WAANDISHI WA HABARI WATAKIWA KUJIKITA KUANDIKA HABARI ZA UCHUNGUZI






Waandishi wa habari mkoani Shinyanga wametakiwa kujikita kuandika habari za uchunguzi kwa kuibua matatizo ndani ya jamii, ambayo yamekuwa yakifichika na kutopaziwa sauti, jambo ambalo litawasaidia wananchi kutatulia kero ambazo zimekuwa zikiwakabili sababu ya kukosa sehemu pa kuzisemea.

Hayo yamebainishwa leo March 23/ 2018 na Mragbishi kutoka mtandao wa jinsia Tanzania (TGNP) Annagrace Rwehumbiza, wakati akizungumza na waandishi wa habari mkoani Shinyanga juu ya kusaidia kupaza sauti za wanyonge kupitia kalamu zao, hususani wale ambao wanaishi maeneo ya vijijini.

Alisema waandishi wa habari wanamsaada mkubwa sana ndani ya jamii kwa kupaza sauti za wanyonge kupitia kalamu zao, kwa kuibua matatizo ambayo yamekuwa yakiwakabili wananchi, na hasa kwa kuandika habari za uchunguzi ili jamii ipate kutatuliwa kero zao.

“Naombeni waandishi wa habari mkoani Shinyanga mjikite zaidi kuandika habari za uchunguzi kwa kuibua matatizo ambayo yamekuwa yakijificha ndani ya jamii, hususani kwa wale wananchi wanaoishi maeneo ya vijijini, ambao wamekuwa wakikosa wa kuwapazia sauti na kuendelea kuishi maisha ya shida,”Alisema Rwehumbiza

Aidha alitolea mfano Kata ya Bunambiu iliyopo wilayani Kishapu, ambapo wananchi wake wamekuwa wakikabiliwa na tatizo la mauji kwa kukatwa mapanga hususani pale wanapodai haki zao hasa wanawake, lakini suala hilo wamekuwa wakikaa nalo kimya na kukosa wa kuwa semea huku wakiendelea kuuawa.

Naye mmoja wa wananchi wa Kata hiyo ya Bunambiu Everada Mayuma, alisema wananchi wamekuwa waoga kutoa taarifa za matukio mbalimbali kwa kuogopa kukatwa mapanga, na hivyo kuendelea kuishi maisha ya shida sababu ya vitisho hivyo.

Nao baadhi ya waandishi wa habari Shabani Alley kutoka kituo cha Matangazo Star tv na Malunde Kadama ,mwandishi wa Malunde 1 Blog, waliwatupia lawama wananchi hususani wa maeneo hayo ya vijijini, ambapo wamekuwa waoga kutoa ushirikiano kwa waandishi wa habari kwa kushindwa kuzungumza matatizo yanayowakabili.

Walisema kwa nyakati tofauti kuwa waandishi wa habari hawezi kuchunguza habari bila ya kupewa taarifa (Tipu) juu ya tatizo linalo wakabili wananchi, pamoja na kutozungumza na wahusika waliofanyiwa matukio hayo ya ukatili ama ndugu, ambapo wananchi hao hua hawapo tayari kuzungumza na kuwakimbia waandishi.

Naye mwandishi wa habari Stephen Kidoyayi wa Gazeti laTanzanite, aliwataka wananchi kuachana na tabia za uoga pale wanapotaka kusemewa matatizo yanayo wakabili kupitia vyombo vya habari, bali wawe karibu na media ambazo ndio msaada mkubwa kwao.

Aidha kwa upande mkuu wa wilaya ya Kishapu Nyabaganga Taraba, ambaye pia ni mwenyekiti wa Kamati wa ulinzi na usalama, naye alisema tatizo la wananchi wa maeneo hayo ya vijijini hua ni wagumu kusema matatizo yao, na kubainisha kuwa suala wananchi kukatwa mapanga Kata ya Bunambiu analifahamu,isipokuwa hua wanakosa ushirikiano kutoka kwa wahusika waliofanyiwa matukio hayo ya ukatili.
TAZAMA PICHA HAPA CHINI.


Muraghbishi kutoka Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) Annagrace Rwehumbiza akizungumza na waandishi wa habari mkoani Shinyanga, na kuwataka kutumia kalamu zao kupaza sauti za wanyonge kwa kuandika habari za uchunguzi ilikuibua matatizo yaliyojificha ndani ya jamii ambayo yamekuwa kero kwao iliyapate kutatuliwa.

Mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari mkoani Shinyanga (SPC) Malunde Kadama ambaye pia ni Mmiliki wa mtandao wa Malunde 1 Blog akichangia mada kwenye Warsha hiyo ya siku moja ya waandishi wa habari na (TGNP)Mtandao, Kuwa tatizo la wananchi wa maeneo ya Vijijini hua waoga kusema matatizo ambayo hua yanawakabili na hata kama wakihojiwa na vyombo vya habari hua hawapo tayari kuzungumza na kuwataka wavunje ukimya huo iliwapate kusemewa matatizo yao na kupatiwa ufumbuzi.

Mwandishi wa habari kutoka Star tv Shabani Alley akizungumza kwenye warsha hiyo alitoa mfano kuwa kuna siku moja alipokuwa akifanya kazi(Coverege) maeneo hayo ya vijijini alipokuwa akitaka kuhoji wananchi juu ya tukio husika kila mtu alianza kumkimbia akikataa kuongea na vyombo vya habari na hivyo kumuwia vigumu kufanya kazi yake kwa ufanisi ya kuwatatulia changamoto ambazo zinawakabili.

Muraghbishi kutoka Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) Annagrace Rwehumbiza akielezea changamoto ambazo amekutana nazo kwenye Kata ya Bunabiu wilayani kishapu wakati akifanya kazi ya kuibua matatizo yanayo wakabili kuwa ni Unyanyasaji wa kijinsia, mfumo Kandamizi hasa kwenye suala kilimo ambapo wanawake ndio huenda mashambani huku waume zao wakikesha kucheza Bao,Kunywa Kahawa, Uhaba wa maji, Lugha chafu kwa wauguzi wa afya,miundombinu mibovu ya barabara, ukosefu wa mabweni kwa shule ya sekondari Bunambiu, Wanawake kuuawa kwa kukatwa mapanga, pamoja na Ubabe wa viongozi na kutotatua kero za wananchi.

Mwandishi wa habari wa ITV Frank Mshana akizungumza kwenye Warsha hiyo amewataka pia wananchi kuacha tabia ya uoga kusema matatizo yanayowakabili,bali wawe wawazi iliyapate kutatuliwa na kuishi kwa amani na siyo kukaa kimya.

Mwandishi wa habari wa AZAM TV Stephen Wang'anyi ambaye pia ni Katibu wa Chama cha waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga (SPC) akichangia mada kwenye warsha hiyo.

Waandishi wa habari wakiwa kwenye warsha hiyo ya TGNP Mtandao.

Mwandishi wa habari wa DailyNews Suleiman Shaghata akichangia mada kwenye Warsha hiyo ya TGNP Mtandao na waandishi wa habari mkoani Shinyanga.

Mratibu wa chama cha waandishi wa habari mkoani Shinyanga (SPC) Estomine Henry akizungumza kwenye Warsha hiyo, amewataka wanakikundi wa vituo vya taarifa na maarifa kutoka Kata ya Bunambiu wilayani Kishapu ambao wamepewa mafunzo na (TGNP) kuhakikishiwa usalama wao sababu pale matatizo ama maovu ambayo yatakuwa yakiibuliwa na waandishi wa habari wao ndio watanyooshewa vidole na maisha yao kuwa hatarini kutokana na maelezo kuwa mtu akionekana kihelehe hua ana pewa vitisho ama kukatwa mapanga.

Naye mwandishi wa habari Stephen Kidoyayi wa Gazeti laTanzanite, amewataka wananchi kuachana na tabia za uoga pale wanapotaka kusemewa matatizo yanayo wakabili kupitia vyombo vya habari, bali wawe karibu na media ambazo ndio msaada mkubwa kwao.

Wanakikundi wa vituo vya Taarifa na maarifa kutoka Kata ya Bunambiu wakiwa kwenye warsha ya (TGNP) Mtandao na Waandishi wa habari mkoani Shinyanga.

Waandishi wa habari wakiwa kwenye Warsha.

Mwandishi wa habari Moshi Ndugulile wa Radio faraja (wa kwanza mkono wa Kushoto) akiwa na Mwandishi wa habari wa ITV Frank Mshana kwenye warsha hiyo ya TGNP Mtandao na waandishi wa habari mkoani Shinyanga.

Mwandishi wa habari wa ITV Frank Mshana mkono wa Kushoto, akiwa na Mwandishi wa Nipashe na Shinyanga News Blog Marco Maduhu.

Mwandishi wa habari wa Star Tv Shabani Alley akichangia Mada kwenye Warsha hiyo, huku wa kwanza kulia ni Mwandishi wa Radio Faraja Izack Edward, na aliyepo mkono wa kushoto ni Yohana Emmanuel wa DIVEN FM.

Wanakikundi wa vituo vya taarifa na maarifa kutoka Kata ya Bunambiu wilayani Kishapu wakiwa kwenye Warsha ya (TGNP) Mtandao na Waandishi wa habari mkoani Shinyanga.

Mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari mkoani Shinyanga( SPC) Malunde Kadama, akizungumza jambo wakati wa kufunga warsha hiyo ya Siku moja kati ya (TGNP) Mtandao na waandishi wa habari mkoani Shinyanga iliyokuwa na lengo la kukumbushana na kuwekana sawa namna ya kusaidia wananchi wa maeneo ya vijijini kuwasemea matatizo yanayowakabili kwa kutumia Kalamu zao na kuzitoa taarifa hizo kupitia media wanazofanyia kazi.


Na Marco Maduhu ambaye pia ni Mwandishi wa gazeti la Nipashe


Powered by Blogger.