ALAZIMISHWA KUFUNGA NDOA NA MAITI AMBAYE NI MCHUMBA WAKE MARA BAADA YA KUMUUA








Leo May 23, 2018 nakusogezea stori kutoka Familia ya marehemu Confidence Nwanma ya nchini Nigeria ambaye inadaiwa alichomwa kisu na kuuawa na mpenzi wake katika ugomvi wao, familia ya Marehemu sasa imemtaka jamaa huyo kuandaa harusi ya kitamaduni na maiti ya mtoto wao kabla ya mazishi.


Saliu Ladayo alijisalimisha polisi na kudaiwa kukiri kumuua Confidence katika nyumba yao. Akizungumza na waandishi habari, baba mzazi wa Marehemu, Jude Nwanma amesema kuwa Ladayo lazima achukue mwili wa marehemu na kumpeleka katika kijiji chao ili amuoe kabla kuzikwa.



‘’ Kwetu ni lazima mwanaume aoe maiti ya mwanetu kabla kuzikwa. Lazima tufuate kanuni hiyo kwa kumpelekea maiti katika kijiji kutakapofanyika harusi. Ni lazima alipie mahari maradufu maana alimleta binti yetu akiwa maiti’’ Baba wa marehemu

Aidha Baba wa marehemu alitoa onyo kali kwa kijana huyo iwapo harusi hiyo haitafanyika.

‘’ Lazima atafuata kanuni zote kabla familia yetu kumuacha. La sivyo kila mmoja katika familia ya kijana huyo atafariki kabla kufika umri wa binti yetu aliyefariki. Watafariki sawa na binti yetu.’’ Aliongezea
Powered by Blogger.