia mapungufu hayo na kuendelea kumyanyua kiuchumi.
Hayo yalibainishwa Feb 14 mwaka huu kwenye Kata ya Kagongwa wilayani Kahama na Ofisa mwandamizi wa Shirika hilo kutoka makao makuu jijini Dar es salaam kitengo cha Madai ya fidia za magari na kilimo Catherine Nangali, wakati akitoa elimu kwa wakulima wa Kata hiyo juu ya umuhimu wa kujiunga na bima hiyo ikiwamo na ya majanga ya moto.
Alisema baada ya Serikali kuona wakulima wa hali ya chini wanakabiliwa na changamoto nyingi kwenye kilimo, ndipo wakaona kuna umuhimu wa kuanzisha bima ya kinga ya mazao, ambapo mkulima pale mazao yake yatakapokuwa shambani na kushambuliwa na wadudu, ukame, mbegu kutoota,kuzidiwa na mvua, atalazimika kulipwa hasara hiyo.
“Bima hii ya kinga ya mazao tutaizindua june mwaka huu, ambayo itamsaidia mkulima kufidiwa hasara zake pale anapozipata kwenye kilimo chake kwa kukosa mavuno ya uhakika, ambapo pia tunatarajia kuanza kutoa mikopo kwa wakulima, ili kuwawezesha kulima mashamba makubwa na kuinuka kiuchumi,”alisema.
Aliongeza kuwa kinachopaswa kwa mkulima atakaye jiunga na bima hiyo, ni kutunza kumbukumbu zake za mavuno kila msimu wa kilimo, ambapo siku mazao yake yakiandamwa na matatizo aweze kufanyiwa Tathimini na hatimaye kulipwa fidia ya hasara aliyoipata, na kumuokoa kutumbukia kwenye janga la umaskini.
Naye Ofisa wa shirika hilo la bima ya taifa kutoka makao makuu Prosper Peter kitengo hicho hicho cha bima za magari na kilimo, alitoa tahadhari kwa wakulima watakaojiunga na bima hiyo, kutotengeneza matukio ya kutofauta Sheria na Kanuni za kilimo iliwapate kulipwa fidia ambapo ikibainika hawatolipwa.
Nao baadhi ya wakulima waliohudhulia elimu hiyo Skolastika Laurent, aliipongeza Serikali kwa kuthamini wakulima wadogo kutaka kuwainua kiuchumi, na kubainisha kuwa bima hiyo itakuwa msaada mkubwa kwao, ikiwa kuna baadhi ya misimu ya kilimo imekuwa ikiwatia hasara kwa kukosa mavuno sababu ya mabadiliko ya tabia nchi.
SOMA HABARI PICHA HAPA CHINI
, Ofisa mwandamizi wa shirika la Bima ya Taifa
kutoka Makao Makuu jijini dare s salaamu Catherine Nangali kitengo cha Madai ya
fidia ya Magari, akiwaeleza wakulima hao ambao watajiunga na Bima hiyo ya Kinga
ya Mazao kuwa watapatiwa mafunzo na wataalamu wa kilimo kutoka wizarani ambao
wataambatana nao namna ya kulima kilimo cha kisasa na chenye tija ambacho
kitawasaidia kupata mavuno mengi pamoja na kusambaziwa pembejeo za kilimo ambazo
ni bora zaidi na hazitakuwa na changamoto kwenye kilimo chao, ikiwamo Mbegu na
madawa ya kuulia wadudu.
Ofisa
wa shirika la Bima la taifa kutoka makao makuu jijini Dar es salaamu Prosper
Peter kitengo cha Magari na Kilimo akitoa Tahadhari kwa wakulima watakaojiunga na
bima hiyo, kutotengeneza matukio ya kutofuata Sheria na Kanuni za kilimo
iliwapate kulipwa fidia ambapo ikibainika hawatolipwa
Ofisa wa Bima ya Taifa kutoka mkoani Shinyanga Stella Paulo kitengo cha Bima za Mali na
Ajali, akitoa elimu kwa wakulima hao juu ya umuhimu wa kujiunga na Bima za
majanga ya moto, na kutoa mfano kunaweza kutokea nyumba zao kupata ajali za moto
ama makazi yao au sehemu zao za biashara kuteketea ambapo wataweza kufidiwa kwa kujengewa
nyumba mpya na kuwarudisha katika hali zao kama zamani.
Kaimu meneja wa Shirika la Bima ya Taifa Mkoani
Shinya nga Fred Magesa akitoa historia ya Bima la Taifa lilivyo anza, kuwa Shirika hilo mwaka 1963 ndipo lilipoanza kwa
muungano wa Tanganyika na makampuni ya kigeni na kuitwa shirika la bima la Tanganyika, lakini mwaka 1965 baada ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar likawa Shirika la Bima laTanzania, na mwaka 1967 baada ya azimio la Arusha Serikali ilitaifisha hisa zote na shirika hilo kumiliki hisa hizo kwa asilimia 100 na kubaki kuwa mali ya serikali, na hivyo kuwataka watanzania walitumia shirika hilo kwa
kuwa wazalendo kwa kupenda vitu vya nyumbani na siyo kwenda kukata bima kwenye
mashirika binafsi ilikuweza kuchangia pato la taifa ambalo litasaidia kutatua
matatizo ndani ya jamii, ikiwamo miundombinu ya barabara ,huduma za Afya ,elimu
Nk.
Mkulima
Skolastika Laurent akiipongeza Serikali kwa kuthamini wakulima wadogo
kutaka kuwainua kiuchumi, na kubainisha kuwa bima hiyo itakuwa msaada mkubwa
kwao, ikiwa kuna baadhi ya misimu ya kilimo imekuwa ikiwatia hasara kwa kukosa
mavuno sababu ya mabadiliko ya tabia nchi.
Mkulima wa Kata ya Kagongwa wilayani Kahama Merry
Bukwimba akiuliza swali kwenye semina hiyo ya Elimu ya Bima, namna
watakavyokuwa wakifaidika na Pembe Jeo ya Mbegu za kilimo ambapo kumekuwa na
tatizo hilo kwa wakulima kuuziwa mbegu zisizo na ubora na kusababisha kutoota
na kuwatia hasara, na kupewa majibu kuwa wale wakulima wataojiunga na Bima hiyo ya Kinga ya Mazao watakuwa
wakisambaziwa mbegu na mawakala kutoka Bima ya Taifa ambao watakuwa wakifanya
nao kazi.
Mwenyekiti wa kikundi cha TAMAKIWAKA Rachel Malisa ambao wanajihusisha na kilimo
cha Mpunga, Mahindi, Viazi vitamu, Alzet
na ufugaji kuku, akiipongeza Serikali kwa kuwapatia elimu hiyo ya bima dhidi ya
Kinga ya mazao na kuahidi kujiunga iliwapate kuwa salama pale wanapokuwa
wakitegemea kilimo kuwainua kiuchumi.
baadhi ya Wakulima kutoka Kagongwa wilayani Kahama wakisikiliza Elimu ya Bima ya Kinga ya Mazao kutoka Shirika la Bima la Taifa
Wakulima wakifuatilia kwa makini umuhimu wa kujiunga na Bima ya Kinga ya Mazao
Mwenyekiti wa Kijiji cha Iponya Kata ya Kagongwa
wilayani Kahama Joint Wiliamu akifungua semina hiyo ya elimu ya Bima ya Taifa
kwa wakulima wa Kagongwa, na kuwataka wakulima hao wajiunge na Bima hiyo ya
Kinga ya Mazao, ilikuwa kuwa komboa na janga la umaskini pale mazao yatakapogoma
kutoa mavuno ya uhakika na kuwasisitiza elimu hiyo waliyoipata wakawe mabarozi
wazuri kwa wenzao ambao hawajafika kupewa elimu hiyo.
Na Marco Maduhu