MKURUGENZI WA TGNP MTANDAO AFUNGA MAFUNZO YA URAGHBISHI
Mkurugenzi wa Mtandao wa jinsia Tanzania (TGNP) kutoka Jijini Dar es salaamu Liliani Liundi amewataka Waraghbishi waliopata mafunzo hayo kwenda kuyafanyia kazi kwa kuhakikisha wanaleta ukombozi wa kutatua changamoto ndani ya jamii ambazo zinawakabili.
Liundi ametoa Nasaha hizo leo March 7,2018 wakati akifunga mafunzo ya siku Tano kwa Waraghbishi kutoka mikoa mitano ya Kigoma, Shinyanga ,Morogoro, Mbeya na Dar es salaamu,ambao wamejengewa uwezo namna ya kuibua matatizo ndani ya jamii pamoja na kuyatafutia ufumbuzi ili jamii ipate kuishi salama.
“Naomba mafunzo haya mkayatumie ipasavyo kwenye maeneo yenu katika kuibua matatizo ndani ya jamii pamoja na kuyatafutia ufumbuzi,mkalete mabadiliko kwa wananchi, sisi tupo kwa ajili ya kutaka jamii ipate kuishi salama.”amesema Liundi.
Naye Anna Sanga Ofisa program mwandamizi kutoka TGNP alitoa vipaumbele ambavyo vinahitaji kufanyiwa kazi na Waraghbishi hao kwenye maeneo yao licha ya kuibua matatizo mengine kuwa ni Sekta ya Elimu ,Afya, Maji,Kilimo,Umiliki wa Ardhi kwa wanawake, pamoja na Madini.
TAZAMA HABARI PICHA HAPA CHINI
Mkurugenzi wa Mtandao wa Jinsia TGNP Tanzania Liliani Liundi akifunga mafunzo ya Uraghbishi Jijini Dar es salaamu yaliyokutanisha Waraghbishi kutoka mikoa mitano ya Kigoma,Shinyanga ,Mbeya,Morogoro na Jijini Dar es salaamu ambao wataenda kufanya kazi ya kuibua matatizo ndani ya jamii ya kuyatafutia ufumbuzi.
Waraghbishi wakitafakari Nasaha iliyotolewa na mkurugenzi wa TGNP Mtandao Liliani Liundi mara baada ya kufunga mafunzo hayo na kutakiwa kuyatumia kikamilifu ilikuweza kuleta matokeo chanya kwa wananchi juu ya kutatua matatizo yanayowakabili.
Waraghbishi wakiendelea kuchukua mawili matatu juu ya Nasaha za Mkurugenzi wa TGNP Mtandao Liliani Liundi juu ya kwenda kuyafanyia kazi mafunzo hayo ya Uraghbishi ,kuleta ukombozi ndani ya jamii.
Baadhi ya wafanyakazi wa TGNP Mtandao wakiwa kwenye ufungaji wa mafunzo hayo ya Uraghbishi.
Na Marco Maduhu ,Dar es salaam