WAZAZI KATA YA SEGESE WADAIWA KUWATUMIKISHA WATOTO WAO WA KIKE BIASHARA YA NGONO
Ofisa maendeleo ya jamii Kata ya Segese Halmashauri ya Msalala Wilayani Kahama Christina Luhanya akiwasilisha mada kwenye mkutano wa Agpahi.
SOMA HABARI KAMILI
Ofisa maendeleo ya jamii Kata ya Segese halmashauri ya msalala wilayani Kahama Christina Luhanya, amedai wazazi kwenye Kata hiyo wamekuwa na tabia ya kuwatumikisha watoto wao wa kike biashara za ngono, kwa lengo la kupata fedha za mahitaji kwenye familia zao.
Alisema biashara hizo zimeshamili kwenye Kata hiyo na kuonekana kama kitu cha kawaida, ambapo imekuwa ikifikia hatua mzazi ana muuliza mtoto wake wa kike kuwa mbona leo haendi kutafuta mabwana, kwa madai kuwa ndani hawana pesa ya kununua chakula.
Luhanya aliyabainisha hayo juzi mjini Shinyanga wakati akiwasilisha mada namna ya kuimarisha utoaji huduma rafiki kwa vijana, kwenye mkutano ulioandaliwa na Shirika la Agpahi linalo fanya shughuli za kuzuia maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi(VVU), na kuhudumia watu ambao walisha athirika na ugonjwa huo wakiwamo na watoto wadogo.
“Familia nyingi katika Kata ya Segese akina mama wamegeuza watoto wao wa kike kuwa vitega uchumi, na wamekuwa wakiwaagiza kwenda kutafuta mabwana ili wapate fedha za kununua chakula nyumbani,”alisema Luhanya.
Aidha alibanisha kuwa katika mkakati wao kwenye kikudi cha maofisa maendeleo ya jamii kwenye mkutano huo wa Agpahi wa kuimarisha utoaji huduma rafiki kwa vijana, ni kuendelea kuhamasisha vijana na akina mama kujiunga kwenye vikundi vya ujasirimali, ili wapate mikopo asimia 10 za halmashauri na kuwaondoa kwenye uduni wa maisha.
Nacho kikundi cha wazazi kikiwasilisha mada yao kwenye mkutano huo na mwenyekiti wao Merry Marco, walisema changamoto ambayo imekuwa ikiwakabili kwenye utoaji huduma rafiki kwa vijana, ni uduni wa maisha, mfumo wa utandawazi na kuwadharau wazazi wao na kutokubaliana na hali ya malezi .
Alisema katika utatuzi wa changamoto hizo za makuzi ya vijana kwenye kundi lao, wamebainisha kuwa akina mama wanatakiwa kuvunja ukimya na kuwaeleza watoto wao elimu ya afya ya uzazi, na madhara ya kufanya ngono zembe wakiwa katika umri mdogo, ikiwamo na kupata ugonjwa wa ukimwi.
Kwa upande wake mratibu wa shughuli za afya ya vijana kutoka Shirika hilo la Agpahi Jane Kashumba, alisema wameamua kufanya mkutano huo wa kuimarisha utoaji huduma rafiki kwa vijana, kwa kukutanisha wazazi, walimu, watoa huduma za afya na maofisa maendeleo ya jamii, ili kuokoa kundi hilo ambalo limekuwa likikabiliwa na changamoto katika makuzi yake.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI
Ofisa maendeleo ya jamii Kata ya Segese Halmashauri ya Msalala Wilayani Kahama Christina Luhanya akiwasilisha mada kwenye mkutano wa Agpahi wa kujadili namna ya kuimarisha utoaji huduma rafiki kwa vijana, ilikuwaondolea changamoto ambazo wanakabiliana nazo katika makuzi.
Merry Marco akiwasilisha mada ya kikundi cha cha akina mama kwenye mkutano huo , amesema changamoto ambayo imekuwa ikiwakabili kwenye utoaji huduma rafiki kwa vijana, ni uduni wa maisha, mfumo wa utandawazi na kuwadharau wazazi wao na kutokubaliana na hali ya malezi .
Annaneema Ntangwa ambaye ni mwalimu wa shule ya msingi Kambarage manispa ya Shinyanga akiwasilisha mada kwenye kikundi chao cha walimu, amesema katika suala la utatuzi wa changamoto ya utoaji huduma rafiki kwa vijana wakiwa mashuleni, ni kuteuwa walimu wa malezi na kuwapatia wanafunzi elimu ya afya ya uzazi na kuwaeleza madhara ya kufanya mapenzi katika umri mdogo.
Mratibu wa shughuli za afya ya vijana kutoka Shirika hilo la Agpahi Jane Kashumba, akizungumza kwenye mkutano huo amesema wameamua kufanya mkutano huo wa kuimarisha utoaji huduma rafiki kwa vijana, kwa kukutanisha wazazi, walimu, watoa huduma za afya na maofisa maendeleo ya jamii, ili kuokoa kundi hilo ambalo limekuwa likikabiliwa na changamoto katika makuzi yake.
Wadau wa utoaji huduma rafiki kwa vijana wakiwa kwenye mkutano huo ulioandaliwa na Shirika la Agpahi.
Kikundi cha akina mama kikiwa kwenye mkutano huo wa kuimarisha huduma rafiki kwa vijana.
Kikundi cha walimu kikiwa kwenye mkutano huo wa kuimarisha huduma rafiki kwa vijana.
kikundi cha watoa huduma za afya wakiwa kwenye mkutano huo wa kuimarisha huduma rafiki kwa vijana.
Kikundi cha watoa huduma ya afya wa halmashauri ya manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye mkutano huo wa uimarishaji wa utoaji huduma rafiki kwa vijana.
Wadau wakiwa kwenye mkutano wa uimarishaji wa utoaji huduma rafiki kwa vijana ulioandaliwa na shirika la Agpahi.
Na Marco Maduhu ambaye pia ni mwandishi wa gazeti la Nipashe mkoani Shinyanga.