MBUNGE MSUKUMA AKAZIA KAULI YAKE SERIKALI IRUHUSU BIASHARA YA BANGI KUUZWA
Mbunge wa jimbo la Geita vijijini Joseph Kasheku (Musukuma) bado anakazia kauli yake ya kuitaka serikali iruhusu biashara ya bangi na mirungi.
Musukuma amesema kuwa bangi ni nzuri kuliko pombe kwani mtu akivuta ana kuwa na nguvu za kufanya shughuli zake huku akidai kuwa hata bungeni kuna viongozi wakubwa wanatumia bangi.
“Mule ndani (bungeni) kuna viongozi wakubwa tu wanavuta bangi, na wakija mule wanakuja na mizuka yao, nilimuomba Spika niwataje akanikataza,” amesema Musukuma kwenye kipindi cha Kikaangoni cha EATV