Taharuki Shinyanga : ALIYEVAA KIASKOFU NA KUSHIKILIA BIBLIA ,MAJEMBE AZUIA MAGARI BARABARANI,ADAI KATUMWA NA MUNGU
Taharuki ya aina yake imetokea katika
eneo la Sisi kwa Sisi ‘Ushirika’ barabara ya Shinyanga kwenda Mwanza
mjini Shinyanga baada ya mwanaume ambaye hajajulikana jina wala makazi
yake aliyevaa nguo nyekundu za kiaskofu akiwa amebeba silaha za jadi
kusimamisha magari barabarani.
Tukio hilo lililodumu kwa takribani dakika 45 limetokea leo Jumamosi Aprili 7,2018 saa tano asubuhi.
Mwanaume huyo anayekadiriwa kuwa na
miaka zaidi ya 40 alikuwa amevaa nguo nyekundu,kofia nyekundu yenye
msalaba,biblia,mito,midoli,msumeno,baiskeli na majembe yenye mipini ya
nondo.
Mashuhuda wa tukio hilo wameiambia
Malunde1 blog kuwa jamaa huyo alifika katika eneo la Ushirika karibu na
ofisi za halmashauri ya wilaya ya Shinyanga kisha kusimama kwenye eneo
la kuvukia ‘Zebra’ akaanza kusimamisha magari.
“Alifika hapa akiwa amevaa joho
jekundu la kiaskofu pamoja na kofia nyekundu yenye msalaba huku akiwa
ameshikilia biblia,baiskeli,msumeno na majembe,akatandaza barabarani
vitu alivyokuwa navyo akawa anasimamisha magari huku akisema yeye ni Malkia wa Nguvu ametumwa na Mungu kuja Kukomboa nchi ya Tanzania”,wameeleza mashuhuda wa tukio hilo.
Aidha wamesema wakati akisimamisha
magari alisikika akisema bado usiku ,hapajakucha wasiendelee na safari
na kwamba yeye ametumwa kuja kukomboa nchi.
“Alisimamisha kila gari pande zote
mbili,akasababisha foleni ndefu,dereva wa basi la Mgamba lililokuwa
linatoka Mwanza alipogoma kusimama ndipo jamaa akapasua kioo cha mbele
akitumia majembe yake ambayo yamechomelewa nondo”,waliongeza mashuhuda.
Kufuatia taharuki hiyo jeshi la polisi
lilifika eneo la tukio na kumkamata mwanaume huyo ambaye alionekana
kutokuwa na wasiwasi wowote akisema wampeleke tu kwenye vyombo vya
sheria kwani yeye hana kosa bali amekuja kukomboa nchi.
Hata hivyo inaelezwa kuwa jana jamaa huyo ambaye hajulikani ametokea wapi alionekana eneo la Ushirika akiwa amevaa kanzu nyeupe na kofia 'kibaraghashia' na hata juzi alifika katika ofisi za halmashauri ya wilaya ya Shinyanga zilizopo hapo Ushirika.
Hata hivyo inaelezwa kuwa jana jamaa huyo ambaye hajulikani ametokea wapi alionekana eneo la Ushirika akiwa amevaa kanzu nyeupe na kofia 'kibaraghashia' na hata juzi alifika katika ofisi za halmashauri ya wilaya ya Shinyanga zilizopo hapo Ushirika.
Mwanaume aliyevaa nguo nyekundu baada ya
kuvua joho jekundu akiwa amesimama katika eneo la kuvukia Zebra eneo la
Ushirika barabara ya Shinyanga - Mwanza baada ya kuvua joho lake
jekundu na kubakiza tisheti na kaptura nyekundu . Pichani ni vifaa
alivyokuwa navyo ikiwemo baiskeli,mfuko mwekundu,biblia,midoli,biblia na
nguo nyekundu -Picha na Malunde1 blog
Jamaa akichezea mdoli barabarani
Mwanaume huyo akiwa ameshikilia msumeno na jembe akizuia magari yasipite
Jamaa akisimamisha magari
Jamaa akisimamisha mabasi
Jamaa akisimamisha basi
Askari polisi wakimwondoa barabarani jamaa huyo akiwa amevaa nguo nyekundu na kofia yenye msalaba
Askari polisi akiokota vifaa vya jamaa huyo ambavyo ni biblia,mto,nguo na mdoli
Askari polisi akiwa ameshikilia majembe ya jamaa huyo
Askari polisi akiruhusu magari yaendelee na safari
Mwanaume huyo akiwa chini ya ulinzi wa
polisi baada ya kuondolewa barabarani.Nguo nyekundu hapo chini ni joho
lake la kiaskofu alilolivua baada ya kuanza kusimamisha magari
Mwanaume huyo akiwa chini ya ulinzi wa polisi
Mwanaume huyo akipelekwa kwenye gari la polisi
Askari polisi wakimpeleka jamaa huyo kwenye gari la polisi
Mwanaume huyo akipelekwa kwenye gari la polisi
Jamaa akipanda kwenye gari la polisi
Askari polisi akiwa ameshikilia msumeno na majembe mawili ya mwanaume huyo
Jamaa akiwa kwenye gari la polisi
Wananchi wakishuhudia tukio hilo
Mwanaume huyo akiondoka na polisi
Picha kwa hisani ya Malunde1 blog