WANAFUNZI WAKIKE SHULE YA SEKONDARI SAMUYE SHINYANGA WADAIWA KUPANGA VYUMBA GEST HOUSE
Wanafunzi wakike Shule ya Sekondari Samuye Kata ya Usanda wilaya ya Shinyanga, wamedaiwa kupanga vyumba kwenye nyumba za kulala wageni (Guest house) kama makazi yao kipindi wanapokuwa kwenye masomo, kutokana na kukabiliwa na changamoto ya umbari mrefu kutoka majumbani mwao.
Imeelezwa kuwa wanafunzi hao wanatoka katika vijiji mbalimbali kwenda kusoma kwenye Shule hiyo ya Sekondari Samuye, ambapo wengine wanatoka zaidi ya kilomita kumi na hivyo kulazimika kupanga kwenye Mageto ilikuwa karibu na Shule, lakini baadhi yao wamekuwa wakiishi kwenye nyumba za kulala wageni.
Hayo yalibainishwa jana Mei 9,2018 na Mthibiti ubora wa shule halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Beatus Manumbu, kweye kikao cha wadau wa elimu, viongozi wa dini na baadhi ya watendaji wa Serikali, kilicho andaliwa na shirika la Agape kujadili utatuzi wa changamoto ya uhaba wa vyumba vya kujistili hedhi mashuleni.
Alisema katika suala la kutokomeza ndoa na mimba mashuleni, kumekuwa na changamoto kwa baadhi ya wazazi kutofuatilia maendeleo ya wanafunzi huko walikopanga Mageto, ambapo baadhi yao wamekuwa wakiishi kwenye nyumba za kulala wageni kwa kupangishiwa na wanaume.
“Katika mjadala huu wa kujadili namna ya kutatua changamoto ya kumaliza uhaba wa vyumba vya hedhi mashuleni. pia tusisahau suala la kutokomeza ndoa na mimba mashuleni ambapo baadhi ya wanafunzi wa kike wa shule ya Sekondari Samuye, wanaishi kwenye nyumba za kulala wageni kama makazi yao ,”alisema Manumbu.
"Taarifa hizi nilizipata kwenye kikao cha wazazi katika shule ya Msingi Zagaluba kuwa baadhi ya wanafunzi wa Sekondari Samuye wanaishi kwenye nyumba hizo za wageni," aliongeza.
Naye mtendaji wa Kata ya Usanda Emmanuel Maduhu, alisema kume kuwepo pia na changamoto ya wanafunzi kufanya ngono kwenye mageto waliyopanga, ambapo hivi karibuni mwanafunzi wa kidato cha Tatu katika shule hiyo ya Samuye, alifumwa akiwa ameingiza mwanaume kwenye chumba chake wakifanya mapenzi.
Kwa upande wake kaimu Ofisa elimu Kata hiyo ya Usanda Kenedy Malesa, alikiri baadhi ya wanafunzi kuishi kwenye nyumba za kulala wageni, na kubainisha kuwa suala hilo wameshawaagiza viongozi wote wa Serikali ya vijiji, na kamati za shule kuitisha mikutano na kuwaeleza wazazi wafuatilie maendeleo ya watoto wao mahari wanapoishi.
Aidha Mkurugenzi wa Shirika hilo la Agape mjini Shinyanga la kutetea haki za watoto John Myola, ambao kwa sasa wanatekeleza mradi wa Afya ya uzazi na ujinsia, alisema wamekutanisha wadau hao kujadili kwa pamoja namna ya kutatua changamoto ya uhaba wa vyumba vya hedhi mashuleni, ilikumkomboa mtoto wa kike kielimu.
TAZAMA HABARI PICHA HAPA CHINI
Mthibiti wa ubora wa shule wilaya ya Shinyanga Beatus Manumbu, akizungumza kwenye mkutano huo amesema licha ya vyumba hivyo vya kujistili hedhi kuwepo mashuleni, bali pia na vifaa vyake viwepo na kuwafikia walengwa, pamoja na kugusia suala la wazazi kujenga tabia ya kufautilia maendeleo ya watoto wao mashuleni hasa waliopanga magheto, ikiwa vyumba hivyo wakati mwingine hugeuka Guest house na kupeana ujauzito.
Mtendaji wa Kata ya Usanda Emmanuel Maduhu, alisema kume kuwepo pia na changamoto ya wanafunzi kufanya ngono kwenye mageto waliyopanga, ambapo hivi karibuni mwanafunzi wa kidato cha Tatu katika shule hiyo ya Samuye, alifumwa akiwa ameingiza mwanaume kwenye chumba chake wakifanya mapenzi.
kaimu Ofisa elimu Kata hiyo ya Usanda Kenedy Malesa, alikiri baadhi ya wanafunzi kuishi kwenye nyumba za kulala wageni, na kubainisha kuwa suala hilo wameshawaagiza viongozi wote wa Serikali ya vijiji, na kamati za shule kuitisha mikutano na kuwaeleza wazazi wafuatilie maendeleo ya watoto wao mahari wanapoishi.
Mkurugenzi wa Shirika hilo la Agape mjini Shinyanga la kutetea haki za watoto John Myola, ambao kwa sasa wanatekeleza mradi wa Afya ya uzazi na ujinsia, alisema wamekutanisha wadau hao kujadili kwa pamoja namna ya kutatua changamoto ya uhaba wa vyumba vya hedhi mashuleni, ilikumkomboa mtoto wa kike kielimu.
Mwezeshaji wa mada kwenye mkutano huo Mstapha Isabuda kutoka Shirika la Agape akielezea namna mtoto wa kike anavyohitaji kukombolewa kielimu kupitia jenzi hizo za vyumba vya kujistili na hedhi mashuleni, pamoja na kuwepo wa upatikanaji wa taulo za kike kwenye vyumba hivyo, kwa lengo la kutompotezea mwanafunzi wa kike kukosa vipindi darasani sababu ya hedhi hiyo.
Watendaji wa Serikali kutoka halmashauri ya wilaya ya Shinyanga wakiwa kwenye mkutano huo wa elimu wa Shirika la Agape la kumkomboa mtoto wa kike Kielimu kupitia vyumba vya Kujistili hedhi.
Viongozi wa dini na watendaji wa Serikali kutoka halmashauri hiyo ya wilaya ya Shinyanga, wakiwa kwenye mkutano huo wa kujadili namna ya kuondoa changamoto ya uhaba wa vyumba vya kujistili hedhi mashuleni.
Mchungaji Lameck Makungu kutoka Kanisa la (AICT) Busanda akichukua mawili matatu kwenye mkutano huo na kwenda kuyafanyia kazi,ili kuhakikisha changamoto hiyo ya uhaba wa vyumba vya kujistili hedhi mashuleni kwa wanafunzi linakwisha.
Viongozi wa Kidini na watendaji wa Serikali wakichangamsha mwili mara baada ya kuendelea na mjadiliano kwa muda mrefu namna ya kuondoa changamoto ya uhaba wa vyumba vya kujistili hedhi mashuleni.
Watendaji wa Serikali wakichangamsha mwili mara baada ya kuendelea na mjadiliano kwa muda mrefu namna ya kuondoa changamoto ya uhaba wa vyumba vya kujistili hedhi mashuleni.
Mwezeshaji wa mada kwenye mkutano huo Mustapha Isabuda kutoka Shirika la Agape, akiwataka pia wadau hao wa elimu wakiwamo na viongozi wa kidini pia kuendelea kutoa elimu ndani ya jamii kuachana na tabia ya kuodhesha watoto katika umri mdogo, pamoja na mafataki kuacha kutongoza watoto wadogo na kuwapatia ujauzito ambao hukatisha ndoto zao.
Bahati Mwaipasa kutoka Ofisi ya elimu mkoa wa Shinyanga , akichangia mada kwenye mkutano huo amesema tatizo ambalo limekuwa likisababisha wanafunzi kuendelea kupata ujauzito ni maadili kushuka ndani ya jamii, ambapo pia wazazi hawana tabia ya kuzungumza na watoto wao juu ya kuwapatia elimu ya afya ya uzazi na ujinsia na kujifanya kuwa busy na maisha, na hivyo kuwataka wazazi wabadilike na kuvunja ukimya, ili kuzungmza na watoto wao pamoja na kuwanunulia pedi.
Diwani wa Kata ya Usanda halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Forest Nkole, akichangia mada kwenye mkutano huo, amsema kinacho paswa ni kutoa hamasa kwa wananchi kuchangia jenzi hizo za vyumba vya kujistili hedhi wanafunzi mashuleni ikiwa hilo ni jambo la msingi kwani limekuwa likisababisha taaluma kwa wanafunzi kushuka kutokana na kukosa vipindi madarasani pindi wanapokuwa kwenye siku zao.
Kaimu afisa elimu msingi kutoka halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Irene Kisweka akichangaia mada kwenye mkutano huo amesema kinachopaswa na Serikali kuendele kutenga bajeti ambayo itasaidia kupunguza tatizo hilo la uhaba wa vyumba vya kujistili mashuleni pamoja na wananchi wenyewe kuhamasika kuweka nguvu kazi. ilikuokoa taaluma kushuka ya watoto hao pindi wanapokuwa katika siku zao za hedhi.
Mtendaji wa Kata ya Usanda halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Emmanuel Maduhu akichangia mada kwenye mkutano huo amesema kuwa katika Tarafa yao ya Samuye yenye vijiji 18,amesema kila kijiji wamekubaliana kuchanga Shilingi 631,000 kwa ajili ya kujenga vyumba vya kujistili wanafunzi wa kike na hedhi mashuleni, pamoja na upatikanaji wa taulo (pedi).
Mchungaji Lameck Makungu kutoka kanisa la (AICT) Busanda akizungumza kwenye mkutano huo juu ya kutokomeza mimba na ndoa mashuleni, amesema elimu ya afya hiyo ya uzazi na ujinsia ianzie pia majumbani ili wazazi wapate uelewa na kuvunja ukimya wa kutoa elimu hiyo kwa watoto wao na kuwaeleza madhara ya ngono katika umri mdogo.
Kaimu Ofisa mipango wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Hezron Mwakabonga, akizungumza kwenye mkutano huo kwa upande wa kutokomeza mimba mashuleni, amesema kinachopaswa ni kutolewa elimu ipasavyo ya afya ya uzazi na ujinsia ndani ya jamii pamoja na Clabu za wanafunzi mashuleni, kwa kuelezwa madhara ya ngono katika umri mdogo.
Kaimu Ofisa elimu Kata ya Usanda Kenedy Malesa akizungumzia kwa upande wa kutokomeza Ndoa na Mimba mashuleni, amsema elimu hiyo ya afya ya uzazi inapaswa kutolewa ipasavyo kwa wanafunzi mashuleni ikiwa wazazi wengi siku hizi hua hawana muda wa kuzungumza na watoto wao juu ya madhara ya mapenzi katika umri mdogo wala kuwapatia elimu hiyo ya afya ya uzazi.
Shekhe Soud Ally kutoka msikiti wa Singita Kata ya Usanda, akichangia mada ya kutokomeza mimba na ndoa mashuleni amesema wanafunzi wanapaswa kupewa hiyo ya afya ya uzazi na ujinsia kwa usahihi, pamoja na maadili ya kuvaa mavazi ikiwa wengi wao wamekuwa wakivaa nusu uchi na hivyo kutamanisha wanaume na kufikia hatua ya kuwatongoza.
Afisa kutoka Shirika la (TAI) Paschalia Mbugani amesema tatizo ambalo bado lipo kwa wasichana wa majumbani na mashuleni ni uhaba wa upatikanaji wa Pedi ambapo wao wamekuwa wakizalisha Pedi hizo lakini kwa sasa wamesitisha kidogo na mambo ya kikaa sawa wataanza tena kuzalisha Pedi hizo na kuzisambaza mashuleni mkoa mzima wa shinyanga, ikiwa hapo awali kwa majaribio walianza katika Kata ya Mwalukwa na Pandagichiza.
Watendaji wa Serikali wakiendelea na mkutano.
Ofisa mtetezi wa mradi wa afya ya uzazi na ujinsia kutoka Shirika la Agape Dotto Wayala amesema lengo la mkutano huo ni kuhamasisha uwajibikaji kwa watendaji wa Serikali na viongozi wa kidini kuunganisha nguvu ya pamoja na wadau wa elimu kupanga mikakati ya kumaliza tatizo la uhaba wa vyumba vya Kujistili hedhi wanafunzi mashuleni, pamoja na kutokomeza suala la mimba na ndoa za utotoni.
Mkutano ukiendelea.
Ofisa mradi wa Afya ya uzazi na Ujinsia kutoka Shirika la Agape Lucy Maganga amesema lengo la mradi huo ni kumkomboa mtoto wa kike kielimu kwa kumuondolea changamoto ambazo zimekuwa zikimkabili ili aweze kutimiza ndoto zake.
Wadau wa elimu wakiwamo viongozi wa dini, shirika la Agape na watendaji wa Serikali katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza mkutano wao.
Na marco Maduhu, ambaye pia ni Mwandishi wa Gazeti la Nipashe mkoani Shinyanga.