KATIBU MKUU CHADEMA AZUNGUMZA SABABU ZA MBUNGE BULAYA KUPELEKWA MAHABUSU
Leo April 13, 2018 Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na Katibu wake, Dk. Vincent Mashinji wameondoka katika Kituo Kikuu cha Polisi central baada ya kuripoti, huku Mbunge wa Bunda Mjini, Esther Bulaya ikidaiwa atalala mahabusu kwa ajili ya kufikishwa mahakamani.
Akizungumza na waandishi wa Habari, Mashinji amesema kuwa wameripoti kituoni hapo kama walivyoamriwa na mahakama, lakini wameambiwa Mbunge Bulaya atabaki mahabusu kwa ajili ya upelelezi. “Mbunge Bulaya amebaki mahabusu kwa sababu za kiupelelezi lakini tumeambiwa ataunganishwa katika shauri letu,” -Dk.Mashinji