WAZIRI DR HAMISI KINGWANGALA MGENI RASMI MAADHIMISHO YA UPANDAJI MITI KITAIFA WILAYANI KISHAPU- SHINYANGA



Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainabu Telack akitoa taarifa ya maadhimisho hayo ya upandaji miti kitaifa wilayani Kishapu mkoani Shinyanga kwa waandishi wa habari.
Waziri wa Maliasiri na utalii Dr Hamisi Kigwangala anatarajiwa kuwa mgeni Rasmi kwenye kilele cha madhimisho ya upandaji miti Kitaifa, ambayo yatafanyika wilayani Kishapu mkoani Shinyanga kwa kupanda jumla ya miti 232,000.

Akitoa Taarifa ya maadhimisho hayo ya upandaji miti leo March 28 mwaka huu kwa vyombo vya habari mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainabu Telack, amesema yatafanyika wilayani Kishapu kuanzia April (3-5) mwaka huu, kwa kufanya shughuli mbalimbali za upandaji miti wilayani humo pamoja na kutolewa elimu ya utunzaji wa mazingira kwa wananchi.

Amesema katika maadhimisho hayo Shughuli kubwa itakuwa ni upandaji miti ambapo pia kila familia itakabidhiwa miti kwa ajili ya kupanda kwenye Kaya zao pamoja na kuitunza, lengo likiwa ni kuondoa hali ya Jangwa wilayani Kishapu na kuifanya kuwa ya Kijani.

“Katika maadhimisho hayo siku ya kilele chake April hiyo 5 mgeni rasmi atakuwa waziri wa maliasiri na utalii Dr Hamisi Kigwangala, ambapo naomba wananchi wajitokeze kwa wingi ilitushiriki kwa pamoja kupanda miti, na kupewa elimu ya utunzaji mazingira na faida zake,” Amesema Telack.

Ameongeza licha ya maadhimisho hayo pia mkoa ulishapanda mpaka sasa Miti Milioni 1.6 , ambayo inaendelea vizuri na kutoa onyo kwa wafugaji kuwa makini na mifugo yao ili kutoharibu miti hiyo.

Na Marco Maduhu ambaye pia ni Mwandishi wa gazeti la Nipashe












Powered by Blogger.