MBUNGE SHABIBY: NONDO ANA UMAARUFU GANI, MNACHAFUA SERIKALI TU!
Mbunge
wa Gairo (CCM), Ahmed Shabiby, amesema hakuna umuhimu mamlaka za
serikali kutumia vyombo vya habari kuwaita baadhi ya watu kwa ajili ya
kuwahoji kutokana na tuhuma wanazokabiliwa nazo.
Shabiby
amesema hayo Bungeni Mjini Dodoma jana Aprili 12, 2018 huku akitolea
mfano tukio la Mwenyekiti wa TSNP ambaye pia ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu
(UDSM), Abdul Nondo, ambaye aliitwa na Mamlaka ya Uhamiaji kwa ajili ya
kuhojiwa uraia wake, na kusema kwamba vitendo hivyo vinaichafua
serikali kwa kiasi kikubwa.
“Sasa
hivi kuna watu kwenye Utumishi ambao wanafanya mambo ya kuichafua
Serikali ya CCM, kulikuwa na haja gani ya kumita yule kijana Abdul Nondo
kumhoji sijui alete cheti cha kuzaliwa cha bibi cheti cha mjomba, cheti
cha babu? Mamlaka inashindwaje kufanya investigations zake (uchunguzi)
ili kubaini ukweli mapaka iite wanahabari?
“Tunawapa
watu umaarufu wakati kesi ipo polisi, ipo mahakamani, kuna watu wengine
watatumia hiyo kitu kusema Serikali ya CCM ikimtaka mtu inamuomba uraia
wake, sidhani kama Serikali ina haja na mtu mdogo kama yule ambaye hata
hana madhara yoyote,” alisema Shabiby.