AGPAHI YAENDESHA MKUTANO WA KUIMARISHA UTOAJI HUDUMA RAFIKI KWA VIJANA



Shirika lisilo la Kiserikali (Agpahi) linalofanya shughuli zake hapa nchini za kuzuia maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi(VVU), na kuhudumia watu ambao walisha athirika na ugonjwa huo wakiwamo na watoto wadogo, limeendesha mkutano wa kuimarisha utoa huduma rafiki kwa vijana, kundi ambalo limekuwa likikabiliwa na changamoto katika makuzi.
Mkutano huo umeendeshwa kwa kushirikisha watoa huduma ya afya, wazazi, walimu, na maofisa maendeleo ya jamii, ambao wote hao wanatoka katika halmashauri Tano za mkoa wa Shinyanga ambazo ni Kishapu, Ushetu, Msalala, Kahama mji, pamoja na manispaa ya Shinyanga.

Akizungumza leo April 3/ 2018 kwenye mkutano huo mratibu wa shughuli za afya ya vijana kutoka Shirika hilo la Agpahi Jane Kashumba, amesema kundi la vijana kwa asilimia kubwa limekuwa likikabiliwa na changamoto katika makuzi, hivyo wakaona ni vyema kukutana na wadau hao kujadiliana na kupanga mikakati namna ya kulisaidia ili lipate kuwa salama.

“Lengo la kufanya mkutano huu na wadau hawa wa huduma za afya, wazazi, walimu na maofisa maendelo ya jamii, ni kuona namna tukakavyo wasaidia vijana katika utoaji huduma rafiki kwao, kuanzia majumbani, mashuleni, sehemu za huduma ya afya, pamoja na serikalini namna ya kuwatoa kwenye dimbwi tegemezi.”Amesema Kashumba.

Ameongeza kuwa mtarajio ya mkutano huo ni kuona vijana wanaondokana na matatizo ambayo yamekuwa yakiwakabili kwenye ukuaji wao hasa rika balehe, ikiwamo kubakwa, mimba na ndoa za utotoni, magonjwa ya zinaa, maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi (VVU), pamoja na kupewa elimu ya kujitegemea na kuwezeshwa.

Pia amewataka wazazi, walimu, na wahuduma wa afya kuvunja ukimya kwa vijana na kuwapatia elimu ya afya ya uzazi mara kwa mara wakiwapo majumbani, shuleni, sehemu za huduma za afya, na kuwa eleza madhara ya kujihusisha kimapenzi wakiwa katika umri mdogo.

Nao baadhi ya wadau hao wa afya waliohudhulia mkutano huo wamelipongeza Shirika hilo la Agpahi kwa kusaidia makundi ya vijana kupatiwa elimu hiyo ya afya ya uzazi kupitia mradi wao wa huduma rafiki kwa vijana, ambao utasaidia kuwakinga vijana kupatwa na matatizo mengi katika makuzi yao likiwamo gonjwa la Ukimwi.

SOMA PIA HABARI PICHA HAPA CHINI


Mratibu wa shughuli za afya ya vijana kutoka Shirika la Agpahi Jane Kashumba, akizungumza kwenye mkutano huo wa kuimarisha utoaji huduma Rafiki kwa vijana ,kuwa vijana ni kundi ambalo linapaswa kusaidiwa katika makuzi yake kuanzia ndani ya familia ,mashuleni na hata kwenye vituo vya kutolea huduma za kiafya ,kwa kupewa elimu ya afya ya uzazi na madhara ya kujiingiza kwenye mahusiano ya kimapenzi wakiwa na umri mdogo.

Wadau wa utaoaji huduma rafiki kwa vijana wakiwa kwenye vikundi wakijadili namna ya kutoa huduma hiyo, changamoto zake pamoja na kuzitafutia ufumbuzi ili vijana wabaki kuwa salama katika makuzi yao na kufikia umri wa utu uzima.

Kundi la walimu likiendelea na majadiliano namna ya kutoa huduma rafiki kwa vijana wakiwapo mashuleni, changamoto zake na kuzitafutia ufumbuzi.

Kundi la watoa huduma wakiendelea na majadiliano kwenye mkutano huo wa kuimarisha utoaji huduma rafiki kwa vijana.

majadiliano yakiendelea.

mjadiliano yakiendelea namna ya kuimarisha utaoa huduma rafiki kwa vijana.

Kundi la wazazi likiwa katika majadiliano namna ya kuimarisha utoaji huduma Rafiki kwa vijana wakiwapo majumbani, changamoto zake na kuzitafutia ufumbuzi.

majadiliano yakiendelea kwenye vikundi.

Kikundi cha watoa huduma ya afya manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye majadiliano namna ya kuimarisha utoaji huduma rafiki kwa vijana kwenye vituo vya afya ikiwamo na kuwapa elimu ya afya ya uzazi, ili kujikinga na magonjwa ya zinaa, ukiwamo na ugonjwa wa ukimwi.

Majadiliano yakiendelea.

Kikundi cha watoa huduma ya afya manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye majadiliano namna ya kuimarisha utoaji huduma rafiki kwa vijana kwenye vituo vya afya ikiwamo na kuwapa elimu ya afya ya uzazi, ili kujikinga na magonjwa ya zinaa, ukiwamo na ugonjwa wa ukimwi.

Kundi la walimu likiendelea na majadiliano namna ya kutoa huduma rafiki kwa vijana wakiwapo mashuleni, changamoto zake na kuzitafutia ufumbuzi.

Frida Paulo ambaye ni mwanakikundi wa utoaji huduma wa afya manispaa ya Shinyanga, akiangalia namna walivyojadili kwenye kikundi chao juu ya Uimarishaji utoaji huduma Rafiki kwa vijana, Changamoto zake na kuzitafutia ufumbuzi, ili vijana wabaki kuwa salama .

Mery Marco akiwasilisha mada ambayo wameijadili kwenye kikundi chao cha wazazi namna ya utoaji huduma rafiki kwa vijana wao pindi wakiwa majumbani, kuwa ni kuvunja ukimya na kuwaeleza elimu ya afya ya uzazi, na kuacha mapenzi katika umri mdogo yakiwamo na madhara yake.


Christina Luhaga ambaye ni afisa maendeleo ya jamii kutoka Kata ya Segese halmashauri ya msalala wilayani Kahama, akiwasilisha mada waliyokuwa wameijadili namna ya utoaji huduma Rafiki kwa vijana, kuwa ni kuwahamasisha wajiunge kwenye vikundi vya ujasiriamali ili waweze kupata mikopo asilimia 5 za halmashauri na kuwaondoa kujihusisha na biashara za ngono hasa kwa vijana wa kike.

Annaneema Ntangwa akiwakilisha kundi la walimu, kuwa wao wataendelea na utoaji elimu ya makuzi, afya ya uzazi na stadi za maisha, kuteuwa walimu walezi ambao watakuwa wakitoa huduma rafiki kwa vijana na kutatua changamoto ambazo zitakuwa zikiwakabili katika mkuzi ya shuleni.

Wadau wa huduma rafiki kwa vijana wakiendelea kusikiliza uwasilishwaji wa mada namna vijana hao watakavyokuwa wakipewa elimu ya afya ya uzazi kuanzia majumbani mwao.

wadau wakiwa makini kusikiliza uwasilishwaji wa mada namna ya kuboresha utoaji huduma rafiki kwa vijana.

wadau wakiwa makini kusikiliza uwasilishwaji wa mada namna ya kuboresha utoaji huduma rafiki kwa vijana.

Mratibu wa shughuli za afya ya vijana kutoka Shirika la Agpahi Jane Kashumba, akichangia mada kwenye uwasilishwaji wa mada hizo na kutaka Clabu za wanafunzi mashuleni ziimarishwe, ambazo hua zinamchango mkubwa katika kuleta mabadiliko kwa vijana, hususani kwenye suala la elimu ya afya ya uzazi.

Richard Wambura ni mwalimu wa shule ya sekondari Ukune halmashauri ya Ushetu, akichangia mada kwenye mkutano huo wakati mada zikiwasilishwa, na kuunga mkono Clabu za wanafunzi mashuleni ziendelee kuimarishwa zaidi, kwani hua zinamchango mkubwa sana kubadili mienendo ya wanafunzi.

Emmanuel Swai ni mwalimu wa Shule ya Sekondari Ngongwa Kahama mji, akichangia mada kwenye mkutano huo amewataka wazazi kuwa na ushirikiano na walimu katika malezi ya vijana kwa mazingira yote ya Shuleni na nyumbani.

wadau wa utoaji huduma rafiki kwa vijana wakiwa kwenye mkutano wa kujadili namna ya kuimarisha huduma hizo kwa vijana na kupanga mikakati jinsi ya kuwafanya wabaki salama katika makuzi yao.


wadau wa utoaji huduma rafiki kwa vijana wakiwa kwenye mkutano wa kujadili namna ya kuimarisha huduma hizo kwa vijana na kupanga mikakati jinsi ya kuwafanya wabaki salama katika makuzi yao.

Mratibu wa kudhibiti ugonjwa wa ukimwi manispaa ya Shinyanga Salome Komba, akiwa kwenye mkutano huo akichukua mawili matatu kwa ajili ya kuyafanyia kazi, ili kuwaokoa vijana na janga la ugonjwa huo ambao ni hatari.

Wadau wa utoaji huduma rafiki kwa vijana wakitafakari namna kuimarisha huduma hizo kwa vijana na kuzitatua changamoto ambazo hua zinawakabili vijana katika makuzi yao.

Na Marco Maduhu ambaye pia ni Mwandishi wa gazeti la Nipashe mkoani Shinyanga




















Powered by Blogger.