WAANDISHI WA HABARI SHINYANGA WAIACHIA UJUMBE MZITO SERIKALI
Viongozi wa Klabu ya waandishi wa habari mkoani Shinyanga (SPC) wakiwa na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa huo ikiongozwa na mwenyekiti wake mkuu wa mkoa huo Zainabu Telack wakisimama kwa dakika moja kuwa kumbuka waandishi wa habari waliofariki.
SOMA HABARI KAMILI
Klabu ya waandishi wa habari mkoani Shinyanga (SPC) imeitaka Serikali kutobinya uhuru wa habari ambao ndiyo chachu ya maendedeleo katika nchi ambayo inataka kukua kiuchumi.
Hayo yamebainishwa leo Mei 3,2018 na Mwenyekiti wa Klabu hiyo Kadama Malunde wakati akisoma taarifa ya Klabu kwa mgeni Rasmi mkuu wa mkoa wa Mkoa wa Shinyanga Zainabu Telack kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani ambapo kitaifa yamefanyika Jijini Dodoma huku kimkoa yakifanyika mjini Shinyanga.
Amesema uhuru wa habari ni chachu ya uwajibikaji wa maendeleo katika mkoa ama nchi ambayo inataka kukua kiuchumi na hivyo kuitaka Serikali kutobinya uhuru huo, pamoja na kuingia kwenye chuki na waandishi wa habari ambao wamekuwa wakivichua maovu ndani ya jamii na kufikia hatua hata ya kuhatarisha usalama wa maisha yao.
“Takwimu zinaonyesha katika nchi zilizoendelea mwandishi wa habari anachukuliwa kama nguzo muhimu kwenye kuibua kero na matatizo mbalimbali yanayoikabili jamii ili yaweze kutatuliwa na hatimaye kukua kiuchumi,”alisema Malunde
“Lakini nchi nyingi katika bara la Afrika waandishi wa habari wamekuwa wakichukuliwa kama mahasimu na maadui hali inayosababisha waandishi wa hao kutokuwa huru na hivyo kupunguza ari ya uwajibikaji katika jamii na kudamaa kimaendeleo,”aliongeza.
Pia alitoa wito kwa watendaji na wadau wa habari mkoani Shinyanga kuepuka suala la kubinya uhuru huo wa habari ili mkoa uweze kufikia malengo ya maendeleo yake yaliyokusudiwa likiwamo la uchumi wa viwanda.
Katika hatua nyingine alivitaka vyombo vya ulinzi na usalama, wadau wa maendeleo na viongozi wa kidini kuunganisha nguvu ya pamoja kupiga vita vitendo vya mauaji ya wanawake kuuawa kwa kukatwa mapanga sababu ya Imani za Kishirikina.
Naye mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainabu Telack aliwatoa wasiwasi waandishi hao wa Habari kuwa waendelee kutekeleza majukumu yao kwa nia njema ya kuleta maendeleo kwa nchi katika nyaja zote ikiwa katika ya nchi ya mwaka 1977 inasema kila raia ana haki ya kupata taarifa ,kutafuta habari kwa chombo chochote bila ya kuingiliwa.
Aliwataka waandishi hao pia kujikita kuandika habari ambazo zitakuwa na mguso ndani ya jamii zenye malengo mahususi ya kuhakikisha zinabadilisha maisha yao kutoka hatua moja kwenda nyingine na hatimaye kukua kimaendeleo.
“Mimi kwenye mkoa wangu nitaendele kuzifanyia kazi habari zote ambazo zitakuwa zikitolewa na waandishi wa habari kwa kuzitafutia ufumbuzi ili jamii iweze kuisha salama na kufanya shughuli za kiuchumi na hatimaye kukua kimaendeleo,”alisema Telack.
Kwa upande wake Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Kamishina msaidizi wa Polisi Simon Haule, alipongeza waandishi hao wa habari kwa kushirikiana na Jeshi hilo katika kutoa taarifa za uharifu kupitia vyombo vyao na kuwataka waendelee kufanya kazi zao kwa weledi ilikutokomeza kabisa uharifu huo na mkoa ubaki kuwa salama.
Alisema Jeshi hilo litaendelekuwa shughulikia watu wote ambao wataendelea kutenda masuala ya uharifu likiwamo la mauaji hayo ya wanawake yatokanayo na Imani za Kishirikina, kwa kuwatia nguvuni na kuwafikisha mahakamani ili wapate kuchukuliwa hatua kali za kisheria.
Maadhimisho hayo ya uhuru wa vyombo vya habari hufanyika kila mwaka Mwezi Mei, ambapo mwaka huu yana kauli Mbiu isemayo Uhuru wa habari ni chachu ya uwajibikaji wa maendeleo ya mkoa ,
TAZAMA MATUKIO KATIKA PICHA.
Wadau wa habari mkoani Shinyanga nao wakiwa wamesimama kuwa kumbuka waandishi wa habari waliofariki.
Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari mkoani Shinyanga Kadama Malunde akisoma taarifa kwenye maadhimisho hayo ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari mkoani humo, na kusema Klabu hiyo ina wanachama 38, wakiume 13, wakike 25, na kuitaka Serikali ishirikiana na waandishi wa habari katika kuleta maendeleo na siyo kubinya uhuru wa habari.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainabu Telack akizungumza kwenye maadhimisho hayo ya uhuru wa habari mkoani humo na kuahidi Serikali kuendelea kushirikiana na vyombo vya habari na kutobinya uhuru wa habari kama katiba ya nchi ya mwaka 1977 inavyosema kila raia ana uhuru kwa kutafuta na kupata habari bila ya kuingiliwa ili mradi asivunje sheria ya nchi.
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Kamishina msaidizi wa Polisi Simoni Haule akipongeza waandishi wa habari kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kutumia kalamu zao kuelemisha jamii juu ya kuachana na masuala ya uharifu na hatimaye matukio hayo yamepungua kwa kiasi kikubwa likiwamo la mauaji ya vikongwe ambalo halipo kabisa.
Mchungaji Yohana Nzela kutoka kanisa la KKKT Mjini Shinyanga akimwakilisha Askofu mkuu wa kanisa hilo Emmanuel Makala, aliwataka waandishi wa habari mkoani Shinyanga kujikita pia kuandika habari za watu wa nyonge ilikupaza sauti zao waweze kutatuliwa matatizo yao hasa wa maeneo ya vijijini.
Kanali Justas Kitta akiambatana na kamati ya ulinzi na usalama mkoa naye alitoa Nasaha kwa waandishi wa habari, kuwa wanachuja habari zao kabla ya kuzitoa ilikuona kama zitaharatisha amani ya nchi na siyo kurusha kila habari.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainabu Telack pia aliwataka waandishi hao wa habari kufungua miradi mbalimbali ambayo itakuwa inawaingizia kipato nje ya kazi yao, ilkuondoa changamoto ta kutumika na baadhi ya wadau wenye pesa na hamatimaye kuandika habari za uchochezi ambazo zitahatarisha amani ya nchi.
Naibu Meya wa Halmashauri ya manispaa ya Shinyanga Agnes Machiya akiwataka waandishi hao wa habari kuunda vikundi vya ujasiriamali au saccos ili waweze kwenye kuomba mkopo katika halmashauri hiyo na kuinuka kiuchumi, ili wawe wanaweza kwenda hata vijijini kutafuta habari za wanyonge na kuwapazia sauti, ikiwa wengi wa waandishi hawana mikataba ya ajira na hivyo suala la nauli kwao huwa ni changamoto na hivyo kushindwa kufika maeneo ya pembezoni.
Katibu wa Klabu ya waandishi wa habari mkoani Shinyanga Stephen Wang'anyi akizungumza kwenye maadhimisho hayo ya uhuru wa habari.
Mjumbe wa bodi ya wakurugenzi kutoka (UTPC) Salma Abdul ambao ndio wanachama wenza wa Klabu 28 za waandishi wa habari hapa nchini ikiwamo na ya mkoa wa Shinyanga (SPC) akitoa salama zake aliwataka waandishi wa habari wasiwe wepesi wa kukata tamaa pale wanapokumbana na changamoto katika utendaji kazi, ikiwa wao ndio sauti kubwa ya wanyonge katika kuwasemea matatizo yao ndani ya Serikali.
Mkurugenzi msaidizi wa Radio Faraja iliyopo mjini Shinyanga Anikadhi Kumbemba ambaye pia ni Mwandishi Mwandamizi, akisoma taarifa yake jinsi maadhimisho hayo ya uhuru wa vyomba vya habari yalivyoanza katika historia yake, kuwa ilitangazwa na baraza kuu la umoja wa mataifa UN General Assembly mwaka 1963 kufuatia azimio la la 26 la Shirika la Elimu Sayansi na Utamaduni (UNESCO) la mkutano mkuu mwaka 1991 na hivyo kuazimiwa kila mwaka mwezi Mei kutakuwa na maadhimisho ya uhuru wa vyombo vya habari.
Mkurugenzi msaidizi wa Radio Faraja iliyopo mjini Shinyanga Anikadhi Kumbemba ambaye pia ni Mwandishi Mwandamizi akwasilisha taarifa yake kwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainabu Telack jinsi maadhimisho hayo ya uhuru wa vyombo vya habari histori yake yalivyo anza.
Madau wa habari Chief Abdalla Sube akichangia mada kwenye maadhimisho hayo ya uhuru wa vyomba vya habari mkoani Shinyanga na kutoa pongezi kwao kwa kuutanga mkoa wa Shinyanga na kutoa elimu mbalimbali kwa jamii kupitia vyombo vyao vya habari.
Viongozi wa Klabu ya waandishi wa habari mkoani Shinyanga ,wakiwa na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa huo, meza kuu siku ya maadhimisho ya uhuru wa vyombo vya habari mkoani Shinyanga.
Kamati ya ulinzi na usalama ikiwa kwenye maadhimisho ya uhuru wa vyombo vya habari mkoani Shinyanga.
Mwanishi wa habari kutoka Radio Faraja Faustine Kasala akichangia mada kwenye maadhimisho hayo na kuwataka viongozi pale wanapokuwa wakifanyakazi na waandishi wa habari waache kuwaelekeza namna ya kuandika Angle ya Habari wanayoitaka, bali wawa achie uhuru ikiwa hiyo ndiyo taaluma yao.
Mchungaji David Hamadi kutoka Kanisa la Agape life Church lililopo Lubaga mjini Shinyanga akiwataka waandishi wa habari kuzingatia maadili yao hasa pale wanapopiga picha na kuzurusha hasa kupitia mitandao ya kijamii.
Malaki Philipo mwandishi wa habari wa Radio Free Afrika( Mkono wa kushoto) akiwa na Moshi Ndugulile mwandishi wa habari Radio Faraja.
James Msimba Ng'ombe Katibu wa chama cha Walimu manispaa ya Shinyanga akiwataka waandishi wa habari pia kujiendelea kielimu.
Mkurugenzi wa Shirika la AGape mjini Shinyanga John Myola akipongeza waandishi wa habari kwa kushirikiana na Shirika hilo kikamilifu hasa kwenye kupigania haki za watoto na kupunguza matukio ya mimba na ndoa za utotoni.
Wafanyakazi wa Radio Faraja wakirusha matangazo moja kwa moja Mubashara kwenye maadhimisho hayo ya uhuru wa vyombo vya habari mkoani Shinyanga.
Waandishi wa habari kutoka Radio Faraja Anastazia Paulo mkono wa kulia akiwa na Lucy Masalu wakiwa katika maadhimisho hayo ya uhuru wa vyombo vya habari mkoani Shinyanga.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainabu Telack (Katikati mwenye ushungi) akichukua mawili matatu ya kuyafanyia kazi, siku hiyo ya uhuru wa vyombo vya habari.
Kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Shinyanga nayo ikisikiliza mada kwa makini siku hiyo ya maadhimisho ya uhuru wa vyombo vya habari mkoani Shinyanga hasa kwenye tatizo la kukithili kwa mauaji ya wanawake kwa kukatwa mapanga kutokana na Imani za Kishirikina.
Mwandishi wa habari wa Gazeti la DailyNews Suleiman Shaghata akichangia mada kwenye maadhimisho hayo ya uhuru wa vyombo vya habari.
Waandishi wa habari wakiwa kwenye maadhimisho hayo ya uhuru wa habari.
Mwandishi wa habari Shagwe Thani kutoka Radio Free mkono wa Kushoto, akiwa na Sianel Gelard ambaye ni Ofisa mahusiano ya mamlaka ya maji na usafi wa mazingira Shuwasa mjini Shinyanga, siku ya maadhimisho hayo ya uhuru wa vyombo vya habari mkoani Shinyanga.
Mwenyekiti wa chama cha ACT- Wazalendo mkoani Shinyanga Siri Yasini aliwataka waandishi hao wa habari kuutangaza mkoa hasa kwenye Fursa ya viwanda.
Viongozi wa Klabu ya waandishi wa habari mkoani Shinyanga , wakiwa na kamati ya ulinzi na usalama Meza kuu, siku ya maadhimisho ya uhuru wa vyombo vya habari mkoani humo.
Maadhimisho yakiendelea .
Kamanda wa Takukuru mkoa wa Shinyanga Gasto Mkono akiwataka waandishi wa habari mkoani humo kuanzisha miradi mbalimbali ya maendeleo ilikujikwamua kiuchumi, na kuacha kutumika ili kuandika habari za wanyonge.
Waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga wakiwa kwenye maadhimisho hayo, wa kwanza mkono wa kulia ni Anikazi Kumbemba, mwandishi habari na mkurugenzi msaidizi wa kituo cha Radio Rafaja, Katikati ni Kareny Masasi mwandishi wa Gazeti la Habari Leo, akifuatiwa na Suzy Butondo Mwandishi wa Gazeti la Mwananchi.
Wadau wa habari wakiwa kwenye maadhimisho ya uhuru wa habari mkoani Shinyanga.
Wadau wa habari wakiwa kwenye maadhimisho ya uhuru wa habari mkoani Shinyanga.
Wadau wa habari wakiwa kwenye maadhimisho ya uhuru wa vyombo vya habari mkoani Shinyanga.
Wadau wa habari wakiwa kwenye maadhimisho ya uhuru wa vyombo vya habari mkoani Shinyanga.
Wadau wa habari wakiwa kwenye maadhimisho ya uhuru wa habari mkoani Shinyanga.
Wadau wa habari wakiwa kwenye maadhimisho ya uhuru wa habari mkoani Shinyanga.
Wadau wa habari wakiwa kwenye maadhimisho ya uhuru wa habari mkoani Shinyanga.
Wadau wa habari wakiwa kwenye maadhimisho ya uhuru wa habari mkoani Shinyanga.
Wadau wa habari wakiwa kwenye maadhimisho ya uhuru wa habari mkoani Shinyanga.
Waandishi wa habari wakiwa kwenye maadhimisho hayo ya habari mkoani Shinyanga.
Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari mkoani Shinyanga Kadama Malunde, mkono wa kushoto akiwa na mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainabu Telack wakiteta jambo.
Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari mkoani Shinyanga Kadama Malunde mkono wa kushoto akifurahia jambo wakati akizungumza na mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainabu Telack.
Kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Shinyanga wakiwa kwenye picha ya Pomoja na wadau wa habari mkoani humo mara baada ya kumaliza kuadhimisha siku hiyo ya uhuru wa vyombo vya habari mkoani hapa.
Waandishi wa habari mkoani Shinyanga wakipiga picha ya pamoja na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa huo.
Na Marco Maduhu, ambaye pia ni Mwandishi wa habari wa Gazeti la Nipashe mkoani Shinyanga.