KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA HESABU ZA SERIKALI (PAC) KUIWEKA KIKAANGONI TBA
Kamati ya kudumu ya Bunge ya hesabu za serikali (PAC), imesikitishwa utendaji kazi mbovu wa wakala wa majengo Tanzania (TBA), kwa usimamizi wake mbaya wa miradi Serikali ambayo imekuwa ikijengwa chini ya kiwango.
Kamati imebaini mapungufu hayo ya (TBA) march 28 mwaka huu wakati ilipofanya ziara yake mkoani Shinyanga, ya kukagua thamani ya matumizi ya fedha kwenye miradi ya Serikali na kubaini kwenye ujenzi wa hospitali mpya ya Rufaa ya mkoa huo, kuna mapungufu mengi huku Mkandarasi akilipwa fedha bila ya kukamilisha ujenzi.
Kamati hiyo ikongozwa na makamu mwenyekiti Aeshi Hilaly ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Sumbawanga, imesema kutokana na wakala huyo wa majengo (TBA) kuonyesha utendaji wake wa kazi kuwa mbovu wa usimamizi wa miradi ya jenzi za Serikali, hivyo wanatarajia kuwaita kwenye kikao mjini Dodoma na kuwahoji.
“Ili mkandarasi apate kulipwa pesa zake lazima (TBA) ambaye ndiye mshauri wetu wa majengo wa miradi ya Serikali ajiridhishe kwanza ndipo aweze kulipwa, lakini tumeona kunatatizo tokea Mwanza tunakumbana na changamoto hizo hizo na hapa Shinyanga imekuwa hivyo hivyo, (TBA) hawaitendei haki Serikali,”Amesema Hilaly
Ameongeza haiingii akilini mkandarasi ashindwe kutekeleza mradi wa ujenzi wa hospitali hiyo ya Rufaa ya mkoa wa Shinyanga na kisha kuvunjwa kwa mkataba wake, lakini wakala huyo wa majengo (TBA) ana idhinisha alipwe pesa na hatimaye kulipwa shilingi 1,164,400,835.60 fedha ambazo zimepotea.
Nao baadhi ya wajumbe wa Kamati hiyo akiwamo Mbunge Allani Kiula wa jimbo la Iramba Mashariki, amesema ujenzi huo wa hospitali mpya ya Rufaa ya mkoa wa Shinyanga una mapungufu makubwa, ambapo tangu awali haukufanyiwa upembuzi yakinifu wa usanifu wa kina ikiwa majengo yake yapo chini ya kiwango.
Kwa upande wake katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga Albert Msovela akisoma taarifa ya ujenzi wa hospitali hiyo ya Rufaa ya mkoa wa Shinyanga ambayo ipo kwenye Kata ya mwawaza mjini humo, alisema ulianza kutekelezwa katika mwaka wa fedha (2013/14) chini ya Kampuni ya M/S STANCE TECHINICAL AND CIVIL ENGENERING LTD.
Amesema mradi huo ulianza kujengwa rasmi March 28/ 2014 na ulitarajiwa kukamilika Novemba 11/2014 kwa gharama ya shilingi 900.799,180.00, lakini katika kutekeleza mradi huo gharama ziliongezeka na kufikia Shilingi 1,120,107,943.35 ikiwa ni ongezeko la Shilingi 219,308,763.35.
Amebainisha sababu za ongezeko za gharama hizo ni kutoka na hali ya udongo na mwinuko wa ardhi wa eneo la ujenzi, upimaji upya wa ujenzi wa nguzo wima, mlalo na slab, upimaji upya wa ukuta,paa na finishing, na kubaishi mkadarasi huyo pia alishindwa kukamilisha kazi kwa wakati na kuomba aongezewe muda.
Ametaja sababu hizo kuwa ni Kuchelewa kuunganishiwa maji na Shuwasa, Kuwapo na ardhi ya mwamba iliyo sababisha shughuli za uchimbaji msingi kuchukua muda mrefu, na kuongezeka kwa ukubwa wa baadhi ya kazi zilizoko ndani ya mkataba(Variations) ikiwamo Vigae,Lipu pamoja na Rangi.
Aidha Msovela amesema licha ya kumuongeza muda mkandarasi huyo alishindwa kufanya kazi yake kwa wakati licha ya jitihada za kushauriana na wakala wa Majengo (TBA) Kumlipa pesa zake ili akamilishe kazi lakini alishindwa na kuamua kuvuja mkataba naye April 12/2017.
Amesema baada ya kuvunja mkataba na mkandarasi huyo ambaye ameshalipwa shilingi 1,164,400,835.60, mkoa uliingia mkataba na kampuni ya Suma JKT,ilikumalizia kazi zilizobaki, ambazo ni mfumo wa maji taka na maji safi, uwekaji masinki ya vyoo na kunawia.
Ametaja kazi zingine kuwa ni uwekaji wa viage,ujenzi wa lampu, ngazi ya kupandishi wagonjwa, ujenzi wa kuchomea taka, pamoja na kuendelea na kazi nyingine ambazo hazikuwepo kwenye mkataba kadri fedha zinapopatikana kuto hadhina, na kubainisha kazi za ujenzi wa hospitali hiyo bado zinaendelea.
Amesema mkataba wa mkadarasi huyo wa Suma JKT atalipwa shilingi 206,585,222.70 ambapo jumla kuu ya gharama za mradi huo hadi kukamilika kwake ni Shilingi 1,625,894,990.88.
TAZAMA MATUKIO KATIKA PICHA HAPA CHINI
Makamu mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge ya hesabu za Serikali (PAC) Aeshi Hilaly ambaye pia ni mbunge Jimbo la Sumbawanga, akizungumza kwenye kikao cha watendaji wa Serikali mkoani Shinyanga, na kubaini kuwepo na usimamizi mbovu wa fedha za serikali kwenye suala la ujenzi wa miradi ambayo ina simamiwa na wakala wa majengo wa Serikali Tanzania (TBA).
Katibu tawala mkoa wa Shinyanga Albert Msovela akisoma taarifa ya mkoa kwenye Kamati hiyo ya kudumu ya bunge ya hesabu za Serikali PAC.
Mkurugenzi wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Shuwasa mjini Shinyanga Eng. Silvester Mahole akisoma taarifa kwenye Kamati hiyo ya Kudumu ya Bunge ya hesabu za Serikali (PAC) na kuelezea kuwa changamoto ambayo wanakabiliana nayo kwenye utoaji wa huduma hiyo ya maji ni madeni ambayo wanazidai taasisi za Serikali ikiwamo Magareza,Polisi na Jeshi la wananchi JWTZ jumla ya Shilingi Milioni 700.9. changamoto ambayo iliahidiwa kufanyiwa kazi.
Mwenyekiti wa bodi taifa VETA Peter Maduki akiwasilisha taarifa ya Veta Shinyanga, amebainisha kuwapo na ufinyu wa bajeti na hivyo kushindwa kurekebishwa miundombinu yake ikiwamo kuongeza madarasa,uzio,upungufu wa dhana za kufundishia ,ambapo kwa mwaka wa fedha 2016-17 chuo hicho kilipanga kutumia shilingi Milioni 614,900,000, lakini kutokana na ukomo wa bajeti kikapangiwa Shilingi 535,913, na fedha ambazo zimepokelewa hadi sasa ni Shilingi 481,804,433.
Makamu mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge ya hesabu za Serikali (PAC) Aeshi Hilaly ambaye pia ni mbunge Jimbo la Sumbawanga mkono wa kushoto akiwa na Naibu waziri wa maji na umwagiliaji Jumaa Aweso wakisikiliza uwasilishwaji wa taarifa hizo pamoja na kupitia makabrasha.
Wajumbe wa Kamati ya kudumu ya bunge ya hesabu za Serikali (PAC) wakisikiliza taarifa hizo tatu pamoja na kupitia makabrasha ya taarifa ambazo hutolewa kwao.
Wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya hesabu za Serikali wakiendelea kusikiliza na kupitia taarifa ambazo huwasilishwa kwao kutoka kwa Katibu tawala mkoa wa Shinyanga Albert Msovela, Mkurugenzi wa mamlaka ya maji Shuwasa Eg Silvester Mahole na Mwenyekiti wa taifa wa bodi ya Veta Peter Maduki.
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya bunge ya hesabu za Serikali (PAC) wakiendelea kusikiliza taarifa hizo.
Taarifa hizo tatu zikiendelea kusikilizwa.
Wajumbe wa kamati ya kudumu ya bunge ya hesabu za Serikali ( PAC) wakiendelea kusikiliza taarifa hizo na kuzifuatilia kiundani, ambapo wakwanza kulia ni Omari Kigue mbunge wa jimbo la Kilindi katikati ni Haji Mponda mbunge wa jimbo la Malinyi akifuatiwa na Mbunge wa jimbo la Bagamoyo Shukuru Kawambwa.
Wajumbe wa kamati ya kudumu ya bunge ya hesebu za Serikali (PAC) wakiwa makini na taarifa hizo tatu ambazo zinawasilishwa kwao.
Mbunge Allani Kiula wa jimbo la Iramba Mashariki, akihoji juu ya taarifa ambayo imesomwa na Katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga juu ya ujenzi wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga, na kuonekana kuna pesa ambazo mkandarasi amelipwa na wakati hakukamilisha kazi huku mkataba wake ukivunjwa, chini wakala wa majengo wa Serikali Tanzania (TBA) na kupewa majibu mepesi ambayo hayakulizisha kamati hiyo.
Mbunge wa viti maalumu mkoani Dodoma Felista Bura akichangia kwenye taarifa hizo na kuishangha Kampuni ya Suma Jkt nayo kushindwa kukamilisha jengo la hospitali hiyo ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga kwa wakati.
Mussa Mbarouk mbunge wa jimbo la Tanga mjini ambaye ni mjumbe wa Kamati hiyo ya kudumu ya bunge ya hesabu za Serikali (PAC)akichangia kwenye taarifa hiyo ya katibu tawala ambayo ndio ilionekana kuwa na changamoto kwenye usimamizi wa ujenzi wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga ,kuwa watu ambao wanashindwa kusimamia na kutekeleza miradi vizuri ya Serikali wachukuliwe hatua kali za kisheria, huku naye akiwanyooshea kidole (TBA) kwa usimamizi wao mbovu wa miradi hiyo ya ujenzi wa Serikali.
Watendaji wa Serikali mkoani Shinyanga wakiandika mawili matatu kwenye kikao hicho .
Watendaji wa Serikali Secretality ya mkoa wa Shinyanga nao wakisikiliza ushauri na maoni ya uchapakazi kutoka kwa wajumbe wa kamati hiyo ya kudumu ya bunge ya hesabu za Serikali( PAC).
Wajumbe wa bodi ya maji ya Shuwasa nao wakiwa kwenye kikao hicho wakiwa na Mkurugenzi wa mamlaka hiyo ya maji Eng Silvester Mahole wa kwanza mkono wa kulia.
Watendaji wa Serikali mkoani Shinyanga wakiwa kwenye kikao hicho.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Wafanyakazi wa chuo cha ufundi Stad Veta nao wakiwa kwenye kikao hicho
Naibu waziri wa maji na umwagiliaji Jumaa Aweso akitoa shukrani kwenye kamati ya (PAC) kuwa wamekuwa msaada mkubwa sana ndani ya Serikali hasa kwa kudhibiti matumizi mabaya ya fedha kwenye jenzi za miradi ya maendeleo.
Wajumbe wa kamati ya kudumu ya bunge ya hesaba za Serikali (PAC) wakiingia kukagua jengo la hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga ambalo linajengwa Kata ya mwawaza tangu mwaka wa fedha (2013-14) .
Katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga Albert Msovela akitoa maelezo kwa wajumbe hao wa PAC ndani ya jengo hilo la hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Shinyanga.
Ukaguzi wa jengo ukiendelea.
Mbunge wa vitimalumu mkoani Dodoma Felista Bura wa kwanza mkono wa kushoto akionyesha vigae ambayo vimewekwa kwenye jengo hilo la Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Shinyanga kuwa vipo chini ya kiwango na vinatakiwa kutolewa.
Makamu mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge ya hesabu za Serikali (PAC) Aeshi Hilaly mkono wa kushoto akizungumza na Katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga Albert Msovela juu ya ujenzi huo wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga na kuonekana lipo chini ya kiwango kutoendana na thamani ya fedha mbazo zimeshatumika kwenye ujenzi huo.
Wajumbe wa kamati ya kudumu ya bunge ya hesabu za Serikali (PAC) wakoinyeshana nyuza za jengo hilo la hospitali ya rufaa ya mkoa wa shinyanga ambalo bado lipo kwenye ukamilishwaji.
Baadhi ya nyufa ambazo zinaonekana kwenye jego hilo la Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Shinyanga.
Mbunge wa Jimbo la Kilindi Omari Kigua mwenye Tshati Nyeupe akisema ujenzi wa jengo hilo la hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga halikufanyiwa upembuzi yakinifu wa usanifu wa kina kitaalamu, na ndio maana lina mapungufu makubwa ikiwamo na usimamizi mbovu.
Wajumbe wa kamati ya kudumu ya bunge ya hesabu za Serikali( PAC) Wakiwa katika chuo cha ufundi Stad Veta akiangalia mashine ya kutengenezea mitambo.
Mkuu wa chuo hicho cha Veta Mkoani Shinyanga Afridon Mkhomoi akitoa maelezo kwa wajumbe wa Kamati hiyo ya (PAC) Namna mafunzo yanavyotolewa kwa vijana ambao hujifunza chuoni hapo jinsi ya kutengeneza Mitambo.
Wanachuo wakitoa maelezo kwa mbunge wa Jimbo la Malinyi mkoani Morogoro Haji Mponda.
Mbunge wa viti maalumu mkoani Mara Joyce Sokombi akisikiliza maelezo kutoka mwachuo wa Veta Juma Daniel namna wanayojifunza fani ya ufundi wa kutengeneza Magari makubwa.
Mwalimu wa mafunzo ya ufundi wa kuchonga madini ya Vito na Kug'arisha Yona Mwambopa akitoa maelezo kwa wajumbe wa kamati ya kudumu ya bunge ya hesabu za Serikali (PAC) namna wanavyotoa mafunzo hayo.
Mwanachuo Jesca Jonathani akiwa Anag'arisha madini hayo ya Vito.
Mbunge wa jimbo la Kilindi Omari Kigua akiwasalimu wanafunzi wa chuo cha Veta Shinyanga na kuwataka wasome kwa bidii.
Wanachuo cha Veta Shinyanga wakifurahia jambo kutoka kwa Kamati hiyo ya PAC.
Wanachuo wa Veta wakisikiliza Nasaha za wajumbe wa Kamati ya kudumu ya bunge ya hesabu za Serikali( PAC).
Naibu waziri wa maji na umwagiliaji Jumaa Aweso akipiga picha ya Pamoja na wanachuo hao wa Veta Shinyanga.
Makamu mwenyekiti wa Kamati hiyo ya Kudumu ya Bunge ya hesabu za Serikali (PAC) Aeshi Hilaly, akiwa na baadhi ya wajumbe wakipiga picha ya pamoja na wanachuo cha Veta Shinyanga.
Naibu Waziri wa maji na umwagiliaji Jumaa Aweso mkono wa Kushoto, awali kabla ya kuwasili mkoani Shinyanga akiwa anasalimiana na Mkurugenzi wa mamlaka ya Maji Shuwasa mjini Shinyanga Eng, Slivester Mahole.
Naibu waziri wa maji na umwagiliaji Jumaa Aweso akisalimia na wajumbe wa Kamati hiyo ya Kudumu ya bunge ya hesabu za Serikali (PAC) Pindi walipowasili mkoani Shinyanga katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainabu Telack wakwanza mkono wa kulia akisalimiana na Wajumbe hao wa Kamati ya kudumu ya bunge ya hesabu za Serikali (PAC) wakati walipowasili mkoani Shinyanga.
Makamu mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya hesabu za Serikali (PAC) Aeshi Hilaly, akisalimiana na mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainabu Telack wakati walipowasili mkoani humo.
mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainabu Telack akiwakalibisha Wajumbe hao wa Kamati ya kudumu ya bunge ya hesabu za Serikali( PAC) ofisini kwake kabla ya kulekea kwenye kikao katika ukumbi wa mikutano kupokea taarifa ya mkoa na kisha kwenda kuangalia miradi .
Na Marco Maduhu ambaye pia ni mwandishi wa gazeti la Nipashe mkoani Shinyanga.