JESHI LA POLISI SHINYANGA LINAFANYA UCHUNGUZI KIFO CHA MWANAFUNZI
Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga, linafanya uchuguzi kifo cha mwanafuzi wa chuo cha uuguzi kilichopo wilayani Kahama mkoani hapa Henry Mwalongo (48), ambaye amedaiwa alikutwa amekufa ndani ya Kalavati katika Kata ya Kambarage mjini Shinyanga.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa juzi na Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Kamishina msaidizi wa Polisi (ACP) Simoni Haule, kuwa tukio hili lilitokea April 6 mwaka huu majira ya usiku, ambapo ilipofika saa 2;45 Asubuhi ndipo wapita njia wakauona mwili huo wa marehemu ukiwa ndani ya kalavati umefukiwa mchanga.
Alisema mwili huo wa marehemu unadhaniwa kuwa ndani kalaviti hilo ndani ya siku tano ambapo sehemu kubwa ya mwili huo ulikuwa umezamishwa ndani ya mchanga, na hivyo kifo chake kuwa na mashaka, na kubainisha kuwa jeshi hilo linafanya uchuguzi ilikubaini undani wa kifo cha mwanafunzi huyo.
“Baada ya mahojiano na baadhi ya ndugu wa marehemu walisema kuwa marehemu alikuwa na tabia za kunywa pombe kupindukia, na hilo lilikuja kujithibitisha baada ya kumkuta akiwa na chupa ya pombe kali katika mfuko wa koti lake alilokuwa amevaa”,alisema Haule. Aliongeza kuwa maelezo ya ndugu yao hayajitoshelezi kutokana na kifo cha marehemu kukutwa mwili wake ukiwa ndani ya kalavati tena umefukiwa mchanga, na hivyo kuwepo na utata juu ya kifo chake, na kubainisha kuwa upelelezi ukikamilika watatoa taarifa rasmi
Na Marco Maduhu, ambaye pia ni Mwandishi wa gazeti la Nipashe mkoani Shinyanga