SHIRIKA LA AGAPE LAFANYA MKUTANO NA MADIWANI KUMKOMBOA MTOTO WA KIKE KIELIMU
Shirika lisilo la Kiserikali la Agape mkoani Shinyanga, linalotetea haki za watoto ambalo linatekeleza mradi wake wa kutokomeza mimba na ndoa za utotoni mjini hapa, limefanya mkutano wa kujadili kumkomboa mtoto wa kike kielimu.
Mkutano huo umekutanisha Madiwani wa halmashauri ya manispaa ya Shinyanga na baadhi kutoka Shinyanga vijijini, wakiwamo na wakuu wa shule, maofisa maendeleo ya jamii, na ustawi, ambao umefanyika katika ukumbi manispaa ya Shinyanga Kalinjuna Lewis.
Akizungumza leo Mei 10,2018 kwenye mkutano huo Ofisa mradi wa kutokomeza Mimba na ndoa za utotoni Mstapha Isabuda kutoka Shirika hilo la Agape, amesema kutokana na tatizo la Mimba na Ndoa za utotoni mkoani Shinyanga kuendelea kuwa tatizo, hivyo wamekutana na madiwani hao kujadili namna ya kumkomboa mtoto huyo wa kike kielimu.
Amesema madiwani hao wana uwezo mkubwa wa kusaidiana na Shirika hilo kutokomeza Mimba na ndoa za utotoni, ambao wanauwezo wa kutunga na kupitisha Sheria ndogo za kuwabana wazazi ambao wamekuwa na tabia ya kuwa odhesha watoto wadogo kwa lengo la kujipatia mali ama mifugo na hatimaye kukatisha masomo yao.
“Lengo la mkutano huu na madiwani hawa ni kuwaonyesha ukubwa wa tatizo lilipo la wanafunzi kupewa mimba na kukatishwa masomo yao, sababu ya kuodheshwa ndoa za utotoni ili wapate kutunga na kupitisha Sheria ndogo ambazo zitasaidia kutokomeza tatizo hilo,”amesema Isabuda.
“Sheria hizo ndogo zitasaidia kwa kiasi kikubwa kutokomeza tatizo la Mimba na Ndoa za utotoni, sababu sheria ya ndoa ambayo ipo ya mwaka 1971 ina ruhusu mtoto aliyechini ya umri wa miaka 18 kuolewa kwa ridhaa ya mahakama na wazazi, na hivyo kuendelea kuwepo kwa tatizo hilo.”ameongeza.
Pia amewataka madiwani hao pale wanapokuwa wakitenga bajeti zao za halmashauri walipe kipaumbele suala la elimu, hasa kwenye upande wa ujenzi wa matundu ya vyoo na vyumba vya kujistili hedhi wanafunzi, ilikumuokoa mtoto wa kike kutopoteza muda wa masomo pindi atakapokuwa kwenye siku zake.
Naye mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga vijijini Ngassa Mboje ambaye pia ni diwani wa Kata ya Mwalukwa, amesema Baraza la madiwani la halmashauri hiyo wameshatunga na kupitisha sheria ndogo ya kutokomeza Mimba na Ndoa za utotoni.
Amesema katika halmashauri hiyo wameshapiga marufuku Mwananchi kuoa ama kuodhesha Binti bila ya kupewa kibali na uongozi wa Serikali ya kijiji, ambapo watakagua vyeti vya kuzaliwa, na kufuatilia taarifa shuleni kama hasomi, ndipo itolewe ruhusa ya ndoa tofauti na hapo hakuna harusi.
Aidha kwa upande wa madiwani wa halmashauri ya manispaa ya Shinyanga, wamesema suala hilo watalijadili kwenye vikao vyao na kutunga sheria ndogo, ambayo itasaidia kutokomeza mimba na ndoa hizo za utotoni na kumuokoa mtoto wa kike kielimu.
TAZAMA HABARI PICHA HAPA CHINI
Ofisa mradi wa kutokomeza mimba na ndoa za utotoni kutoka Shirika la Agape Mustapha Isabuda, akizungumza kwenye mkutano huo amesema takwimu bado zinaonyesha mkoa wa Shinyanga unatatizo kubwa la Mimba na ndoa za utotoni, ambapo katika mwaka (2015 - 2017) katika halmashauri moja ya wilaya ya Shinyanga vijijini ,wanafunzi 85 walipewa ujauzito na kuacha masomo, na mwaka jana (2017) Katika Kata ya Usanda wanafunzi 10 walipewa ujauzito, na hivyo kuwataka madiwani watunge sheria ndogo za kutokomeza tatizo hilo.
Mkurugenzi wa Shirika la Agape John Myola, linalofanya shughuli ya kutetea haki za watoto, amesema katika mradi wao huo wataendelea kupanua wigo wa kufanya kazi za kutetea haki za watoto hao kwenye Kata nyingi, na kuwaomba wadau wa maendeleo na elimu, kusaidia watoto ambao amekuwa akiwasaidia kupata elimu mara baada ya kukatishwa masomo yao sababu ya kupewa ujauzito, ama ndoa za utotoni, ikiwa wanahitaji misaada zaidi katika kutimiza ndoto zao.
Mastahiki Meya wa manispaa ya Shinyanga Gulamu Hafeez Mkadamu, akizungumza kwenye mkutano huo amelipongeza Shirika hilo la Agape kwa kazi wanazozifanya za kumkomboa Mtoto wa kike kielimu, na kuahidi Serikali itaendelea kushirikiana nalo kwa kuhakikisha tatizo hilo la Mimba na Ndoa za Utotoni linakoma.
Madiwani wakijiandaa na mjadiliano ya nini kifanyika ili kumkomboa mtoto wa kike kielimu kwa kutunga Sheria ndogo, kutenga bajeti ya kujenga matundu ya vyoo na vyumba vya kujistili hedhi, ili mwanafunzi huyo wa kike apate elimu sawa na mtoto wa kiume na kutokosa vipindi darasani sababu ya hedhi, ikiwamo na upatikanaji wa Pedi kwenye vyumba hivyo.
Madiwani wakiwa kwenye mkutano wa kujadili namna ya kumkomboa mtoto wa kike kielimu kwa kutokomeza Mimba na Ndoa za utotoni, likiwamo na suala la upatikanaji wa vyumba vya kujistili hedhi mashuleni.
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga vijijini Ngassa Mboje ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Mwalukwa,akichangia mada kwenye mkutano huo, amesema wao katika halmashauri yao wameshatunga Sheria ndogo ya kukomesha mimba na ndoa hizo za utotoni, kuwa Mwananchi akitaka kuoa ama kuodhesha lazima atoe taarifa kwa Serikali ya kijiji, ambayo ndio itampatia kibali mara baada ya kumaliza kujiridhisha kuwa binti anaye olewa siyo Mwanafunzi wala siyo chini ya umri wa miaka 18, kwa kukagua vyeti vyake vya kuzaliwa na kufuatilia tarifa shuleni kama Asomi.
Mwalimu mkuu wa Shule ya Msingi Twendapamoja katika Kata ya Mwamalili manispaa ya Shinyanga Luhende Lyongo akichangia mada kwenye mkutano huo amesema kinachopaswa sasa madiwani watoe elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa kuwa na vyeti vya kuzaliwa, ilikusaidia mtu ambaye ana taka kuodhesha Binti yake lazima aonyeshe Cheti cha kuzaliwa ilikubaini kama hana umri wa chini ya miaka 14.
Diwani wa Kata ya Chibe halmashauri ya manispaa ya Shinyanga Petro Kisandu, akichangia Mada kwenye mkutano huo amesema halmashauri zote ziungane kupiga vita tatizo hilo la Mimba na Ndoa za Utotoni, kwa kutoa elimu kwa wananchi.
Mkuu wa shule ya Sekondari Dididia Magesa Faustine akizungumza kwenye mkutano huo amesema suala la Mimba mashuleni bado ni changamoto hivyo kunahitaji nguvu ya pamoja kulitokomeza, ambapo mwaka huu (2018), Tayari Wanafunzi Watatu wamepatikana kuwa na Ujauzito.
Mkuu wa Shule ya Sekondari Masekelo manispaa ya Shinyanga Steven Mihambo akichangia Mada kwenye mkutunao huo amesema katika Shule yake mwaka huu kuna Mwanafunzi Mmoja Tayari ana ujuazito wa miezi Mitatu.
Wakuu wa shule za sekondari wakiendelea na mkutano.
Diwani wa Kata ya Lubaga halmashauri ya manispaa ya Shinyanga Obed Jilala akichangia mada kwenye mkutano huo, amesema pia itungwe na Sheria Ndogo ya kuwabana mabinti wa dogo ambao nao wamekuwa wakifanya biashara ya ngono, ilikutokomeza vitendo hivyo ambavyo navyo vimekuwa vikichangia takwimu kuongezeka za Mimba na Ndoa za utotoni mkoani Shinyanga.
Wakuu wa shule za sekondari Manispaa ya Shinyanga na Vijjini wakiwa kwenye mkutano huo, uliondaliwa na Shirika la Agape kwa ajili ya kujadili na kupanga mikakati ya kumkomboa mtoto wa kike Kielimu.
Diwani wa Kata ya kizumbi manispaa ya ShinyangaLubeni Kitinya naye ametilia mkazo suala la kupitisha Sheria ndogo ya kubana wazazi, kuwa akitaka kuodhesha lazima aonyeshe Cheti cha kuzaliwa cha Binti yake ili kujiridhisha kama hana umri chini ya miaka 18 na asomi Shule.
Madiwani wakiwa kwenye mkutano huo wa kutokomeza Mimba na Ndoa za utotoni, ambapo mkono wa Kushoto ni Diwani wa Viti maalumu manispaa ya Shinyanga Mariamu Nyangaka, akiwa na Diwani wa Kata ya Chibe Petro Kisandu.
Mstahiki Meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafeez Mkadamu (mkono wa kulia) akiwa na Diwani wa Kata ya Ndembezi David Kulila ambaye pi ni Mjumbe wa Bodi kutoka Shirika hilo la Agape, wakiwa kwenye mkutano huo wa kujadili namna ya kumkomboa mtoto wa kike Kielimu.
Diwani wa Viti maalum manispaa ya Shinyanga Mariam Nyangaka, akichangia mada kwenye mkutano huo amesema suala la kutokomeza Mimba na Ndoa za utotoni liwe ajenda ya kudumu kupigiwa kelele kwenye mikutano mbalimbali.
Diwani wa Kata ya Ndembezi manispaa ya Shinyanga David Nkulila ambaye pia ni mjumbe wa Bodi wa Shirika hilo la Agape, akichangia mada kwenye mkutano huo ame wataka Madiwani kushikanama pamoja na wananchi kuwa kitu kimoja, ikiwa tatizo hilo siyo la mtu mmoja ambapo kila mtu ana mtoto wake na siku likimtokea kwenye familia yake, binti yake kapewa ujauzito akiwa shuleni ndipo ataona uchungu, ambapo wakati ni sasa wa kupambana kutokomeza tatizo hilo.
Mkutano ukiendelea.
Ofisa mradi wa kutokomeza Mimba na Ndoa za Utotoni kutoka Shirika la Agape Mustapha Isabuda akizungumza kwenye kikao hicho, pia amewataka madiwani hao pindi watakapokuwa wakihamasisha ujenzi wa vyumba vya kujistili hedhi wanafunzi mashuleni, wasisahau na suala la upatikanaji wa vifaa vyake ikiwamo Pedi , na kutolea mfano kuna shule Saba za msingi zina vyumba hivyo vya kujistili hedhi, lakini kunachangamoto ya ukosefu wa vifaa na hivyo kushindwa kumsaidia mwanafunzi anapokuwa katika siku zake za hedhi.
Mkuu wa idara ya maendeleo ya jamii katika halmashauri ya manispaa ya Shinyanga Mwanamsiu Dossi, akichangia mada kwenye mkutano huo amesema Suala hilo la kutungwa kwa Sheria ndogo anatalifikisha kwa Mwanasheria wa halmashauri ili lianze kufanyiwa mchakato.
Mkurugenzi wa halmashauri ya manispaa ya Shinyanga Geofley Mwangulumbi, amesema yale yote yaliyozungumzwa kwenye mkutano huo na kutolewa maoni atayafanyia kazi likiwamo la kutungwa kwa Sheria ndogo na kutokomeza Mimba na Ndoa za utotoni.
Mkutano ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.
Picha ya pamoja mara baada ya mkutano kumalizika.
Na Marco Maduhu ambaye pia ni Mwandishi wa Gazeti la Nipashe mkoani Shinyanga.